Huko Kinondoni kumetokea zogo na vurugu mtaani baada ya raia kugoma mwenzao kuondoka na mtu aliyejitambulisha kama afisa wa Jeshi La Polisi Ukonga.
Katika video hiyo, mwanaume mmoja alijitambulisha kama Polisi alikuwa akitaka kumchukua kijana mmoja kinyemela.
Wananchi baada ya kuona tukio hilo, walimzingira Polisi huyo na kuanza kumuuliza maswali mbalimbali ikiwemo kwanini hajavaa nguo za kiaskari, kwanini hana gari la Polisi, kama yeye ni Polisi kutoka Ukonga kwanini anakuja Kinondoni kukamata?
Tukio hili linakuja siku chache tangu afisa mmoja wa TRA kupigwa mpaka kufa wakati anajaribu kumkamata raia wa kawaida bila kufuata utaratibu.
Wananchi wanarudisha mamlaka mikononi mwao yaliyoporwa na utawala dhalimu wa serikali ya chama dola kongwe ya kibaguzi inayotumia mamlaka zake vibaya kupitia matumizi haramu ya vyombo vya usalama.
Mama em fanya kitu...tatizo watu wakifa mnaongea tu hamchukulii serious...
Mngeanza kwa kuua hao police wanaochukua watu....
Sasa hii kimya mnakuwa mnajichora sana
Ccm ikitaka itolewe madarakani ni kwa kuendelea kutumia vibaya Jeshi la Polisi. Maana hizi shida ndogondogo za kila siku zitapelekea wananchi kuwaona askari wa kawaida anaweza akavimbiwa tuu na asifanye chochote, sasa siku yanatokea maandamano polisi wanajikuta hawana nguvu tena
Wananchiu wapo sahihi kabisa kwa sababu wasiojulikana wamekuwa wengi,kutokuwepo ama kutokufuata taratibu za ukamataji kutaligharimu taifa hili.
Huu ni mwanzo tu, na ipo siku hata askari wenye sare hawatoaaminika mbele ya wananchi na ipo siku wananchi wataamua kuwadhibiti wakamataji na watekaji.
Haya ndo matunda ya utekaji, huu ni mwanzo, muda si mrefu tutaelekea pabaya iwapo hakuna hatua zitakazochukuliwa dhidi ya watekaji na wasiojulikana.