Video: Vijana kuweni serious. Kuna huyu Thobias Kahimba alianza kwa kuchoma CD kwa Tsh 100 hadi amekuwa Bilionea. Mnakwama wapi?

Vijana wako in a denial state

Kazi ipo
Vijana hawakubali kuamini kuna wanaoanza from scratch na kufanikiwa. Wanaamini kila aliefanikiwa kapitia njia za panya ambazo hasemi. Hii yote ni ku justify kuwa kufeli kwao ndio kawaida ya maisha.

Hata mimi nimechoka mbaya ila naamini wapo matajiri waliofanikiwa from scratch kwa juhudi na jasho lao sio njia za mkato. Nimefeli kwasababu kuba vitu nimekosea kwenye mapambano.
Ukikaa na waliofanikiwa utajiona ulikosea wapi. Sisi wengine hatuna muda wa kubadili ila vijana muda bado mnao badilikeni bado mna nafasi ya kutoaboa. Ila ukiamini huwezi kutoboa bila njia za mkato endelea tu tena unatakiwa utumie hizo njia ufanikiwe.
 
Unaihakiki vipi habari aliyohadithia?

Biashara zina siri nyingi, utajuaje huyu kasema kweli wapi a wapi kaficha ukweli na kupiga hadithi ya uongo?
 
Vita ikitkea hapa Tanzania sasa hivi kati ya wewe na MO Dewji nani atakuwa wa kwanza kuwa na ACESS ya kukimbia nchi?

Ndugu yako akipotea na ndugu wa Lugumi akipotea unadhani serikali itashughulika kumpata nani kwanza?
Hayo ni majanga kama majanga mengine eg. Mafuriko nk.

By the way hojayako inazungumzia afya na usalama, ambavyo nimevimention tayari.

Pia tambua kwamba kila unavyozidi kutajirika ndivyo usalama wako unakuwa hatarini.
Bila mabaunsa wa kutosha huwezi toka na ukawa na amani
 
Habari yoyote inahitaji uhakiki.
 
kapambana kwa biashara ipi?
Bilioni 4 kwa miaka 13 ina maana kaifikisha kivipi?
Ana mikopo. Kwa maelezo yake alianza kukopa 50m, mpaka sasa anakopeshwa billion. Inawezekana sema wenjine wakipata hio mikopo wananunua LC200/300 wanajenga magorofa kchenji inayobaki ndio wanaiweka kwenye biashara mwisho wa siku benki wanakuja kuchukua kila kitu.
 
Ubilionea haupatikani kiboya boya kihivyo kama vipi na wewe nenda kachome cd uwe bilionea.
Hakuna mtu atakayekwambia ukweli namna alivyopata utajiri wake.
 
Unaihakiki vipi habari aliyohadithia?

Biashara zina siri nyingi, utajuaje huyu kasema kweli wapi a wapi kaficha ukweli na kupiga hadithi ya uongo?

Yeye ameleta story ya maisha yake, unachobisha ni nini? Ulikuwa wakati anatafuta?

Au wewe ni ndugu yake?

Story za Steve Jobs, Elon Musk, Bill Gates na Mark mnaziamini ila akija Mbongo mwenzenu mnaleta ubishi.

Hebu tupe ushahidi kwamba anadanganya?
 
Habari yoyote inahitaji uhakiki.

Ndiyo maana katika uandishi wa habari kuna kanuni za kuthibitisha habari kwenye vyanzo tofauti.

Ukipuuza kanuni hii, mtu yeyote anaweza kukujaza uongo wowote, na wewe ukaukubali, kwa sababu amesema tu.
 
Ubilionea haupatikani kiboya boya kihivyo kama vipi na wewe nenda kachome cd uwe bilionea.
Hakuna mtu atakayekwambia ukweli namna alivyopata utajiri wake.

Ameleta arguments mbili.

Kwamba alianza kwa kuuza CD na sasa ana Bilioni 2 na ameajiri watu 71.

Hajasema kwenye hiyo video kwamba kuna vitu hafichi au hajafanya vitu vingine kutajrika.

Wewe unachobisha hapo ni nini? Yeye kuuza CD au kuwa Bilionea?

Ushahidi wako uko wapi?
 
Yeye ameleta story ya maisha yake, unachobisha ni nini? Ulikuwa wakati anatafuta?

Au wewe ni ndugu yake?

Story za Steve Jobs, Elon Musk, Bill Gates na Mark mnaziamini ila akija Mbongo mwenzenu mnaleta ubishi.

Hebu tupe ushahidi kwamba anadanganya?
Wewe ni kijana au mzee? Umekwama au ulikwama wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…