Video: Ubishani ni Zanzibar ni nchi au siyo? Wenzenu upande wa Zanzibar ni Wazanzibari au Watanzania? Wasira, Rais Samia vs Tundu Lissu: Nani mkweli?

Kwani Waarabu wa Dubai hawana Undugu na Samia?
Pili Umesahau kila uongozi nahisi Hili swala La muungano Huwa linaibuka Hata kwa Magufuli liliibuka Ila Magufuli alishughulika nalo..
Kwa kikwete hivyo Hivyo na hata kwa Mkapa kama una kumbukumbu..

Limekuwa likiibuka sana..
Japo muda mwingi lilikuwa Likiibuka Zanzibar kwa kasi sana ils safari hii Limeibuka Bara kwa Kazi kuliko zanzibar..

Ila kila Utawala lilikuwepo ndo maana nimekuuliza Kuhusu mtikila kama Unafahamu..?

Mtikila kipindi cha Mkapa na Kikwete
Kipindi cha Tume ya Waryoba na Bunge la Bajeti Pia Ikaendelea Mpaka kwa Magufuli na sasa Imeibuka tena kwa Samia..

Nadhani Hili swala Linaibuka kutokna na Changamoto za Muungano zinavyozidi Kukua
 
Ndio ujitolea mkuu uwaelimishe ndugu zako, wao wanaona kuvaa makoti na mabuti ya jeje ndio usomi smh! vitu vidogo wanashindwa kupambanua useless empty brain.
 
Unamuamini Ponda badala ya historia iliyoandikwa? Huyu Ponda Mrundi anayejifanya mtu wa Kigoma? Na umri wake je ana miaka mingapi?
 
Siyo kweli. Umesoma vibaya alipoandika Samuel Sitta au Sitta alijielekeza vibaya. Jina Tanzania lilianza kutumika Novemba 1, 1964.

View attachment 2991615
Mkuu nauelewa upande Wako unaosema na mimi nipo upande huo huo..
Ila kuna muda Huwa sifumbi macho kuona facts zilizopo kwa upande wa Pili...

Nakushauri Tafuta kitabu cha Pius Msekwa kinaelezea Vizuri sana niliyokuwa nayaelezea

Pia tafuta
-Amri ya masharti ya Mpito ya Muungano ya mwaka 1964..

-Amri ya katiba ya Muda ("Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na zanzibar ya mwaka 1964")

-Amri ya masharti ya Mpito namba 2 ya mwaka 1964

Utaelewa kwanini watu wanalalamika kuhusu Muungano
 
Wakina Mtikila, Njelu Kasaka, Aboud Jumbe, Faki, Seif Sharif Hamad walilibua na kutumia lugha yenye ukakasi kuliko hii na wamekufa Muungano umebaki.

Na sisi tutakufa na akina Tundu Lissu na Jussa ila Muungano utabaki.

Muungano huu ungekuwa siyo mzuri na hautatui kero basi ungeshavunjika kama Mungano wa USSR au Yugoslavia, au United Arab Republic (Egypt & Syria) au Senegambia.

Ziko nchi zina kabila moja, dini moja kama Somalia au Sudan, katika miaka 60 ya Muungano wa Tanzania zimepigana, watu wameuana na miungano yao imesambaratika. Muungano wa Tanzania bado uko solid.

Mtu asikudanganye kwamba Zanzibar nje ya Muungano itapiga maendeleo. Zanzibar ni maskini sana na haina raslimali zozote za maana. Mdiyo maana hata viwango vya kodi inayotozwa ni ndogo kwa vile watu wa kule ni maskini sana. Angalia hata umeme hawawezi kulipa kama huku bara, lazima tuwawekee ruzuku.

Mategemeo yao ni kujisalimisha kwa masultani wao wa zamani tu (Oman) na wao kubakia vijakazi
 
Wazenji wengi wana undugu na waarabu japo mara nyingi ni kizazi kimoja au viwili nyuma, isiwe nongwa kwa Samia kuwa na udugu na waarabu. Mtikila namkumbuka na ile hotuba yake ya 'magabacholi'.
 
Mkuu Mimi simo maana Wakikusikia Ndugu zangu (Wazanzibar) nawajua Vizuri wao Matusi Huwa yapo karibu na watasema Unaleta Lugha za kuwabagua
 

Wewe jamaa ni kilaza sana .
Hapo nilipo bold umedanganya .
Huu Muungano unayo mambo mahususi ya muungano.
Huwezi kusema mambo ya Tanzania ni ya wote acha kupotosha sio kweli
 
Wewe jamaa ni kilaza sana .
Hapo nilipo bold umedanganya .
Huu Muungano unayo mambo mahususi ya muungano.
Huwezi kusema mambo ya Tanzania ni ya wote acha kupotosha sio kweli
Ukiwa hujui na unajua kuwa hujui, wewe ni mjinga, ukielimishwa utaerevuka, ujinga utakutoka, utakuwa mwerevu.

Ukiwa hujui, na hujui kuwa hujui, bali unajidhania unajua, wewe ni... (naomba nisimalizie kwa kukuheshimu).

Ndio maana nimesisitiza elimu kuhusu huu muungano wetu adhimu inahitajika sana.
Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye uraia mmoja tuu wa JMT. Kila Mtanzania bila kujali anatoka wapi, ana haki sawa kabisa. Ila Watanzania wenye ukaazi wa Zanzibar, wana haki za ziada za Uzanzibari.

P
 
Performance ya muungano ndio hii , Pascal labda wewe unaona sawa na nzuri kwa sababu wanaoumia si watu wako
Elimu ya uraia inahitajika sana!. Uhalali wa ndoa sio shahada ya ndoa, ni performance ya ndoa, consummation. Hivyo hata mkichukuana tuu bila kufunga ndoa, mkafanya performance ya ndoa, mnakuwa mna ndoa halali baada ya kuishi kinyumba for sometime.

Vivyo hivyo kwa muungano, hata kama mmoja hakuridhia lakini anatimiza majukumu ya muungano, ni kuuhalalisha!. Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?
P
 
1. Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye uraia mmoja tuu wa JMT. Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT.
2. Wananchi wa Zanzibar ni Watanzania ila pia ni wakaazi wa Zanzibar. Ukaazi sio uraia.
P
Mkuu P

Tatizo liko hapa na hizi siasa zilizopo kuna muda zitafikia pabaya bila nchi zote za mwanzo kuyapoteza majina yao ya asili
1. Katiba ya Zanzibar 1984


2. Katiba ya Zanzibar 1985

3. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

4. Wanasheria wakuu wa serikali ya JMT na SMZ ambao ni Andrew Chenge na Idd Pandu wanajibika katika mtanziko wa katiba hii inayopingana yenyewe wazi wazi bila aibu. Yaani mtoto anadai 'wewe kaka hukunizaa, nilijizaa mwenyewe hivyo niachie mambo yangu ila ya kwako unijumushe'!!!
Uzanzibari ni sawa na watu wanaojiita wa Kasikazini, Pwani, Kanda ya Ziwa, Nyanda za Juu Kusini nk.

Huu ni ubaguzi utakiwa ukomeshwe na katiba ambayo inaweza kusimamiwa kwa dhati bila kuingiza siasa za kuleana. Mzanzibari ana fursa Tanganyika (Tanzania bara) lakini Mtanganyika (Mtanzania bara) hana fursa zozote za umiliki wa kudumu mali Zanzibar hii sio haki.

Mzanzibari anaweza kugombea au kuteuliwa uongozi Tanganyika (Tanzania bara) lakini Mtanganyika (Mtanzania bara) ni mwiko kugombea au kuteuliwa kuongoza hata idara huko Zanzibar-ni ubaguzi

Angalizo: Hakuna Mzanzibari wa asili huko Zenj kuna uzao uliotoholewa kwa mchanganyiko wa jamii tofauti na nyingi zimetokea bara hasa Mtwara, Lindi, Tanga, Kigoma, Shinyanga, Tabora, Comoro, Malawi (Wanyasa), Kongo (Manyema na Wabembe) na Lamu.

Kudai kwamba hawataki kuchanganywa na Wabara kwamba wanalinda utamaduni wa KiZanzibari hii sio haki wakati wenyewe wanashiriki kwa kasi kuua utamaduni wa Watanganyika haiwezekani..

This must come to an end to maintain respect to each other.
 
Hata kama wazanzibari hawaukubali ?? Performance ipi ya kuwauwa wazanzibari kila uchaguzi ili kuweka vibaraka vya Tanganyika ??
Ziko ndoa nyingi tuu, wanandoa wanasigana, lakini performance inaendelea na ndoa inaendelea. Usisikilize kelele za vitimbakwiri vya wapinga muungano, muungano wetu ni imara, na tutaulinda kwa gharama yoyote, hata kama baadhi ya gharama hizo ni machozi, jasho na damu!.
P
 

1. Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye uraia mmoja tuu wa JMT. Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT.
2. Wananchi wa Zanzibar ni Watanzania ila pia ni wakaazi wa Zanzibar. Ukaazi sio uraia.
P
Katiba ya Zanzibar inasema zanzibar ni nchi au sio nchi?.
 
Katiba ya Zanzibar inasema zanzibar ni nchi au sio nchi?.
Katiba ya Zanzibar ni kwa ajili ya mambo ya ndani ya Zanzibar, Katiba ya JMT haitambui katiba ya Zanzibar. Tanzania ni nchi moja ya JMT, Zanzibar sio nchi ni sehemu ya JMT. Hivyo haijalishi katiba ya Zanzibar inasema nini kuhusu Zanzibar, hayo ni mambo yao, hayatuhusu!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…