Video na picha: Waafrika weusi tii walioishi India miaka elfu 60

Video na picha: Waafrika weusi tii walioishi India miaka elfu 60

Hawa jamaa wamechorwa kwenye mawe miaka elfu nne iliyopita..hawa jamaa ni kutoka katika kabila la afars djibuti afrika..
Beja_4.JPG
 

Attachments

  • Beja_4.JPG
    Beja_4.JPG
    17.9 KB · Views: 81
Sina tatizo kwa hilo hata kidogo, sana sana ndo nazidi kupata hamu zaidi! Hadi Papua New Guinea... is a long terrible and dangerous trip hasa tukizingatia enzi hizo hapakuwa na vifaa bora! Sasa hapo ndipo ninapokosa jibu... ni nini hasa kiliwafanya wahatarishe maisha kwa kukata bahari wakati walikuwa na option nyingi tu?! Ni kwamba, kutoka kwenye makazi yao ya asili wakaelekea East na kuchukua mitumbwi wakati, hata kama ni kusaka makazi bora, bado wangeweza kuelekea West/North/South na kuanza kula pori kwa pori kama ilivyokuwa kwa Wazulu ambao hatimae walitua Mkoani Ruvuma! Labda kama walikuwa ni wakazi wa asili wa moja ya visiwa vidogo vya bahari ya Hindi kwenye ukanda wa Afrika Mashariki! Impact ya Mzungu na Mwarabu kuvuruga bahari hadi Afrika inaonekana mpaka leo kwenye uchumi wao... kwamba, walivuruga bahari kutafuta kitu na kitu hicho kinaonekana hadi leo! Sasa hawa ndugu zetu pamoja na kuvuruga bahari bado hawaoneshi ni nini hasa walikuwa wanatafuta hadi ku-risk maisha yao kiasi hicho!
Au waliondoka na meli za wachina waliokuja kufanya biashara
 
I like history,thank you foe bringing this thread.ant time any where kuliko na ishu zinazohusu historia ninaomba kuhusishwa.big up Copenhagen DN,Imhotep and other expert in Historical events and facts
 
Historia kuna wakati inanichangaya sana tatizo wazungu kila kitu wao ndo wanajifanya wagunduz inakera
 
Au waliondoka na meli za wachina waliokuja kufanya biashara
Hii ina-make sense na ninalipa benefit of doubt kwavile hadi sasa hakuna aliyenipa driving force/motivation factor iliyowafanya wahatarishe maisha yao wakati walikuwa wana uwezo wa kufanya migration ya nchi kavu kwa nchi kavu!

Na zamani moja ya labor force iliyokuwa inahitajika sana ni labor force ya kusaidia usafiri wa baharini!
 
tatizo wazungu kila kitu wao ndo wanajifanya wagunduz inakera
Kuna ukweli mkubwa hapo,wazungu walikuwa wanadai mtu mweusi hana uwezo wa kuanzisha ustaarabu wa aina yoyote,lakini walipo gundua majengo ya mawe ya "great zimbabwe" wakasita kidogo halafu wakaja na nadharia ya kuwa kuna makabila ya kizungu yalirudi afrika na kujenga majengo hayo.
 
Hii ina-make sense na ninalipa benefit of doubt kwavile hadi sasa hakuna aliyenipa driving force/motivation factor iliyowafanya wahatarishe maisha yao wakati walikuwa wana uwezo wa kufanya migration ya nchi kavu kwa nchi kavu!

Na zamani moja ya labor force iliyokuwa inahitajika sana ni labor force ya kusaidia usafiri wa baharini!
Mkuu nime confirm uki google ancient chines histoy of trade with africa wameandika kwa mapana sana
 
Great zimbabwe haya majengo deep inside afrika ndio yaliyowafanya wazungu wabadilishe mtizamo halafu wakatengeneza uwongo ya kuwa watu weupe walikuja afrika kuyajenga😀
Zimbabwe-191.jpg
140127172826-great-zimbabwe-unesco-outer-wall-horizontal-gallery.jpg
wall-great-zimbabwe.jpg
 
Visiwa vya andaman vilikabidhiwa kwa serikali ya india na wakoloni wa kiingereza,lakini serikali ya india imepeleka wahamiaji wengi kupita kiasi,hadi kutishia kuwafuta wenyeji ambao ni wajarawa nk.
 
Back
Top Bottom