Hakuna namna Hamas washinde Israel, haiwezekani vinginevyo wapalestina wataisha, wapalestina wangeweza kuwaunga mkono endapo Hamas wangejitoa kupigana na Israel, lakini kitendo cha hamas kupigana na kujificha kwa raia huo ni uuaji mkuu sana. Palestinians imepoteza watu zaidi ya elfu 26, hapo majeruhi watakuwa ni wengi, bado hamas na wananchi wa kawaida wengi wamekamatwa na jeshi la Israel. Bado wapalestina zaidi ya laki 1 wamefukuzwa kazi kule Israel, dunia iache ujinga, nawashauri watu wa Ghaza, West bank na Israel wakubaliane waishi pamoja ndani ya nchi moja ya Israel ili maisha yasonge mbele, kwa sababu haitawezekana Israel kuachia ardhi eti nchi inagawanywa, waarabu wa Palestinians wasitangulize maslahi ya dini , uzuri kule wayahudi wengi waliotoka Ulaya hawana habari na mambo ya Udini, wenye Udini ni wayahudi wachache sana marabii ambao hawana hata nguvu yoyote, mfano mzuri kuna waarabu , waislamu, wakristo ambao wanaishi Israel na wengine ni viongozi wa kisiasa, wanafurahia maisha, suluhisho ni kuundwa taifa moja tu la Jamuhuri ya Muungano wa Israel na Palestiniana. Kama ilivyo nchi ya Trinidad & Tobago.