Video: Ubishani ni Zanzibar ni nchi au siyo? Wenzenu upande wa Zanzibar ni Wazanzibari au Watanzania? Wasira, Rais Samia vs Tundu Lissu: Nani mkweli?

TANZANIA sio Tanganyika
 
Dawa ni kuwepo Serikali ya Tanganyika! Kila serikali ijiamlie mambo yake kasoro Ulinzi,Uhamiaji,mambo ya nje na ndani yawe ya Muungano kama ilivyo sasa!
Tanganyika na Zanzibar zisiwe nchi bali mataifa mawili ndani ya nchi moja ya Tanzania.
Mkuu serikali iliyopo ni ya Tanganyika ila ililazimisha kibabe iwe serikali ya Tanzania.

Maana hakuna utaratibu uliofanyika wa kuunda muungano isipokuwa Nyerere (Tanganyika) aliamka asubuhi na decree ya kubinafsisha Tanganyika kuwa Tanzania!

Hatujawahi kuwa na serikali ya Muungano!
Hata ukiwa na kila kitu, bila sovereignty, wewe sio nchi!. Zanzibar haina dola, haina sovereignty hivyo sio nchi!.
P
Mkuu, kimsingi unakubali kuwa Tanganyika tunatumia mabavu kuikalia Zanzibar! Kwa sababu tunajua kuwa Tanganyika ndio Tanzania!
 
TANZANIA sio Tanganyika
Tanzania mpaka mwaka 1965 haikuwa kuwepo ila ilikuja mwaka 1965 ila Nchi ilikuwa ikiitwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar..

Na hata Katiba ya Muungano ya mwaka 1964 iliitwa katiba ya Muungano wa Tanganyika Na zanzibar..

Ila baada ya 3 decrees za Mwalimu nyerere..
Akabadilisha Serikali ya Tanganyika na Kuwa Serikali ya Muungano na Viongozi na mali zote zikawaa chini ya Muingano na Tanzania huku Zanzibar Haikugushwa na Decree hizo..

Ndo maana Mara nyingi watu wakigusa hizo decree huonekana Wabaguzi lakini hapo ndiyo shida ilipoanza..
Maana hizo decrees zio Makubaliano ya Muungano...
 
Mkuu nyakati hubadilika, himaya za uajemi, ugiriki, rumi, uingereza na usovieti zilisambaratika, siku watanganyika wakigutuka hutaamini, ni suala la muda tu!
 
✍️📝👍👌👏🤝🙏🛡️
 
Wanachofany Wenzetu sio kujipodoa bali kujipofua Ili wasione uhimu wa ndoa yetu ... Hili linatikisa Misingi ya ndoa yenyewe!
 
Huyo ndio Ansbert Ngurumo !
Maswali magumu. !!
Hoja hujibiwa kwa hoja sio kwa kutumia Nguvu za aina yeyote ile. !🙏
Au nasema uongo nduguzanguni ??!! 🙏🙏😇😳🙄
 
Kuna hoja zingine ni kama funika kombe mwanaharamu apite
 
Dawa ni kuwepo Serikali ya Tanganyika! Kila serikali ijiamlie mambo yake kasoro Ulinzi,Uhamiaji,mambo ya nje na ndani yawe ya Muungano kama ilivyo sasa!
Tanganyika na Zanzibar zisiwe nchi bali mataifa mawili ndani ya nchi moja ya Tanzania.
United States of Tanzania !!??
 

Pascal, mambo siyo rahisi kiasi hicho.

Kama Zanzibar ni mke basi ni mke aliyekengeuka na kuota mapembe. Mke gani anakuwa na mamlaka mpaka ya kumpora mali ( bandari, mbuga za wanyama na hifadhi za misitu) mumewe, tena ulizochuma kabla hamjaoana; halafu anaenda kuwagawia wanaume wengine wa asili yake (waarabu), na wewe bado utajiita ni wanaume? Hapo si unakuwa mume bwege?
 
1. Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye uraia mmoja tuu wa JMT. Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT.
2. Wananchi wa Zanzibar ni Watanzania ila pia ni wakaazi wa Zanzibar. Ukaazi sio uraia.
P

Hiyo ya Wananchi wa Zanzibar imekaaje .....!!?

Hivi kusema Wananchi wa Mwanza, Wananchi wa Mbeya au Wananchi wa Moshi ni sawa pia....!!?
 
Zanzibar ni nchi , mbaya zaidi zile tamaduni za Tanganyika na zenji licha kuungana kwa miaka mingi ila bado haziendani ...Kuna baadhi ya mikasa nilikutana nayo chuo ndio nikajua kwamba kuna bifu kubwa .

Kipind nasoma chuo watu walishapigana kabisa tena mtanganyika msukuma ndio alianzisha ugomvi , baadae alitoa shutuma nzito mbaya kwa wazenji nao wazenji wakasema tabia zote za ovyo zililetwa baada ya muungano. Ukifika zenji wanadai huku ndio wameleta tabia za ovyo.

Kiufupi mila haziendani ndio sababu kubwa ,Nyerere alitaka kupeleka mila za huku kwend zenji akafeli akabaki kupiga kelele tu.
 
Kwakweli hizi arguments unazotoa hapa zinanishangaza sana na kunisikitisha pia.
 
Ninefuatilia hii mijadala ya mambo ya muungano sehemu mbalimbali ila kote huko naona kama kuna kitu hakipo sawa.

Nadhani ni busara sana Serikali ikafanya maamuzi sasa na kutengeneza aina ya muungano ambao hauna maswali kama huu wa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…