Lissu hakuwepo kwa sehemu kubwa ya awamu hii na wa kulaumu sio yeye bali ni waliobaki nyuma ndio walifanya kosa kubwa ambalo sasa linawagharimu kuhusiana na tume ya uchaguzi.Kama ni matatizo yetu tuyajadili wenyewe, siyo mtu anatuletea mambo ya Kenya kama rejea ya mafanikio na majivuno yao bandia. Nayaita bandia kwa sababu wakenya kila wakati wanajiona eti wako bora kuliko sisi wakati kisiasa wako hovyo kabisa. Baada ya Rwanda, ndo pekee waliouwana ktk ukanda huu kwa sababu za uchaguzi. Bahati mbaya sana sisi, kama unavyoona akina dikteta2020 anamwita mtu ni mchambuzi wakati hana lolote! Mafanikio ni mfumo siyo kuandikwa tu ktk katiba. Z'bar tume ilipalaganyika pamoja na kwamba ilikuwa na uwakilishi wa vyama vyote vikuu!
Hapa kwetu mambo yako hovyo kabisa na tunaostahili kulalama ni sisi wananchi. Hawa wanasiasa wetu wa upinzani wako hovyo maana ndo wamekuwa Bungeni miaka yote wakifanya show off. Wanalalama ili sisi wananchi tuwasaidie kurudi Bungeni, wakifika hatuwasikii wakitia presha juu ya mambo ya msingi. Leo hii tusingekuwa na mkuu wa mkoa au wilaya anayejihusisha na siasa za CCM. Wako kimya wakihangaikia kusikika Bungeni kwa matusi nk. ili uchaguzi ukifika warudishwe.
Mtu kama Lissu nilitegemea apambane na mambo kama hayo na jumuiya ya kimataifa, badala yake yeye ana mwanasheria anayemlinda, yeye akiwa nje ya nchi; zoezi la kijinga kuliko yeye mwenyewe anavyoamini. Yaani ashinde wakati majimbo yako chini ya wakurugenzi, usalama uko chini ya mkuu wa wilaya, na mkuu wa wilaya ni mkuu wa usalama wilayani? Halafu unategemea vitisho na kujivuna eti tutawapeleka mahakamani! Trash!
Kwa vyovyote vile baada ya uchaguzi mkakati sasa lazima uwe ni katiba mpya itakayotoa fursa ya nchi kupata pia na tume huru ya uchaguzi ili tuachane na chaguzi za kihuni na hata ikilazimu nchi kuwekewa vikwazo, tuwekewe tu. It's worth it.