Uchaguzi 2020 Video: OCD wa Hai amwambia Mbowe hata afanyeje hawezi kumshinda mgombea wa CCM Hai

Uchaguzi 2020 Video: OCD wa Hai amwambia Mbowe hata afanyeje hawezi kumshinda mgombea wa CCM Hai

Hatuwezi kuwa na Taifa la watu ambao wanaovunja sheria kwa sababu tu kuna kujitetea.Je mimi ruksa kukuua wewe apo kwa sababu tu nitapewa nafasi ya kujitetea?
Ni haki kujitetea.
Maana unaweza fanya kitu kwa kutokutarajia.
 
Tulipofikia panaogopesha mno. Hadi askari ana upande aisee!
 
Katika hali ya kushangaza OCD wa Hai ameonekana akimwambia Mbowe hadharani kuwa hawezi kushinda uchaguzi katika jimbo la Hai.

Ikumbukwe kuwa Jeshi la polisi ni miongoni mwa taasisi ambazo zinapaswa kutokuegemea upande wowote katika uchaguzi huu.

Video hii hapa:

View attachment 1593384
Babylon dogs
 
Ila ikitokea hakuna namna.
Ilhali si kwa makusudi, exactly hakuna shida.
Kutenda kosa bila ya kukusudia haitakufanya uwe mtenda kosa mwema wala haitakufanya uwe hujatenda kosa.Usitumia kutenda kosa bila kukusudia kama excuse
 
Msivyopenda kutii sheria bila shuruti, mnawapandisha hasira polisi mpaka wanaamua kusema ya moyoni😂😂😂
 
Kama anapenda cheo na ashaambiwa ahahakikishe Mbowe anadhindwa shida iko wapi? Huu uchaguzi hauwezi kuamuliwa na jazba za polisi Bali mituno ya wagombea, tuachieni wapiga kura tuamue. Hai wamesambazwa makundi hatari ya vijana wanaofadhiliwa na tayari tushawaona Ila NEC kimyaaaa
 
Katika clip inayotembea mitandaoni,inamuonesha OCD Wilaya ya Hai akitoleana maneno na mh Alkael Mbowe Freeman.Mbowe analazimishwa aingie ndani ya gari na aondoke eneo lile ili asiongee na wananchi wapiga kura wake.

Kunachochefua zaidi ni pale OCD anapotumia kinywa chake kutoa maneno ya kwamba "YULE HUMSHINDI, HATA UFANYEJE, HUMSHINDI, NDIVYO UNAVYOWADANGANYA WANANCHI KWAMBA, UTAMSHINDA! NAKUHAKIKISHIA HUMSHINDI"Panda gari uondoke hapa. Haya ni maneno yanayotoka kinuwani mwa huyo KIRAZA anayechafua sifa ya jeshi letu la polisi

Kwa maneno yale,dhahiri wagombea wa FWISIEM sehemu nyingi wanasaidiwa na polisi kutangazwa washindi hata kama siyo chaguo la wananchi walio wengi

Siku zote najiuliza, hawa polisi wanakubali vipi kutumiwa na chama twawala? Kwani wakichaguliwa viongozi toka upande tofauti na CCM, hawa wafunga buti watafutwa kazi? ajira zao si ziko palepale? Ya nini sasa kutumia nguvu nyingi kuwabeba CCM ilihali wakijua wananchi wengi tumeshakichoka hicho chama?

Na hili kosa la UCHOCHEZI liende wapi kama siyo kwa huyo OCD kiraza?Hakufanya uchochezi hapo? Na wananchi wangechachamaa na kumtwanga mawe angemlaumu nani?

Polisi msipokuwa makini kipindi hiki cha uchaguzi,mtakuwa wa kwanza kuvuruga amani yetu na kuleta machafuko nchini.Waacheni wananchi waamue mgombea gani awawakilishe,siyo nyie kutia nguvu na mabavu yenu!

Kama kweli mnatenda haki na mna ubavu, hamuoni ukiukwaji wa sheria,kanuni na taratibu anaoufanya Magufuli? Mbona msianze na huyo?
 
Ila Mbowe yeye anaweza kumwambia Afisa kuwa atashinda hata wakimbeba mgombea wa ccm au? Mbowe ameyataka mwenyewe basi ayaoge!
Mbowe kaongea kisiasa...lazima ajipe matumaini ya kushinda, polisi kaongea kama nani??...anampa nani matumaini ya kushinda au yeye ni mgombea pia? Alipaswa asmjibu mbowe kisiasa, hapo kaharibu na ukizingatia cheo chake kajibu kwa pupa!
 
Katika hali ya kushangaza OCD wa Hai ameonekana akimwambia Mbowe hadharani kuwa hawezi kushinda uchaguzi katika jimbo la Hai..
Huyo OCD, ikumbukwe kwanza kuwa yeye SI MALAIKA, SI MGENI HAPA NCHINI, SI AMSTERDAM na SI "KISIWA", anajua yote yanayoendelea katika siasa na hasa kipindi hiki cha uchaguzi.

Kinachomponza ni hayo mavazi ya kazi, VINGINEVYO, anayo hakiya kutoa maoni yake kufuatana na hali anavyoiona hapo HAI na kwa Mbowe. Asihukumiwe kwa kusema mawazo yake, tatizo ni kuwa kayasema akiwa kwenye hiyo SARE!
 
Back
Top Bottom