Video: Vurugu zazuka Kinondoni baada ya raia kugoma mwenzao kuchukuliwa na Polisi wakihofia Polisi huyo kuwa mtekaji

Video: Vurugu zazuka Kinondoni baada ya raia kugoma mwenzao kuchukuliwa na Polisi wakihofia Polisi huyo kuwa mtekaji

At the end of the day kama ni muhalifu watamuweka ndani
 
Naomab kurudia tena , we are not that special, they are not that special. Soon watagundua
Mkuu yaan ujue sis watz yamkin kuna mahali tumerogwa sio bure.Tunajiona kama nchi pekee yenye vyombo vya usalama,nakwamva nchi ambazo znamachafuko hazina jeshi,polisi wala secret services au pengne wananch wao hawana akili Ndo maana unakuta washabiki wa vyama na baadhi ya viongoz hawaoni kama haya matukio yanaweza kuzaa kitu ambacho kitatushangaza.
 
Wakuu,

Huko Kinondoni kumetokea zogo na vurugu mtaani baada ya raia kugoma mwenzao kuondoka na mtu aliyejitambulisha kama afisa wa Jeshi La Polisi Ukonga.

Katika video hiyo, mwanaume mmoja alijitambulisha kama Polisi alikuwa akitaka kumchukua kijana mmoja kinyemela.

Wananchi baada ya kuona tukio hilo, walimzingira Polisi huyo na kuanza kumuuliza maswali mbalimbali ikiwemo kwanini hajavaa nguo za kiaskari, kwanini hana gari la Polisi, kama yeye ni Polisi kutoka Ukonga kwanini anakuja Kinondoni kukamata?

Tukio hili linakuja siku chache tangu afisa mmoja wa TRA kupigwa mpaka kufa wakati anajaribu kumkamata raia wa kawaida bila kufuata utaratibu.

Ndio kusema kwamba watanzania wameanza kuamka?

View attachment 3173103


View attachment 3173105
Kama watanzania tutaendelea hivi basi maendeleo tutayaona maana watz 5w +h question hatunaga
 
Ccm ikitaka itolewe madarakani ni kwa kuendelea kutumia vibaya Jeshi la Polisi. Maana hizi shida ndogondogo za kila siku zitapelekea wananchi kuwaona askari wa kawaida anaweza akavimbiwa tuu na asifanye chochote, sasa siku yanatokea maandamano polisi wanajikuta hawana nguvu tena
Katiba mpya tu ndiyo kimbilio
 
Siku hizi hawa under cover watapata tabu sana kuteka mtu imekuwa ngumuu balaaa labda mvizie akiwa peke yake.
 
Mbna kama maigizo tu haya? Aliyetekwa mwenyewe yupo yupo tu wanaompigania ni wakina mama tu yeye wala hajipambanii😄
 
Safi sana, polisi walichokitengeneza wataona matunda yake jinsi muda unavyokwenda.

Nawapongeza wananchi wa eneo hilo kwa kutambua na kutumia haki yao kikatiba kujilinda.

Jana nilikuwa napitia ile video ya Nape kutolewa bastola 2017 ukifuatilia ile video utagundua watekaji wanavyokuja na ukizubaa jinsi wanavyokuteka.

Nape anasikika akimwambia mtekaji jitambulishe, ila badala ya mtekaji kujitambulisha kwa kutoa kitambulisho chake badala yake anatoa bastola aliyoificha.

Jeshi la polisi kupitia waziri wa mambo ya ndani kipindi hicho lilimkana huyo mtu kuwa sio mtumishi wa jeshi la polisi wala wizara ya mambo ya ndani na hiyo habari iliishia pale pale.

Mimi na wewe tujiulize kama ni kweli polisi sio wahusika nani anaweza kujitokeza kutishia kumteka waziri kwa kutoa bastola hadharani kwenye umati mkubwa kama ule kama sio polisi?


View: https://youtu.be/WqAGTpuRFSg?si=8v3mpisiUGybpEfe
 
Back
Top Bottom