Utaratibu mzuri ni stendi iheshimiwe mabasi yaanzie hapo safari na si yapaki!?,pia ofisi za mizigo ambazo ndio zilikuwa za mabasi zibakie na kazi ya vifurushi,aidha gari ianzie kwenye vifurushi ndipo iende mbezi baada ya hapo ikute booked pesengers ipakie chap isepe!
Kuna vitu vya kufanyia kazi kabla ya kusema haya mambo:
1: Uwezo wa stendi kwa wakati mmoja ni mabasi mangapi ikiamuliwa yapaki pale?
2: Kuanza safari kunalichukua basi husika kutumia muda gani kuwasubiri abiria na mizigo yao na kuwa kwenye gari?
3: Kuna turn around time ya mabasi mangapi kwa siku/kiuwezo wa kutoka nje na kuingia ndani ya stendi kimiundombinu/kutumia barabara zinazotoka na kuingia?
4: Kwa ujumla kuna mabasi mangapi ya mkoani/Kutoka Dsm-Mikoani kwa siku.
5: Je kituo kinamudu tunachokiwazia hata kama magari yasipopaki yote ndani yawe yanaenda kuanza safari?
Mfano: Abood ana gari ngapi kwa Morogoro na foreni yake kuingia na kutoka itamhitaji muda gani ili awasubiri abiria wake wote wapande na awashushe?
NB: Je kituo kinaweza kumudu safari kuanzia pale au kupitia pale.
Suala la msingi ni kupitia pale kama ulivyoeleza beba au shusha mizigo michache iliiyopo na abiria waliopo na uondoke. Jambo mhimu ni kuhakikisha yadi zao zinakidhi mahitaji ya jamii na usalama pia wakati tunatafuta ufumbuzi ulio na tija?
Kama tunatamani na kuhitaji suluhu iwe hivyo wanavyotaka, basi tujiandae kujenga vituo kwa kuzingatia kanda za magari husika na kwa kuzingatia idadi ya watu na miundombinu inayohitajika ndani ya miaka 50 ijayo.
Hii itajibu sayansi, je kituo kina miundombinu toshelevu kwa usalama wa jamii na mabasi?
Je kuna mpangilio toshelevu/salama wa movements ndani ya kituo? Tujiandae kwanza, tusifate mihemko ya kila mtu kutaka suluhiaho kwa njia ya mkato.