Video: Vijana kuweni serious. Kuna huyu Thobias Kahimba alianza kwa kuchoma CD kwa Tsh 100 hadi amekuwa Bilionea. Mnakwama wapi?

Acha mawazo potofu
Sijui kwanini watu huwa hawasemi turning point, Kuna ile point inayotrigger mafanikio yako. Hiyo ndiyo inayoleta hamasa.

Mfano wa turning point: Kuna kijana dalali, kapambana sana na udalali, akanunua kaplot, miaka kadhaa ikapita yale maeneo yakahitajika na kanisa, ofa ya bei aliyopewa ikawa turning point.

Sasa wakati anasema historia yake, ili atoe hamasa inabidi aseme hiyo turning point na kushauri kuwa ukiwa unafanya kazi wekeza kwenye Asset hata kwa kidogo unachopata.
 
Huyo anaitwa mdaka five vipi hajasema mbao za magendo , hajasema mafuta ya magendo, hajasema korosho za magendo toka msumbiji, vipi hajasema mafuta ya petrol ya magendo akisema hayo uje unieleze hapa, mueleze mbinga mbinguni ni pazuri
Mkuu una za ndani kabisa au unamchafua tu?
 
Tatizo Ni Nchi Za Afrika Hazitoi Fursa Za Kutajirika Kwa Njia Za Halali Either Mfumo Ukubebe Au Kalumanzila Atahusika Au Toa Damu Pata Pesa.
 
Huyo anaitwa mdaka five vipi hajasema mbao za magendo , hajasema mafuta ya magendo, hajasema korosho za magendo toka msumbiji, vipi hajasema mafuta ya petrol ya magendo akisema hayo uje unieleze hapa, mueleze mbinga mbinguni ni pazuri
Duh! Je hajawahi pewa tenda za kusupply vifaa vya ujenzi kwenye miradi ya halmashauri na wilaya? Hizo tenda mtu kupata 100m hadi 500m ni kawaida. Cha msingi ukubali kutoa 10%



Au yeye ni geresha tu. Inawezekana ni mradi mtu mzito.



Au kapata hela kupitia connection
 

Mkuu kuandika kiingereza complicated cha darasani doesn't mean kwamba you're right, it just shows kwamba una ka-ushamba fulani na lugha ya kiingereza.

Inashangaza sana kumuona myu anayetaka ushahidi kila mara kuhusu mada za imani, leo anafanya 360 kwa kitu chepesi kama hiki.

Kwa hiyo mada ikiripotiwa na chanzo kimoja ndo inakosa credibility? Hiyo tip ya fact checking nani alikupa?

Kwa hiyo ITV, Clouds na TBC wangechukua the same news piece wakaipost kwao, ndo inakuwa credible?

Mbona ulikuwaga very logical mkuu, au umeingia UVCCM?
 
Na We Tupe Ushahidi Kama Anasema Kweli!
 
Thobias kahimba si ndo mchungaji thoby? Mbona kama story yake hii ina mapengo. Yani uchome cd mbinga huko hadi uwe milionea?
 
Mwandishi Amekwenda Kuona Kitu Kilichokamilika La Sivyo Alete Video Ya Wakati Anatafuta Hizo Bilioni Kusema Ni Lahisi.

Ila Hakuna Ushahidi Kwamba Ni Utajiri Wa Halali Au Wa Magumashi Usiamini Kila Lisemwalo Kisa Tu Amesema Mtu Mwenye Mabilioni .
 
Hujasema wewe billionaire ulianza na mtaji kiasi gani na sasa unamiliki nini.
 
Kwahiyo unahamasisha watu waendelee kukiuka hakimiliki za biashara za watu au unamaanisha nini?
 
Tunaye hapa mbinga ila kuhusu utajiri wake siri anajua mwenyewe , na asituchoshe Kwa story za kuburn CD 😁
Nadhani kuna jambo tunaliacha hewani. Kama jamaa ametaja kuwa kaanza na kuchoma CD, haimaanishi kuwa kazi hiyo ndiyo imemletea umilionea.
Lazima kuna biashara aliianzisha na ikafanikiwa iliyomwingizia pesa nyingi hapo katikati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…