Uchaguzi 2020 Video: OCD wa Hai amwambia Mbowe hata afanyeje hawezi kumshinda mgombea wa CCM Hai

Hakuna la kushangaza hapa.
Inajulikana toka zamani kwamba wateule wote waliopelekwa Hai waliteuliwa kwa lengo maalum, la kumshughulikia Mbowe.
 
Alafu OCD ana lafudhi ya bwana yule kwahiyo anatetea chama cha kabila lake[emoji1787][emoji1787]

Si hivyo tu bali anaonekana kuongea akiwa na kilevi kichwani na akijiamini 100% na kile alichokuwa anakiongea pasipokujali kuwa kuna watu wanachukua picha ambayo inaweza kuwa ushahidi huko mbeleni

Mara nyingi ukiona Police au Mwajiriwa wa Tume anavunja sheria na kanuni zinzotambuliwa basi elewa kuwa pana kitu ambacho anakitegemea kwani hapa duniani hakuna anayependa kusota mtaani huku familia yake pia ikiteseka
 
Mbowe hilo jimbo mwaka huu hawezi kushinda.
alicho ambiwa ndio ukweli wenyewe hakuna ubishi.
 
OCD atapewa Lawama bure tu.

Mbowe ndio kamchokoza "......Hata mmbebe vipi huyo mgombea hawezi kunishinda"

Mlitaka asijibu aonekane " kaufyata" kama mnavyopublish.

Akaamua kijimwagaa...Sasa atafanyaje!
Acha kutuchana ukweli
 
Huyo OCD angekuwa Semakafu, angetumbuliwa! Lakini kwa vile yeye ni mbereko ya ushindi wa CCM Jimbo la Hai badala ya kutumbuliwa atateuliwa kuwa RPC.
 
Msiwalaumu wanaotumwa wakipoteza ajira zao mtawatetea!! Wasipofanya hivyo watafukuzwa kazi na elimu zao mnazijua hawaajiriki kwingine.Wanatetea mlo wao na watoto wao, lawama ziende kwa wanaowatuma kukagandamiza na kunyanyasa washindani wao wa kisiasa, dawa ni kudai katiba mpya ili timu moja isiwe na mamlaka ya kuchagua na kufukuza kirahisi wasimamizi wa mechi
 
Kosa lake ni kusema Ukweli, na ukweli siku zote huwa haupendwi!

Mbowe kaambiwa ukweli kuwa hata ajipasue pasue hawezi kumshinda Magufuli [emoji23][emoji23]
Kwani Magufuli anagombea ubunge wa Hai? Mafisiem mnakwama wapi?
 

OCD Shinyanga adaiwa kuja na bango la CCM lililochanwa nyumbani kwa mgombea wa ubunge Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA ili kumkamata​

 
Hajui anaongea nanaliyekuwa KUB...hizi shule za sasa kwa kweli
 
Si ajabu uyo afisa baada ya uchaguzi akapewa u-Rpc wa mkoa,hii nchi inachekesha sana
 
Mbowe hajavunja sheria. Mbowe kasema mpinzani wake wa CCM hawezi kushinda. Ana haki ya kusema kuwa mpinzani wake hawezi kushinda.
Ila alisema habebeki.

Hii si kauli nzuri. Ndio maana akaamua kumlipua.
Hapo ilikuwa ni jazba tu.
 
Lakini Mkuu huyu Kamanda amkumbuke yele wa Arusha aliyekuwa akitembea na ilani (Chana R.I.P) Nini kilimpata kabla ya mauti kumfika.
Hii hoja ya mtu kukumbuka aliekufa sijawahi ielewa.

Kwani wewe utaishi milele.
Fanya uovu au mema kumbuka utakufa.
 
Sawa,

Lakini hio ndio hali halisi.
Atajua mwenyewe namna ya kujitetea.
Hatuwezi kuwa na Taifa la watu ambao wanaovunja sheria kwa sababu tu kuna kujitetea.Je mimi ruksa kukuua wewe apo kwa sababu tu nitapewa nafasi ya kujitetea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…