Video: Vurugu zazuka Kinondoni baada ya raia kugoma mwenzao kuchukuliwa na Polisi wakihofia Polisi huyo kuwa mtekaji

Video: Vurugu zazuka Kinondoni baada ya raia kugoma mwenzao kuchukuliwa na Polisi wakihofia Polisi huyo kuwa mtekaji

1. Polisi wanatumika kisiasa.
2. Uthamani wa Raia ktk Nchi Umetoweka.
3.Wenye mamlaka hawatoi ufafanuzi wasiojulikana ni nani.
4. Jeshi la Polisi linajikingia kifua kwa Kila Jambo kua wao wako sahihi ila ukitazama Kuna udhaifu mkubwa unaonekana juu ya swala la Watu kutetwa why wasitolee ufafanuzi Ili swala la kutekana tekana.
5.Wananchi wanakosa Imani na Jeshi la Polisi, mwisho wa siku wananchi watakosa Imani na Serikali.
6.Waliomadarakani Hawataki kukosolewa, Why msikosolewe, wananchi wanakua na maumivu ya ndani kwa ndani, mmatengeneza sumu mbaya kwa Jamii kwenda kwa Jeshi la Polisi au Serikali, watu watapoteza Imani na Serikali na ikitokea siku Viongozi wa Serikali wamekutwa na tatizo Wananchi au Baadhi ya Wananchi Hawatokua na Moyo wa simanzi kwa Viongozi wao.
Mfano mzuri soma Comment za watu juu ya Ajari ya Gari la Bunge ndo utaelewa nn kinaendelea ktk miyoyo wa watu juu ya Viongozi wao.
 
Maneno ya Mzee Warioba watu wengine wanayachukulia poa tu lakini yana uzito mkubwa sana.

Tunajiona tuko special sana kwamba hii erosion of trust and national unity haiwezi kutuharibia nchi, we are not that special.
Naomab kurudia tena , we are not that special, they are not that special. Soon watagundua
 
Ndivyo inavyotakiwa....tunapokataa matukio ya kutekana sio kwamba tunatetea uharifu.

Waharifu wataendelea kukamatwa na kushtakiwa kwa makosa yao.
Hii ya kutekana ilitaka kuchukuliwa kama Loop Hole ya waharifu wa kwenye system.

Wanakulilua risasi wanaenda kulipoti kwamba ulitaka kupindua nchi. Imeisha hiyo
Polisi ni waadilifu sana hawana hizo mbanga ni vile tu wamepakwa sana matope na hawana time ya kujitetea
 
Safi sana hiyo nzuri sana na waendelee kufanya hivyo hivyo sio kila siku tunasikia mtu katekwa harafu tunakuja kuambiwa kuwa wamemwacha ajitambui hao ni wahuni tu inabidi wapate kipigo sasa hivi..
 
Polisi ni waadilifu sana hawana hizo mbanga ni vile tu wamepakwa sana matope na hawana time ya kujitetea
Polisi wa wapi hao? I agree kuna wale mema wapo, kazi zimenyooka na utendaji umetukuka. Halaf kuna wale wahuni, wao ni misconducts tu, ndio hao wanakosana na watu daily
 
Wakuu,

Huko Kinondoni kumetokea zogo na vurugu mtaani baada ya raia kugoma mwenzao kuondoka na mtu aliyejitambulisha kama afisa wa Jeshi La Polisi Ukonga.

Katika video hiyo, mwanaume mmoja alijitambulisha kama Polisi alikuwa akitaka kumchukua kijana mmoja kinyemela.

Wananchi baada ya kuona tukio hilo, walimzingira Polisi huyo na kuanza kumuuliza maswali mbalimbali ikiwemo kwanini hajavaa nguo za kiaskari, kwanini hana gari la Polisi, kama yeye ni Polisi kutoka Ukonga kwanini anakuja Kinondoni kukamata?

Tukio hili linakuja siku chache tangu afisa mmoja wa TRA kupigwa mpaka kufa wakati anajaribu kumkamata raia wa kawaida bila kufuata utaratibu.

Ndio kusema kwamba watanzania wameanza kuamka?

View attachment 3173103


View attachment 3173105
Mbuyu ulianza kama mchicha!
 
Looooh! Jamani nchi inaelekea kutotawalika ,hivi watanzania tumekosea wapi? Huu moto ukienea nchi nzima hivi nchi hii itakuwaje? Naona giza
 
Watu wa dar tatizo kweli, yaani mtu analeta sitofahamu kwa kumkaba mtu halafu mnamuimbia pambio badala ya kumtandika na kumtia kiberiti?🤔🤔🤔
 
Back
Top Bottom