VIDEO: Msanii Roma na wenzake warejea rasmi uraiani. Kufunguka Jumatatu

VIDEO: Msanii Roma na wenzake warejea rasmi uraiani. Kufunguka Jumatatu

Polisi awe uniformed au kiraia ni lazima afuate TARATIBU.

Katika mazingira ya kukamatwa kina Roma mambo yafuatayo yalitakiwa yakamilike kabla ya wao kukubali wito/kuingia kwenye gari.


1 Wahusika waliofika studio walipaswa kujitambulisha--ni kina nani, na wamefuata nini.

2.Walipaswa kueleza wanampeleka wapi Roma na wenzake.

3.Roma na wenzake walikuwa na haki ya kuwasiliana na ndugu(mke,mzazi, ndugu, wakili, bosi..) zao kuwaeleza "ugeni" walioupata na kinachoendelea.

4.Kabla ya vifaa vya studio kuchukuliwa mwenye studio/mwenye mali alipaswa kutaarifiwa. Hawezi kuja mtu mahali umeajiriwa halafu akachukia vitu vya mwenye mali na wewe uliyekabidhiwa mali hizo uruhusu jambo hilo bila kupata baraka za mwenye mali.

5.Yeyote aliyebaki studio alipaswa kunakili namba za gari iliyoondoka na kina Roma.

6.Kama issue ilikuwa ni kuhitajika kituo cha Polisi, Roma na wenzake walikuwa na haki ya kuomba waende kituoni kwa kutumia usafiri wao wenyewe.
Hayo yote uliyoyaeleza yanawezekana lakini kumbuka kuwa kuna mazingira tofauti mtu anapotiwa nguvuni, yaani kuna mahali mtu anakamatwa "ARRESTED" na kuna mahali pengine mtu anatekwa "KIDNAPPING" sasa mtu anapotiwa nguvuni kwa mtindo wa kwanza hapo ndipo utaratibu wa arresting order au hata search warrant hutumika hapo ndipo hizo taratibu ulizozianisha zinalazimika kuzingatiwa, Sasa ktk mazangira ya kutekwa hali ni tofauti hapa mtu hutiwa nguvuni bila utaratibu wa kisheria tena wakati mwingine under gun point na watekaji kwa sababu wanafanya hivyo kinyume cha sheria hawatoi fursa yoyote kwa kanuni hizo ulizozitaja kuzingatiwa ndio maana hata judge anaweza kutekwa.
 
Watanzania tunaweza kujua ukweli kupitia kinywa cha Roma kuwa alikuwa wapi na kina nani!!!
Kama yeye atahamua kutudanganya watanzania, hatuna budi kumwamini aliko kuwa.
Wengine wote tungesubuli kusikia kutoka kwake yeye mwenyewe.
 
Kaaz kwelikweli!!!

Ndio Tanzania yetu, Matukio ya kuhamisha matukio yanafanyikia kwenye maisha ya watu!!!
Tutarajie kuongezeka kwa magonjwa ya moyo na pia afya ya akili itazototeshwa sana miaka hii!!!

Wenzetu hutengeneza matamasha ili kuhamisha matukio tata yanayosibu siasa zao!!!

Vyombo husika vikiwa havijui.... yuko mtu anajua kinachoendelea.... Nchi hii!!!

Tenga la samaki sote tuko humo tusubiri zamu zetu!!!
 
Ndugu huyo wa Roma ambaye hata hivyo alikataa kutaja jina lake, aliliambia gazeti hili kuwa hadi anafikishwa hospitalini hapo, msanii huyo hakuwa katika hali nzuri.

“Huo ndio ukweli ingawa hatujaruhusiwa kushuhudia mahojiano yao, lakini tumeambiwa kapelekwa… kwa kumwangalia ana mikwaruzo, wengine wapo vizuri, lakini Roma kaathirika zaidi, amehojiwa kama shahidi na si mtuhumiwa, polisi ndio wana taarifa zaidi,” alisema.

Hata hivyo, Kamanda Kaganda hakuwa tayari kuzungumza lolote kuhusu tukio hilo zaidi akisema kuwa hadi watakapotoka hospitali.

Wakili wa Roma aliyejitambulisha kwa jina la Jebra Kambole, alisema mteja wake alikuwa anachechemea na ana majeraha mkononi hali iliyomfanya ashindwe kusalimiana naye.

Wakili huyo wakati akisema hayo naye alikuwa hajapata fursa ya kuzungumza naye.

Zaidi alisema Roma na wenzake walianza kuhojiwa saa nane mchana hadi saa moja usiku kabla ya kupelekwa hospitali.

Hali ya Roma si nzuri, anatetemeka, wenzake wana afadhali kidogo… amehojiwa kama mtu wa kawaida na si muhalifu ili awasaidie polisi katika upelelezi, hadi sasa hakuna shtaka lililofunguliwa dhidi yao, wakimaliza kuangaliwa afya zao wataachiwa huru kwenda nyumbani,” alisema.

Wakati wakili huyo akisema hayo, ofisa mmoja aliyefika kituoni hapo ambaye hakutaka kutaja jina lake gazetini, aliliambia MTANZANIA Jumapili kuwa kuna vitu vimemshangaza kuhusu tukio hilo na kwamba alikuwa akilifuatilia kwa ukaribu.

“Nimetoka humo ndani, lakini kuna vitu sijavielewa, tunataka kuangalia kama ni michezo imechezwa au kweli wanahitaji msaada… tumefanya juhudi nyingi, lakini kuna vitu vimenitia wasiwasi,” alisema ofisa huyo pasipo kuvitaja vitu hivyo.

Ofisa huyo aliliahidi kulipatia gazeti hili taarifa za kina pale atakapokamilisha kulifuatilia jambo hilo kwa kina.

Taarifa zisizo rasmi zilizolifikia gazeti hili, zinaeleza kuwa Roma na wenzake walionekana tangu asubuhi katika mahali ambako hapakuwekwa wazi.

Inaelezwa mtu wa kwanza kupigiwa simu kujulishwa taarifa za kupatikana kwa akina Roma, alikuwa ni Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba.

Hata hivyo, Ruge ambaye alikuwapo kituoni hapo na baadae katika Hospitali ya Mwananyamala, alilitaka MTANZANIA Jumapili kumuuliza suala hilo Roma mwenyewe na si yeye.

Majira ya saa 3:00 usiku, Roma na wenzake wakiwa hospitalini hapo kuchukuliwa vipimo, askari nao walikuwa wakisubiri majibu yake ili kuyawasilisha kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni.

Pamoja na hayo, baadhi ya watu wameanza kuhoji tukio zima la kutekwa hadi kupatikana kwa wasanii hao, wengine wakidai kuwa huenda ni mchezo uliochezwa na kiongozi mmoja. ,....

Wanaohoji hilo, wanatilia shaka kitendo cha Diamond kukutana na kiongozi huyo siku mbili baada ya tukio la utekaji kufanyika na kisha kutoa wimbo mpya siku moja kabla ya wasanii hao kuachiwa huru.

Watu hao wamekwenda mbali na kuhoji hatua ya Babu Tale kuhamasisha wasanii kuungana kuwasaka wenzao na zaidi akidaiwa kuwashawishi wakutane na kiongozi huyo ambaye alikaririwa akisema watapatikana kabla ya Jumapili.
- Chanzo gazeti la Mtanzania

Najaribu kuunganisha dots hapo!!! Kuna mengi mengi zaidi yaliyojificha!!! Napata shaka na khofu hali hii ni miaka miwili tu je miaka mingine miwili ijayo hali itakuwaje?
 
..wangefuata hatua nilizozieleza hapo juu kusingekuwa na mashaka yoyote kama walitekwa na Polisi au wahalifu wengine.
Police wanatekaje RAIA? Mzee unajifananisha na bavicha kwenye kufikiri!
 
Watanzania tunaweza kujua ukweli kupitia kinywa cha Roma kuwa alikuwa wapi na kina nani!!!
Kama yeye atahamua kutudanganya watanzania, hatuna budi kumwamini aliko kuwa.
Wengine wote tungesubuli kusikia kutoka kwake yeye mwenyewe.
Atasema lakini sio sasa wala kesho
 
Cha msingi wamepatikana, bora tu waendelee na life maana kuongea ongea huko unaweza ukateleza ulimi ukajikuta mikono salama bureee!

Kwa sababu, Roma na wenzie waliambia jeshi la polisi kuwa hawajui waliowateka na mahala walipokuwa hawapajui!!
Japo, walisema maneno tu kuwa walichapwa na kuchubuliwa na kuulizwa mambo machache.
 
Nchi hii sijuhi ilikuwaje ikawepo hapa duniani, Mungu wetu ilikuwaje ukatuumba hivi tulivyo sie watanzania. Ni bora lingebaki kuwa pori ukaweka wanyama tu kuliko kuwa nchi ya watu wa hajabu hivi
 
The guy is in shock, anaonekana psychological hayuko okey!!! Inaonekana hatutapata nafasi yakuujua ukweli, ukimsoma vizuri nikama kuna vitisho vikubwa sana kapewa!!!

Mwanashera wake anaonekana kama sio mkongwe sana thats why wame muweka pembeni wakati kisheria anayo room yakusikiliza mahojiano hayo wakati yanaedelea.

ila totaly nimejiridhisha kuwa kunamkono wa serikali ya mkoa katika hili 100% hiyo haikwepeki

Nakubaliana na uchambuzi wako 100%.

Kwa kumwangalia tu huyu kijana unamwona sio yeye, kwa lugha ya kitaalaam unasema ametishwa na akatishika (under fear) na yuko kwenye mtikisiko (shock). Uso wake umesawajika na kutawaliwa na hofu. Na hata lugha na maneno yake ni ya kuchagua la kusema (ni lipi) ili kukwepa kuingia shakani zaidi.

Anadai yuko vizuri wakati anaonekana dhahiri anachechemea. Sasa Je alikuwa anatembea kwa kuchechemea kabla ya kutekwa? Na aliyekuwa vizuri anapelekwa hospitali kufanya nini? Naona na yeye anajisahau kuwa anazughumza na umma (audiance) ya aina gani.

Mwisho wa siku bado nailaumu serikali nzima kwa unyama na dhuluma ya aina hii. This is absolutely un acceptable to our society ...No matter what!
 
Nchi hii sijuhi ilikuwaje ikawepo hapa duniani, Mungu wetu ilikuwaje ukatuumba hivi tulivyo sie watanzania. Ni bora lingebaki kuwa pori ukaweka wanyama tu kuliko kuwa nchi ya watu wa hajabu hivi
Mkuu uwezo wako wa kufikiri ndio upo hivyo?

Watu wa hajabu ndiyo nini kwanza?
 
Kuna uwezekano watekaji sio part ya majeshi yetu ya ulinzi na usalama. Which means ni vijana tu makatili wanaotumiwa kwa ujira na kufanya kazi kwa maelekezo ya mabosi wao wanasiasa.
Lakini inawezekana pia ni vijana waliochomolewa kwenye taasisi yetu ile nyet na kufanya kazi nije ya utaratibu wao rasmi. Afadhali kama ni kundi la kwanza maana kwa jinsi walivyo kanwa na mamlaka rasmi kama ni hilo kundi la pili patakua shida.
From now on kosa dogo kwenye timing yao ndugu zao na taifa litapata hasara maana ni vijana wetu. They are working day and night for safety of this nation na sio kulinda interest za mtu mmoja.
Nimewahi kushuhudia askali wa voda fasta akipigwa hadi kuzimia na mob justice pamoja na bastora yake pale Mindu village morogoro. Hao watekaji wamekanwa na mamlaka zinazo tambulika. And they are not that invisible wasijidanganye, i dont want to imagine what will happen to them siku wakistukiwa.

Hivi hakuna namna ingine which is the best way kusolve What ever the misunderstandings tulizo nazo?
Hii komoana, visasi , kutekana itapelekea maafa kwa victims na hata watesaji wenyewe. Narudia tena they are not that invisible na vijana ambao wanatii amri haramu huku
 
Tanzania inaiacha njia yake, Upendo umekwisha ,amani yatoweka tena kwenye mioyo ya Watu. Mungu tunaomba utusaidie.
 
Back
Top Bottom