Video: Ubishani ni Zanzibar ni nchi au siyo? Wenzenu upande wa Zanzibar ni Wazanzibari au Watanzania? Wasira, Rais Samia vs Tundu Lissu: Nani mkweli?

Video: Ubishani ni Zanzibar ni nchi au siyo? Wenzenu upande wa Zanzibar ni Wazanzibari au Watanzania? Wasira, Rais Samia vs Tundu Lissu: Nani mkweli?

Mkuu serikali iliyopo ni ya Tanganyika ila ililzimisha kibabe iwe serikali ya Tanzania.

Maana hakuna utaratibu uliofanyika wa kuunda muungano isipokuwa Nyerere (Tanganyika) alitamka asubuhi na decree ya kubinafsisha Tanganyika kuwa Tanzania!

Hatujawahi kuwa na serikali ya Muungano!

Mkuu are sure huu mfano uliotumia unaakisi the reality uliyo taka kupresent au unakimbia hoja kwa mfano mwepesi???
TANZANIA sio Tanganyika
 
Dawa ni kuwepo Serikali ya Tanganyika! Kila serikali ijiamlie mambo yake kasoro Ulinzi,Uhamiaji,mambo ya nje na ndani yawe ya Muungano kama ilivyo sasa!
Tanganyika na Zanzibar zisiwe nchi bali mataifa mawili ndani ya nchi moja ya Tanzania.
Mkuu serikali iliyopo ni ya Tanganyika ila ililazimisha kibabe iwe serikali ya Tanzania.

Maana hakuna utaratibu uliofanyika wa kuunda muungano isipokuwa Nyerere (Tanganyika) aliamka asubuhi na decree ya kubinafsisha Tanganyika kuwa Tanzania!

Hatujawahi kuwa na serikali ya Muungano!
Hata ukiwa na kila kitu, bila sovereignty, wewe sio nchi!. Zanzibar haina dola, haina sovereignty hivyo sio nchi!.
P
Mkuu, kimsingi unakubali kuwa Tanganyika tunatumia mabavu kuikalia Zanzibar! Kwa sababu tunajua kuwa Tanganyika ndio Tanzania!
 
TANZANIA sio Tanganyika
Tanzania mpaka mwaka 1965 haikuwa kuwepo ila ilikuja mwaka 1965 ila Nchi ilikuwa ikiitwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar..

Na hata Katiba ya Muungano ya mwaka 1964 iliitwa katiba ya Muungano wa Tanganyika Na zanzibar..

Ila baada ya 3 decrees za Mwalimu nyerere..
Akabadilisha Serikali ya Tanganyika na Kuwa Serikali ya Muungano na Viongozi na mali zote zikawaa chini ya Muingano na Tanzania huku Zanzibar Haikugushwa na Decree hizo..

Ndo maana Mara nyingi watu wakigusa hizo decree huonekana Wabaguzi lakini hapo ndiyo shida ilipoanza..
Maana hizo decrees zio Makubaliano ya Muungano...
 
Mkuu mdukuzi , hilo haliwezekani aslaan!. Unakijua kilichomkuta Abdul Jumbe?. Nani atathubutu kufanya ujinga huo?. Tanzania ni nchi moja ya JMT, kitendo cha kujitoa muungano ni sawa na uhaini kwa JMT!, no one can dare do that!. Mwisho wa uwezo wao ni kwa vitimbakwiri kupiga tuu kelele!, there's nothing they can do!. Huu
Muungano wetu adimu na adhimu tutaulinda kwa gharama yoyote!.
P
Mkuu nyakati hubadilika, himaya za uajemi, ugiriki, rumi, uingereza na usovieti zilisambaratika, siku watanganyika wakigutuka hutaamini, ni suala la muda tu!
 
Tanzania mpaka mwaka 1965 haikuwa kuwepo ila ilikuja mwaka 1965 ila Nchi ilikuwa ikiitwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar..

Na hata Katiba ya Muungano ya mwaka 1964 iliitwa katiba ya Muungano wa Tanganyika Na zanzibar..

Ila baada ya 3 decrees za Mwalimu nyerere..
Akabadilisha Serikali ya Tanganyika na Kuwa Serikali ya Muungano na Viongozi na mali zote zikawaa chini ya Muingano na Tanzania huku Zanzibar Haikugushwa na Decree hizo..

Ndo maana Mara nyingi watu wakigusa hizo decree huonekana Wabaguzi lakini hapo ndiyo shida ilipoanza..
Maana hizo decrees zio Makubaliano ya Muungano...
✍️📝👍👌👏🤝🙏🛡️
 
Mimi nimezaliwa Tanzania, na wengi wetu tumezaliwa Tanzania, waliozaliwa Tanganyika wote by now ni wastaafu, wako over 60 years, na walipopata akili, walikuwa tayari Tanzania, ni Watanganyika gani hao wa kuililia Tanganyika na kujivunia Tanganyika?.

Muungano ni kama ndoa, Zanzibar ni kama mwenza, sasa wewe kama mwenza wako anajipodoa, na wewe utataka kujipodoa ili mlingane?. Hebu acheni hizi kitu!.
P
Wanachofany Wenzetu sio kujipodoa bali kujipofua Ili wasione uhimu wa ndoa yetu ... Hili linatikisa Misingi ya ndoa yenyewe!
 
View attachment 2991056
Ndugu wana JF - Jukwaa la Siasa;

Mjadala wa muungano tata wa Tanganyika na Zanzibar (1964) unaendelea tena leo....

Na kwa kweli mjadala huu haupaswi kuishia njiani isipokuwa tu wote tumeelewana na kukubali kuwa lipo tatizo ktk muungano huu linalostahili kutatuliwa sasa na sio kesho kama tunataka kuendelea nao...

Leo katika video hiyo☝🏻☝🏻 ni makala ya uchambuzi toka kwa mchambuzi nguli wa maswala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ndugu Ansbert Ngurumo kupitia YouTube channel yake [SK Media Online TV] anayeishi uhamishoni Uingereza

Katika uchambuzi huu, Ansbert Ngurumo anazimulika kauli za watu watatu juu muungano wa Tanganyika na Zanzibar (1964) ambao ni;

1. Mzee Steven Wassira a.k.a Tyson (CCM)
2. Rais Samia Suluhu Hassan (CCM)

3. Tundu Antipasy Lissu (CHADEMA)

Hawa wote wanajibu maswali mawili muhimu yafuatayo ambayo ndiyo msingi mkuu wa ubishani unaoendelea sasa ktk muungano huu;

1. KWAMBA, Zanzibar ni nchi au sio nchi?

2. KWAMBA, Watu au wananchi wa nchi ya Zanzibar ni Watanzania au Wazanzibari?

Nani mkweli kati ya hawa watu watatu kuhusu muungano wetu? Nini maoni yako? Tatizo liko wapi? Ni kitu gani kinafichwa kupitia muungano huu?

Tazama na sikiliza video hiyo ya dakika 14 tu hadi mwisho kisha tumia akili yako kupima mwenyewe halafu sema kitu.

Na bila shaka kasi ya internet imeboreka kiasi chake na hivyo kila mtu ataifungua video hii bila kuhangaika sana..
==========================================
Huyo ndio Ansbert Ngurumo !
Maswali magumu. !!
Hoja hujibiwa kwa hoja sio kwa kutumia Nguvu za aina yeyote ile. !🙏
Au nasema uongo nduguzanguni ??!! 🙏🙏😇😳🙄
 
Dawa ni kuwepo Serikali ya Tanganyika! Kila serikali ijiamlie mambo yake kasoro Ulinzi,Uhamiaji,mambo ya nje na ndani yawe ya Muungano kama ilivyo sasa!
Tanganyika na Zanzibar zisiwe nchi bali mataifa mawili ndani ya nchi moja ya Tanzania.
United States of Tanzania !!??
 
Huu ndio ukweli wa mambo, tena sio wanahisi tumewaoa, bali huyo mwanamke ndie alijitongozesha, akajibebisha, Mzee Tanganyika akachukua ngoma, akaoa, akatia ndani, analisha, anatunza, anagharimia kila kitu, mke kazi kupendeza tuu, kila kitu bure!.

Niliwahi kuuliza humu Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe?

Tanzania itakuwa na wanaume wa ajabu wanao ona wivu na wake zao kwa kutamani wawe sawa kwa sawa!.
Mwacheni mkeo apendeze. Mpe kila anachokitaka!.

P

Pascal, mambo siyo rahisi kiasi hicho.

Kama Zanzibar ni mke basi ni mke aliyekengeuka na kuota mapembe. Mke gani anakuwa na mamlaka mpaka ya kumpora mali ( bandari, mbuga za wanyama na hifadhi za misitu) mumewe, tena ulizochuma kabla hamjaoana; halafu anaenda kuwagawia wanaume wengine wa asili yake (waarabu), na wewe bado utajiita ni wanaume? Hapo si unakuwa mume bwege?
 
1. Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye uraia mmoja tuu wa JMT. Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT.
2. Wananchi wa Zanzibar ni Watanzania ila pia ni wakaazi wa Zanzibar. Ukaazi sio uraia.
P

Hiyo ya Wananchi wa Zanzibar imekaaje .....!!?

Hivi kusema Wananchi wa Mwanza, Wananchi wa Mbeya au Wananchi wa Moshi ni sawa pia....!!?
 
Zanzibar ni nchi , mbaya zaidi zile tamaduni za Tanganyika na zenji licha kuungana kwa miaka mingi ila bado haziendani ...Kuna baadhi ya mikasa nilikutana nayo chuo ndio nikajua kwamba kuna bifu kubwa .

Kipind nasoma chuo watu walishapigana kabisa tena mtanganyika msukuma ndio alianzisha ugomvi , baadae alitoa shutuma nzito mbaya kwa wazenji nao wazenji wakasema tabia zote za ovyo zililetwa baada ya muungano. Ukifika zenji wanadai huku ndio wameleta tabia za ovyo.

Kiufupi mila haziendani ndio sababu kubwa ,Nyerere alitaka kupeleka mila za huku kwend zenji akafeli akabaki kupiga kelele tu.
 
Mimi nimezaliwa Tanzania, na wengi wetu tumezaliwa Tanzania, waliozaliwa Tanganyika wote by now ni wastaafu, wako over 60 years, na walipopata akili, walikuwa tayari Tanzania, ni Watanganyika gani hao wa kuililia Tanganyika na kujivunia Tanganyika?.

Muungano ni kama ndoa, Zanzibar ni kama mwenza, sasa wewe kama mwenza wako anajipodoa, na wewe utataka kujipodoa ili mlingane?. Hebu acheni hizi kitu!.
P
Kwakweli hizi arguments unazotoa hapa zinanishangaza sana na kunisikitisha pia.
 
Ninefuatilia hii mijadala ya mambo ya muungano sehemu mbalimbali ila kote huko naona kama kuna kitu hakipo sawa.

Nadhani ni busara sana Serikali ikafanya maamuzi sasa na kutengeneza aina ya muungano ambao hauna maswali kama huu wa sasa.
 
Back
Top Bottom