The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Hii ni kutoka katika maktaba ya mjadala na michango ya wajumbe mbalimbali wa bunge la kupata katiba mpya mwaka 2012/2013 huko Dodoma. Bahati mbaya CCM walivuruga mchakato huo na hivyo kukwama na taifa kupata hasara mabilioni ya fedha zilizopotea bure bila kuleta matokeo...
Katika bunge hilo la mchakato wa kupata katiba mpya, wajumbe wengi walitoa michango iliyotia fora sana na kuwa kumbukumbu nzuri...
Ila baadhi wachache walikuwa na michango na mawazo bora zaidi ya wengine..
Mmoja wa mchango wa kukumbukwa sana ulikuwa wa ndugu Tundu Lissu mbunge wa bunge la katiba (CHADEMA) na mbunge wa bunge la JMT kutoka Jimbo la Singida Mashariki wakati huo....
Mnakumbuka, kabla ya hii, ilitanguliwa na hotuba yake kali sana ya kuukosoa muungano wenyewe na kumkosoa vikali pioneer wa muungano huo na mwasisi wa taifa hili Mzee Julius K. Nyerere...
Baadhi ya wana CCM walikwazika sana kiasi cha kumjengea hoja kuwa "kamtukana" baba wa taifa lao yaani Mwl. Julius K. Nyerere. Wakamshambulia sana ndani na nje ya bunge hilo...
Siku chache baada ya negative reaction ya hotuba yake hiyo toka kwa baadhi ya wana CCM, sasa kwa dakika kama 10 hivi, mtazame na sikiliza akijibu viroja vya wana CCM hao ktk video hiyo hapo juu...
NB:
Samahanini sana kwa ubora duni wa picha wa video hiyo. Hata hivyo, sauti ndiyo muhimu zaidi na inasikika kwa uzuri sana...
Pia background, unaweza kuisikia sauti ya Mama Samia Suluhu Hassan [Sasa ni Rais wa JMT] lakini wakati huo akiwa mmoja wa wenyeviti wa bunge hilo la katiba ya wananchi..