Video: Treni ya SGR yadaiwa kusimama baada ya kupata hitilafu eneo la Gongo la Mboto

Video: Treni ya SGR yadaiwa kusimama baada ya kupata hitilafu eneo la Gongo la Mboto

Status
Not open for further replies.
Kodi za Watanzania zinateseka sana.

Siku si nyingi watajitokeza wasiokuwa nachakupoteza halafu tutaanza kulaumiana.

Kuna haja yakuanza kuwashitaki viongozi wa Tanzania mahakama za kimataifa kwa kufuja Kodi za wananchi na kuliingiza Taifa kwenye madeni kila kona, tukiomba dunia izuie account za nje za viongozi wa Tanzania, kuwazuia kusafiri nje ya mipaka ya Tanzania na hata kuzuia member waa familia zao kuishi, kusoma au hata kutibiwa Ulaya.
 
Subirieni kifo cha kitaifa kama ile iliyokuwa inaenda kigoma miaka wakati wa serikali ya mkapa
 
Swala sio project yenyewe, Project tunaipenda na tunaiunga mkono, ila utekelezaji ndiyo unasikitisha. Kaangalie Sgr za umeme za China alafu linganisha na huo mkweche tulioletewa. Unajiuliza nani aliyepitisha na kukubali hayo matreni mabovu yanunuliwe?
Ten percent
Kulamba asali unajifanya hujui

We hupendi kulamba asali

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
TUSIWE NEGATIVE SANA kama imepata changamoto itatatuliwa hakuna shida hapo. Changamoto kitu cha kawaida, na mwanzo ni mgumu karibu kwa kila kitu. Baadhi yenu mlisema Bwawa la Nyerere ni WHITE ELEPHANT ama mnataka kusema kitu chochote atakachoanzisha mwafrika ni White Elephant??
Tutafika tukiwa tumechoka sana au pengine hatutafika kabisa. Kwa nini kile kinachaonzishwa na kusimamiwa na sisi wenyewe hapa nchini haraka sana kinadorora katika hatua za mwanzo tuu, halafu wanakuja watu e.g. ww na wanatoa maelezo ya utetezi na blaa blaa nyingi.? Mbona huko kwingine miradi inawekewa time frame na viashiria wakati wa majaribio ili baadaye Mradi utakapoanza full scale yasijitokeze madhila kama hayo? Sasa waliokwama hapo wanarudi Dar (kwa usafiri upi na gharama za nani)au wanasubiri yafanyike matengenezo? (Wataishije hapo porini).
 
Ila wabongo haki mmechoka aisee. Kila anaye comment ni povu tu la negative. Dah! Serekali angalieni hili swala. Wananchi wanachuki sana na serekali ni vile tu hamtaki kufungua masikio msikie.

Kwani hizi mambo zilishaanza safari commercial? Inawezekana zipo kwenye majaribio jamani. Panapo majaribio treni inaweza kusimama popote jamani. Kwann mnawaza limebuma?

Lakini pia Inawezekana kuna changamoto na ndio maana ya majaribio ili kabla ya kuanza safari officially hizi changamoto zote ziwe zimetatuliwa

Pamoja na yote, serekali kaeni kwa kutulia sana, wananchi wana sumu nyingi sana mioyoni mwao juu yenu
Huyo sirikal unamjua?
Ulishawahi muona?

Hata wewe ni sirikal kama hujui

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sgr siyo treni ya umeme Wala yenye umbo la risasi,sgr ni gauge ya relief,china Ina hela,nchi yako fukara,Kodi unakwepa,tozo unapinga,hela za kununua bullet train zitatoka wapi?
Zinatoka kwenye bandar,mbuga za wanyama,misitu,maziwa,migod,gas,madini,mifugo,watalii,
Kilimo,

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Tutafika tukiwa tumechoka sana au pengine hatutafika kabisa. Kwa nini kile kinachaonzishwa na kusimamiwa na sisi wenyewe hapa nchini haraka sana kinadorora katika hatua za mwanzo tuu, halafu wanakuja watu e.g. ww na wanatoa maelezo ya utetezi na blaa blaa nyingi.? Mbona huko kwingine miradi inawekewa time frame na viashiria wakati wa majaribio ili baadaye Mradi utakapoanza full scale yasijitokeze madhila kama hayo? Sasa waliokwama hapo wanarudi Dar (kwa usafiri upi na gharama za nani)au wanasubiri yafanyike matengenezo? (Wataishije hapo porini).
Kwani imeishaanza kufanya kazi ama ni majaribio! Kuna vitu vingi sana vilianza hata huko kwa wazungu na vikapata changamoto za hapa na pale na bado wakafanyia marekebisho na wakatoboa. Kama una uhakika kuwa safari zimeanza tafadhali sema na tupe RATIBA.
 
Hii ni SGR ya umeme ya China, linganisha na hii takataka ya sobibo ya Tanzania

images - 2024-05-16T192716.502.jpeg
 
Kwani imeishaanza kufanya kazi ama ni majaribio! Kuna vitu vingi sana vilianza hata huko kwa wazungu na vikapata changamoto za hapa na pale na bado wakafanyia marekebisho na wakatoboa. Kama una uhakika kuwa safari zimeanza tafadhali sema na tupe RATIBA.
Aisee; Hapo ilipokwama, kwa mujibu wa video clip, ilikuwa inaenda wapi na ilibeba nini? Kama haikuwa na abiria; basi mkuu, nasitisha na naondoa karata yangu. Ngoma ichezwe.
 
Mbona treni zingine za SGR zinazotumia umeme huko kwingineko duniani zina muonekano bora na mzuri kuliko hii ya Tanzania?
Nadhani muonekano wa treni hutegemea imeundwa itembee kwa spidi gani. Mfano hapa Ujerumani kuna treni zinaitwa ICE ( Intercity Express ) ambazo zinatembea mpaka spidi 300km/h. Pia kuna Regional Trains ( RE , RB, S-Bahn ) ambazo hutembea kati ya spidi 80km/hr - 150km/hr.
ice.jpeg

Intercity Express (ICE)

RB.jpeg

Regional Train ( RB)

Japokuwa haipendezi kweli kuona treni zetu zimeanza kusumbua mapema hivi.
 
Ukweli unajulikana. Waswahili wanafanya hujuma ili mabasi ya Sh
Mradi huu lazima uangaliwe kwa umakini mkubwa sana,ili kuleta faida kwa umma.
Ukweli unajulikana. Waswahili wanafanya hujuma ili mabasi ya viongozi yasikose soko. Esther Bus (Mwigulu - Waziri), Shabiby Bus (Shabibu - Mbunge), Abood Bus (Abood - Mbunge), Musukuma Bus (Musukuma - Mb) n.k.

Viongozi wakubwa pia wana hisa kwenye kampuni hizo zenye zaidi ya mabasi 600 kwa ujumla wake. Wenye akili tunajua ni hujuma.

R.I.P JPM
 
Huwa kuna tatizo la kawaida kipande flani cha reli kukosa umeme na treni ya umeme kusimama, hiyo ni hali ya kawaida sana kule developed countries. Japo kwa wenzetu mainjinia wao hutatua haraka.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom