Video: Suala la Congo, Watutsi (Banyamulenge) na M23 lachukua sura mpya. Inachanganya sana

Mipaka ya mkoloni ilifànywa kwa makusudi ije kuzua matatizo.

Wagawe uwatawale.
 
Sijui umeandika nini. Hoja yako ni nini? Kwamba kuwaunganisha watusi walioko Congo ndio suluhu? Ok. Mauaji ya kimbari ya Rwanda yalikuwa Watuso na wahutu ndani ya nchi moja kwa hoja yako hiyo walitakiwa kila kabila kiqe nchi yake?
Kwamba umekariri mbinu ya kuwagawanya watu na kuwaibia inafanywa na mataifa ya Ulaya ni moja? Kama Tz wanaiba kwa 84% huoni tatizo ni lile lile kuwa kuna viongozi wananunulika tofauti tu hakuna ufadhiri wa vikundi, na kwanini wafadhili kama wanaweza kuchukua pasipo vurugu?
Unajua Congo nchi ngapi zinaenda kufanya uporaji tofauti na kile unasema wizi unafanyika kwa 84%?

Anyway mawazo yako yana lengo la kuchukia kuibiwa. NIMEYAKUBALI
 
DRC ni mali ya wakongoman, waachwe wakongo na kongo yao.
Rwanda anafuata nini Kongo?:
 
Viongozi waafrika Wanaokubali kufarakanishwa ni sababu ya raslimali za Congo na wao ni wanufaika pamoja na wazungu. Hii ndiyo neo colonialism at work with petty bourgoisie soma kitabu cha silent struggle cha Issa Shivji
 
Ngara yote kigoma yote wale sio wenzetu,murugwanza,rulenge,mukididiri,kumejaa wanyarwanda tu
Hii hoja mfu sana.Kama tumeshakubaliana na mipaka waliyotuwekea Wakoloni basi Mmasai aliye ndani ya mipakaya Tanzania ni Mtanzania na aliyepo Kenya ni Mkenya. Hakuna tena Mtanzania wa Kenya wala Mkenya wa Tanzania. Kama kuna kabila sehemu wapo Rwanda na sehemu wapo Tanzania basi waliopo Rwanda ni Wanyarwanda na waliopo Tanzania ni Watanzania,kama hataki kuwa Mtanzania basi aende ndani ya mipaka ya Rwanda and vise versa.Vivo hivyo kwa Wamakonde,Wanyasa,Wajaluo n.k.
 
Video kwa wale wasio na mihemko na wanaoelewa Kiingereza tu.

View attachment 3220390
Huyu anasema wakazi wa Goma wanawashangalia M23 wakiingia mjini. Anadhani wananchi wao ni wajinga wakae kimya katika hali hiyo ya Vita, wanyamaze wasimpokee mtawala mpya? Kwani hawajipendi? Hata leo ikatokea jeshi la Congo likaurejesha mji bado wananchi haohao watashangilia
 
hawaelewi.Hapo hiyo ngoma itapiganwa mpaka mshindi apatikane hiyo ndo suluhu tu KWENYE MALI HUWA KIFO NDO KINACHOAMUA AMANI
Tukienda hivi mbona mshindi anajulikana, tatizo M23 akishinda kutakuwa na amani ya kudumu kama kuna jamii zingine zinawaona "walowezi". Hapa issue ni referendum tu wananchi waulizwe kama wanaenda Rwanda au wabaki Drc, vijiji vitakavyosema Yes vienne Rwanda na vinavyosema No vibaki DRC. Ni muhimu kuwa inclusive kwa jamii zote na ikishindaja seccession is vital.
 
Iko vile !
Nayachukia macongo yaliyomkamata na kumuua Lumumba !
Laana ile itawaandama vizazi na vizazi !
 
Hoja yangu ni kwamba, tusilaumu wazungu kwa vita za DRC maana kufadhili vikundi ili upate dhahabu HAINA FAIDA kama kupora dhahabu kupitia mikataba mibovu maana hautoingia gharama ya kununua silaha we kazi yako ni kutoa rushwa kwa watu wachache kuliko kufadhili VITA!! kwahiyo hakuna mwekezaji atapenda vita kuliko amani, so sio kweli kuhusu hili.

Hoja yako ni nini? Kwamba kuwaunganisha watusi walioko Congo ndio suluhu? Ok. Mauaji ya kimbari ya Rwanda yalikuwa Watuso na wahutu ndani ya nchi moja kwa hoja yako hiyo walitakiwa kila kabila kiqe nchi yake?
Huko Ituri, Kivu nord na sud, hao wanyamulenge wanaonekana ni "wakuja" au "wavamizi" kwahiyo hata iweje itakua ngumu kuwa incorporated. Ila wakijiunga na "ndugu" zao wa Rwanda na Burundi itapunguza tension maana hata assimilation itakua rahisi.

Nimeshauri referendum, iwe level hata ya kijiji wataoafiki kipande cha ardhi kimegwe kiwe assimilated na Rwanda. Patengenezwe buffer state ili kupunguza vita ukanda huo otherwise itakua mauaji tu maana ukabila umewameza.

Kwa baadae hata Burundi na Rwanda ziungane tu maana assimilation yao ni rahisi pia. Tupunguze tensions kwa simple solutions sio kulazimisha mambo yaliyofeli.
 
Ni kweli huwezu kufukuza Wajaluo wa Mara ukasema ni Wakenya. Au Kenya ikafukuza Wamasai eti ni Watanzania.
 
Pumbaf kabisa
 
Shida ya Madini iliyoko Congo iko afrika nzima, tofauti ni M23 wamejaribu kukataa kuibiwa Mchana Kweupe ndio maana hayo yanatokea
 
DRC ni mali ya wakongoman, waachwe wakongo na kongo yao.
Rwanda anafuata nini Kongo?:
Bahati mbaya siasa kati ya nchi huwa haziendi hivyo kwa kuachwa tu. Watu wanapigana karibu na mpaka wako utasema unawaacha tu? Unafikiri kwa nini Kenya iliingia Somalia Au Misri inakuwa na kelele sana kuhusu matumizi ya maji ziwa Victoria??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…