Video: Mwanamke adhurika vibaya baada ya kula chips zinazosemekana kukaangwa kwa mafuta ya transfoma

Video: Mwanamke adhurika vibaya baada ya kula chips zinazosemekana kukaangwa kwa mafuta ya transfoma

The unpaid Seller

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2019
Posts
2,360
Reaction score
6,922
Wakuu mko poa,

Kipindi cha nyuma nadhani 2016 wakati Muhongo akiwa waziri aliwahi kupiga marufuku matumizi ya mafuta ya transfoma kwa mapishi ya chips, wakati huo zilikua ni tetesi tu kua kuna wauza chips wasio waaminifu wanatumia mafuta ya transfoma.

Sasa leo nimekutana na video ya simulizi ya mwanadada anaeitwa Agatha ambae inasemekana kua yeye na wenzake walikula chips zilizokaangwa kwa mafuta ya transfoma aise ni huzuni.

Wakuu tuchukue taadhari sana maana kwa hali hii tutadhurika sana. Pia mamlaka zinazohusika na udhibiti ubora wa chakula zifanye tafiti za kina kuhusu tuhuma hizi.

Ikibainika kuna hatia za makusudi kwa wanaofanya videndo hivi wachukuliwe hatua kali.

Tazama video :

View: https://vt.tiktok.com/ZSVUpcd9a/
 
Wakuu mko poa,

Sasa leo nimekutana na video ya simulizi ya mwanadada anaeitwa Agatha ambae inasemekana kua yeye na wenzake walikula chips zilizokaangwa kwa mafuta ya transfoma aise ni huzuni.
Ina maana hao wengine hawakudhurika, kwamba mafuta ya transformer kwenye chips kuna watu yanawadhuru na wengine wanapeta tu?
 
Ina maana hao wengine hawakudhurika, kwamba mafuta ya transformer kwenye chips kuna watu yanawadhuru na wengine wanapeta tu?
kwani hata wanaovuta sigara wote wanaugua mapafu ?! Kwamba kuna watu nikotin ya sigara inawadhuru na wengine haiwadhuru ?! KWAHIYO HATA SIGARA SIO HATARI NA HAINA MADHARA KWA KUA SIO WOTE WANADHURIKA ?!
 
Back
Top Bottom