Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 12,463
- 27,556
Kwanini nimesema una uwalikini mkubwa?
Vile tunashuhudia humu jukwaani hata huko uraiani mambo ni yaleyale.
Kuna jamaa walikuwa wanatambiana kuwa ana nguo za kulalia nyingi kiasi kwamba mademu wakija getoni kwake wanaziiba!
Mwingine huwa anaandika hadi thread za kutuhamasisha wanaume tusikilize mziki wa Taarabu!
Kuna jamaa sikumbuki uzi ule ulikuwa unasemaje zaidi ila nakumbuka ulikuwa unazungumzia Dressing table.
Jamaa mmoja aliyejitamba kuwa anaishi mlimani city sijui apartment yake analipia 600k kwa mwezi yeye alipost meza yake ya chumbani ilivyosheheni mapodozi ya kila aina jambo lililo niacha mdomo wazi.
Humu Kuna mambo huwa yanafanywa na wanaume wa Dar huwa yanatuacha Hoi sisi wanaume wa mikoani.
Maana mimi hadi nakua nilijua lotion ni za wanawake tu kitu ambacho kimeniathiri hadi maana ni ngumu sana mimi kupaka lotion!