Uchaguzi 2020 Video: OCD wa Hai amwambia Mbowe hata afanyeje hawezi kumshinda mgombea wa CCM Hai

Uchaguzi 2020 Video: OCD wa Hai amwambia Mbowe hata afanyeje hawezi kumshinda mgombea wa CCM Hai

Katika hali ya kushangaza OCD wa Hai ameonekana akimwambia Mbowe hadharani kuwa hawezi kushinda uchaguzi katika jimbo la Hai.

Ikumbukwe kuwa Jeshi la polisi ni miongoni mwa taasisi ambazo zinapaswa kutokuegemea upande wowote katika uchaguzi huu.

Video hii hapa:

View attachment 1593384
Ni tukio la aibu OCD unaapa mtu hatashinda wakat wew si msemaji wa wapiga kura. Unaonyesha mwelekeo, sas huo ni ushaidi wa kutosha kwa Amsterdam atakaotumia.
 
Japo sijasikia vizuri maneno yote, Ila lafudhi ya huyo boss inanifanya nitafakari sana nini kinaendelea.
 
Sawa, huo ni mtazamo wako.

Lakini, Kwa sababu kisheria inakubalika, na ni haki kujitetea sio shida. Maana binadamu si malaika.
Hakuna anaepinga wala kukataa kuwa kujitetea siyo sahihi.Mimi ninachopinga ni kutumia mgongo wa kujitetea kama kisingizio cha kufanya uhalifu
 
Imeonekana Video Fupi inayozunguka ikionyesha Mabishano kati ya Freeman Mbowe na OCD wilaya ya Hai.

Ili Kutenda Haki tujiulize na Kujibu maswali machache:

1. Je, Freeman Mbowe alipaswa kuwepo pale kwa mujibu wa ratiba ya Tume?bila shaka hakupaswa ndio maana anaonekana akisema hata Rais akipita anaweza kusimamishwa, kwa maana hyo aliingilia Ratiba na Alivunja kanunu

2. Mbowe anasikika akimuambia OCD" huyo mnayembeba habebeki' Je? Kwa kiongozi mature na mwenyekiti wa Chama aliyesaini hati ya maadili alipaswa ku-provoke mamlaka inayolinda na Kusimamia mikutano yake?

3. Kitendo cha Mgombea ubunge mbowe kujilinganisha na Rais badala ya kutii ratiba ambayo polisi wanaisimamia ili kuzuia uvunjifu wa amani ni sahihi?

Kwa vyovyote vile busara ilipaswa na inapaswa kuwa Reciprocal, sio sawa kujadili matamshi ya OCD huku tukijifanya hatuoni muenendo wa matukio yaliyopelekea kauli hiyo na Kupishana huki kutokea.

Kama ambavyo Jeshi la Polisi lina wajibu wake lakini vyama vya siasa vina wajibu mkubwa zaidi wa kutii na kuheshimu Ratiba,kanuni na makubaliano waliyoyaweka hasa katika kipindi hiki cha mpito,na Freeman Mbowe hukwepi lawama katika hili.

Nimalizie kwa kusema Hai Vita haitakuwa Lele mama, inaonekana vita Sio nyepesi hata kidogo, Mbowe awekeze kurudisha imani ya Wapiga kura wake na sio confrontation zinazofanya aonekane mwepesi siasani.

#ImeishaHiyo
 
Askari kama huyu ni wakufukuzwa kazi. IGP chukua hatua mapema
 
Kwanini Mbowe alikuwa anamwambia huyo Afisa maswala ya ushindi wake? Hivyo Afisa amemjibu sahihi kabisa! Aliyataka mwenyewe!
Ushindi wa nani? Huyo Lisu mwenyewe wamemtimua huko, video wanazotuletea za nyomi tu hizi zingine za kuzomewa hawaturushii
 
Back
Top Bottom