Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Huko Kinondoni kumetokea zogo na vurugu mtaani baada ya raia kugoma mwenzao kuondoka na mtu aliyejitambulisha kama afisa wa Jeshi La Polisi Ukonga.
Katika video hiyo, mwanaume mmoja alijitambulisha kama Polisi alikuwa akitaka kumchukua kijana mmoja kinyemela.
Wananchi baada ya kuona tukio hilo, walimzingira Polisi huyo na kuanza kumuuliza maswali mbalimbali ikiwemo kwanini hajavaa nguo za kiaskari, kwanini hana gari la Polisi, kama yeye ni Polisi kutoka Ukonga kwanini anakuja Kinondoni kukamata?
Tukio hili linakuja siku chache tangu afisa mmoja wa TRA kupigwa mpaka kufa wakati anajaribu kumkamata raia wa kawaida bila kufuata utaratibu.
Ndio kusema kwamba watanzania wameanza kuamka?