Video: Vijana kuweni serious. Kuna huyu Thobias Kahimba alianza kwa kuchoma CD kwa Tsh 100 hadi amekuwa Bilionea. Mnakwama wapi?

Video: Vijana kuweni serious. Kuna huyu Thobias Kahimba alianza kwa kuchoma CD kwa Tsh 100 hadi amekuwa Bilionea. Mnakwama wapi?

Acha mawazo potofu
Sijui kwanini watu huwa hawasemi turning point, Kuna ile point inayotrigger mafanikio yako. Hiyo ndiyo inayoleta hamasa.

Mfano wa turning point: Kuna kijana dalali, kapambana sana na udalali, akanunua kaplot, miaka kadhaa ikapita yale maeneo yakahitajika na kanisa, ofa ya bei aliyopewa ikawa turning point.

Sasa wakati anasema historia yake, ili atoe hamasa inabidi aseme hiyo turning point na kushauri kuwa ukiwa unafanya kazi wekeza kwenye Asset hata kwa kidogo unachopata.
 
Huyo anaitwa mdaka five vipi hajasema mbao za magendo , hajasema mafuta ya magendo, hajasema korosho za magendo toka msumbiji, vipi hajasema mafuta ya petrol ya magendo akisema hayo uje unieleze hapa, mueleze mbinga mbinguni ni pazuri
Mkuu una za ndani kabisa au unamchafua tu?
 
Vijana hawakubali kuamini kuna wanaoanza from scratch na kufanikiwa. Wanaamini kila aliefanikiwa kapitia njia za panya ambazo hasemi. Hii yote ni ku justify kuwa kufeli kwao ndio kawaida ya maisha.

Hata mimi nimechoka mbaya ila naamini wapo matajiri waliofanikiwa from scratch kwa juhudi na jasho lao sio njia za mkato. Nimefeli kwasababu kuba vitu nimekosea kwenye mapambano.
Ukikaa na waliofanikiwa utajiona ulikosea wapi. Sisi wengine hatuna muda wa kubadili ila vijana muda bado mnao badilikeni bado mna nafasi ya kutoaboa. Ila ukiamini huwezi kutoboa bila njia za mkato endelea tu tena unatakiwa utumie hizo njia ufanikiwe.
Tatizo Ni Nchi Za Afrika Hazitoi Fursa Za Kutajirika Kwa Njia Za Halali Either Mfumo Ukubebe Au Kalumanzila Atahusika Au Toa Damu Pata Pesa.
 
Huyo anaitwa mdaka five vipi hajasema mbao za magendo , hajasema mafuta ya magendo, hajasema korosho za magendo toka msumbiji, vipi hajasema mafuta ya petrol ya magendo akisema hayo uje unieleze hapa, mueleze mbinga mbinguni ni pazuri
Duh! Je hajawahi pewa tenda za kusupply vifaa vya ujenzi kwenye miradi ya halmashauri na wilaya? Hizo tenda mtu kupata 100m hadi 500m ni kawaida. Cha msingi ukubali kutoa 10%



Au yeye ni geresha tu. Inawezekana ni mradi mtu mzito.



Au kapata hela kupitia connection
 
Hujaelewa hoja yangu.

Huwezi kufanya abstract thinking.

Sijasema he is not any of those things he claims.

Nimesema habari ya chanzo kimoja ina low credibility, ili habari iwe ya kuaminika inahitaji kuwa supported na several sources.

Unaelewa tofauti ya mtu kusema huyu muongo na mtu kusema habari hii haina ushahidi wa kutosha kukubalika?

Niki comment habari ambayo haijahakikiwa hilo halimaanishi kuwa hii habari imehakikiwa.

That is a non sequitur logical fallacy.

But I suspect you don't know what that is, if you even know what a logical fallacy is at all.

Mkuu kuandika kiingereza complicated cha darasani doesn't mean kwamba you're right, it just shows kwamba una ka-ushamba fulani na lugha ya kiingereza.

Inashangaza sana kumuona myu anayetaka ushahidi kila mara kuhusu mada za imani, leo anafanya 360 kwa kitu chepesi kama hiki.

Kwa hiyo mada ikiripotiwa na chanzo kimoja ndo inakosa credibility? Hiyo tip ya fact checking nani alikupa?

Kwa hiyo ITV, Clouds na TBC wangechukua the same news piece wakaipost kwao, ndo inakuwa credible?

Mbona ulikuwaga very logical mkuu, au umeingia UVCCM?
 
Yeye ameleta story ya maisha yake, unachobisha ni nini? Ulikuwa wakati anatafuta?

Au wewe ni ndugu yake?

Story za Steve Jobs, Elon Musk, Bill Gates na Mark mnaziamini ila akija Mbongo mwenzenu mnaleta ubishi.

Hebu tupe ushahidi kwamba anadanganya?
Na We Tupe Ushahidi Kama Anasema Kweli!
 
Thobias kahimba si ndo mchungaji thoby? Mbona kama story yake hii ina mapengo. Yani uchome cd mbinga huko hadi uwe milionea?
 
Mwandishi ameenda hadi kwenye biashara zake. What else do you want?

Kama umeangalia hiyo video. Yupo kwenye hardware na kuna watu kweli amewaajiri na no wengi

Ulitaka akuletee bank statement ndo uamini?

Kwa hiyo habari zote za Azam TV wabongo mnaamini ila mtu kuelezea utajiri wake ndo mnaanza kuleta doubts.

Nimekwambia uniletee ushahidi kuwa hana hizo hela au hakuanza kwa kuchoma CD unaangaika tu.

Ushahidi wako uko wapi?
Mwandishi Amekwenda Kuona Kitu Kilichokamilika La Sivyo Alete Video Ya Wakati Anatafuta Hizo Bilioni Kusema Ni Lahisi.

Ila Hakuna Ushahidi Kwamba Ni Utajiri Wa Halali Au Wa Magumashi Usiamini Kila Lisemwalo Kisa Tu Amesema Mtu Mwenye Mabilioni .
 
Wakuu,

Kuna muda kama vijana inabidi muwe serious na maisha.

Kuna huyu kijana nimemuona huko Azam TV anasema alianza kwa kuchoma CD yaani nyimbo moja alikuwa anaweka kwa Tsh 100 aka-fight sana.

Anasema alikuwa kwa siku alikuwa anatumia 1000 mpaka 1500 tu kuna kipindi mpaka akaumwa vidonda vya tumbo.

Sasa hivi ni Bilionea mkubwa tu. Ana duka kubwa la hardware na anafanya mambo ya usafirishaji na ameajiri watu wengine 71

Sasa vijana mnakwama wapi kuwa kama huyu? Kuweni serious

Hujasema wewe billionaire ulianza na mtaji kiasi gani na sasa unamiliki nini.
 
Kwahiyo unahamasisha watu waendelee kukiuka hakimiliki za biashara za watu au unamaanisha nini?
 
Tunaye hapa mbinga ila kuhusu utajiri wake siri anajua mwenyewe , na asituchoshe Kwa story za kuburn CD 😁
Nadhani kuna jambo tunaliacha hewani. Kama jamaa ametaja kuwa kaanza na kuchoma CD, haimaanishi kuwa kazi hiyo ndiyo imemletea umilionea.
Lazima kuna biashara aliianzisha na ikafanikiwa iliyomwingizia pesa nyingi hapo katikati.
 
Back
Top Bottom