Kwanza nimpe pole sana mshikaji wangu Roma na wenzake kwa madhila waliyoyapata, kwa hakika mashetani haya yameshindwa na yataendelea kushindwa tu.Nayaita maharamia haya mashitani kwa sababu kitendo cha kutekwa na koptezwa kwa msanii huyo kilikua cha kishetani na kiharamia.Niende mbali zaidi kwa kusema kua huenda yalikua magaidi kama walivyo Alshababu.
Baada ya kutoka kule kituo cha polisi ambapo walienda kutoa ushahida,msanii Roma na wenzake waliotoka kuelekea majumbani kuonana na familia zao ingawa waliokua dhoofu bin hali.
Alipoulizwa na waandishi wa habari waliokua wapi?alishikiliwa na nani?amefanyiwa nini?ameona nini na anasemaje? Amesema hawezi kuongea chochote kulingana na masharti ya kuachiwa kwao ispokua mengi atayasema siku ya jumatatu.
SWALI,
1.Hivi ni kweli Roma ataweza kua na ujasiri wa kusema lolote juu ya masharti aliyopewa zaidi ya kuwapgopa watesaji hao? je, kama watesaji walikua ni maharamia tu na sio vyombo vyetu vya dola atapgopa nini kuwataja au kufunguka wazi?
2.Au atasingizia kua anapisha uchunguzi na upelelezi wa kipolisi hivyo hawezi kusema chochote juu ya yaliyompata?
3.Sio ataogopa kupotezwa mazima?Maana juzi hata baada ya msanii Nay wa Mitego kuachiwa tu akasema kua yeye hana chama ilihali umma unaijua kadi yake.
4.Tuna vyombo vyenye dhamana ya kulinda usalama wa raia, Roma awe muwazi tu kuuambia umma tu alikua wapi maana kwa sasa yuko salama na anatambua kua lazima kuanzia sasa awe na tahadhari kubwa.
5.Ujasiri wa Roma Mkatoliki tuujuavyo utakuwepo tena? Au alikua akiongea na kuimba kwa vile hayajawahi kumkuta?Rejea wimbo wake wa "Mkanitupe Segerea"