Video: Vijana kuweni serious. Kuna huyu Thobias Kahimba alianza kwa kuchoma CD kwa Tsh 100 hadi amekuwa Bilionea. Mnakwama wapi?

Sasa kama kuna shughuli nyingine iliyompa mafanikio kwa nini story inakuwa kuchoma CD!

Wewe hujaangalia video.

Amesema hapo kuwa ana kampuni ya usafirishaji na ana kampuni ya hardware.

Ulitaka ataje nini ndo uridhike? Ngada?
 
Siri ya utajiri wa mtu haijawahi kuwa wazi. Acheni mbwembwe.
 
Sio rahisi hivyo,Kuna mengi nyuma ya pazia hajayasema
Ni sahihi, ukiona mtu anasema hivi au vile kuhusu mafanikio yake ujue kuna kitu anataka kukificha na pia anataka kujenga imani kwa jamii ili waamini kuhusu hilo jambo
 
Katika maisha yangu hadi nilipofikia kiumri, nimejifunza kuwa:

Hakuna tajiri yeyote atakayekuambia siri ya mafanikio yake.

Yeye hajataja siri yoyote. Video umeiangalia?

Amesema alianza kuchoma CD akapata hela akaenda kuanzisha biashara nyingine.

Wewe ndo unataka mambo ya siri.

Mwenzio ameongelea alipoanzia.

Fanya kazi acha kujifariji mambo ya ajabu
 
Kama hio kazi inawafanya watu mabilionea mbona mimi sikuwahi kuwa billionea.

Niliifanya hio mishe 2009-2010 ila zaidi ya kupata mademu hamna nilichofaidika nacho. Hela ya kula tu.
Uzi huu umezidi kunionesha kuwa Watanzania wengi ni wajinga sana tu bado.

Yani hoja rahisi na ya msingi kama vile habari kutakiwa kuwa na vyanzo tofauti ili kuweza kuwa na credibility ya juu bado inawapiga chenga Watanzania wengi.

Hawajui au hawajali kwamba wafanyabiashara wengi hawako wazi kuhusu vyanzo vya mafanikio yao, na jambo hilo linahitaji uhakiki wa kina, na mtu kuwa chanzo cha habari ya kuhusu chanzo cha mafanikio yake, bila ya habari hiyo kuwa na chanzo tofauti, ni tatizo, habari hiyo inakuwa na low credibility.

Wabongo wengi ukiwaambia hii habari ina low credibility kwa sababu mtoa habari anatoa habari kujihusu yeye mwenyewe, na habari haina chanzo kingine tofauti, wanakwambia una wivu, una chuki.

Wanashindwa kuangalia hoja, wanakuja kimahaba kumtetea bilionea wao.

Wengine wanashindwa kueleea hoja ya kuhoji chanzo cha ubikionea, wanaukiza "kwa hiyo unasema jamaa si bilionea?"

Hawaelewi kuwa kwenye habari habari si mtu kuwa bilionea tu, habari ni mpaka chanzo cha ubilionea.

Hapo ndipo utajua mfumo wetu wa elimu umefeli.

1. No critical thinking.
2. No abstract thinking.
3. No logical thinking.
4. No reading comprehension.
 
Ni sahihi, ukiona mtu anasema hivi au vile kuhusu mafanikio yake ujue kuna kitu anataka kukificha na pia anataka kujenga imani kwa jamii ili waamini kuhusu hilo jambo

Ila wakina Zuckerberg na Steve Jobs hadi speeches zao mnasikiliza freshi.

Shida yenu maisha yenu yana-rotate around social media.

Mkata viuno Diamond akisema yeye ni tajiri mnakubali ila akisema mtu ambaye hujawahi kumuona hamuamini.

Hivi mnajisikia?
 
Having said all that, why don't you believe that guy can be a billionare from scratch? Maneno yako yanathibitisha inawezekana. Dogo kaanza hustle baada ya kuhitimu form 4 now he is 30, miaka mingapi hio? Si chini ya 15
 

😂😂 huyu si ni ali-ignore?
 
True wanaficha best part ya story zao ila hii inahusisha na imani tulizojijengea kiafrika na roho mbaya tulizonazo hatutaki kuona wenzetu wameendelea bali tunataka tuwashushe wawe kama sisi
 
Having said all that, why don't you believe that guy can be a billionare from scratch? Maneno yako yanathibitisha inawezekana. Dogo kaanza hustle baada ya kuhitimu form 4 now he is 30, miaka mingapi hio? Si chini ya 15
It might be true given that ali venture into other kind of businesses. Ila kusema kwamba ku burn CD ndio main source ya ubilionea hio ntaendelea kukataa.
 
It might be true given that ali venture into other kind of businesses. Ila kusema kwamba ku burn CD ndio main source ya ubilionea hio ntaendelea kukataa.
Hapana watu tu wameshikia bsngo hoo kuchoma CD. Na media zetu wanajua wakisema Kawa bilionea kwa kuchoma CD habari itakuwa hot.
 
Wewe hujaangalia video.

Amesema hapo kuwa ana kampuni ya usafirishaji na ana kampuni ya hardware.

Ulitaka ataje nini ndo uridhike? Ngada?
Mimi sina haja ya kuangalia hiyo video kwa sababu nimeona habari yote jana kupitia UTV.
Hizo gari,hardware na kuwa na akaunti iliyonona ndiyo mafanikio yenyewe,sasa ni kweli mafanikio hayo yamepatikana kwa kuchoma hizo CD au ilifikia wakati akapata channel nyingine ambayo ndiyo imemfikisha hapo alipo ambayo hakuiweka wazi kwa sababu zake binafsi?
Kwa sababu katika hali ya kawaida ni vigumu sana kupata mafanikio aliyonayo sasa kwa kuchoma CD tu.
 
Zuckerberg na hao wengine wote wanatokea upper middle class families. Hata vyuo walivyokuwa wanasomea hawaendi maskini. Hivyo kuwa mabilionea wala sio habari.

Diamond ameanza maisha na amekuwa on limelight toka anaanza hustle 2009. Strategies zake unaweza hata kuzi document kwa sababu ziko visible. Alikutana na watu wakamuamini and he did his part well. Hata ukitathmini sasa ni 15 years toka ameanza kuonekana kwa Media. Leo hii hata akasema he is worth 35 Billions in Tshs. wala sitashangaa.
 
Kwenye hio habari kwenye TV wamezungumzia kuchoma CD tu?
 
Ah wabongo utawaweza? Huyo Diamond kila siku anapigwa vita kuhusu utajiri wake. Kitu amba ho nchi mnakikubali ni shida tu. Mtu akisemwa masikini hamuwezi kuhoji kama akisema ni tajiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…