Katika clip inayotembea mitandaoni,inamuonesha OCD Wilaya ya Hai akitoleana maneno na mh Alkael Mbowe Freeman.Mbowe analazimishwa aingie ndani ya gari na aondoke eneo lile ili asiongee na wananchi wapiga kura wake.
Kunachochefua zaidi ni pale OCD anapotumia kinywa chake kutoa maneno ya kwamba "YULE HUMSHINDI, HATA UFANYEJE, HUMSHINDI, NDIVYO UNAVYOWADANGANYA WANANCHI KWAMBA, UTAMSHINDA! NAKUHAKIKISHIA HUMSHINDI"Panda gari uondoke hapa. Haya ni maneno yanayotoka kinuwani mwa huyo KIRAZA anayechafua sifa ya jeshi letu la polisi
Kwa maneno yale,dhahiri wagombea wa FWISIEM sehemu nyingi wanasaidiwa na polisi kutangazwa washindi hata kama siyo chaguo la wananchi walio wengi
Siku zote najiuliza, hawa polisi wanakubali vipi kutumiwa na chama twawala? Kwani wakichaguliwa viongozi toka upande tofauti na CCM, hawa wafunga buti watafutwa kazi? ajira zao si ziko palepale? Ya nini sasa kutumia nguvu nyingi kuwabeba CCM ilihali wakijua wananchi wengi tumeshakichoka hicho chama?
Na hili kosa la UCHOCHEZI liende wapi kama siyo kwa huyo OCD kiraza?Hakufanya uchochezi hapo? Na wananchi wangechachamaa na kumtwanga mawe angemlaumu nani?
Polisi msipokuwa makini kipindi hiki cha uchaguzi,mtakuwa wa kwanza kuvuruga amani yetu na kuleta machafuko nchini.Waacheni wananchi waamue mgombea gani awawakilishe,siyo nyie kutia nguvu na mabavu yenu!
Kama kweli mnatenda haki na mna ubavu, hamuoni ukiukwaji wa sheria,kanuni na taratibu anaoufanya Magufuli? Mbona msianze na huyo?