KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Rafiki Erythrocyte, ulikuwa umeanza kupiga hatua kadhaa mbele, ni kitu gani kinakurudisha nyuma sasa?Tuliwaambia mapema sana kwamba ndani ya Chadema hakuna mkubwa kuliko Chama , sasa wametimuliwa wanaanza kutia huruma .
Mzee Lwakatare ulipiganiwa na chama kwa kiwango cha kutisha mno , ukatolewa ndani ya mdomo wa mamba ili uishi tena leo unasaliti bila aibu , Umevuna ulichopanda
View attachment 1447377
Usipoteze umakini mkuu, soma alama za nyakati na uzielewe vyema.
Nyinyi CHADEMA mmefika hapa kwa taabu sana, kwa nini muendelee kuwa na kumbukumbu fupi kiasi hiki kama sisi waTanzania wenzenu?
Tunawategemea nyinyi muwe mnatukumbusha tunaposahau haraka manyanyaso tunayofanyiwa na hawa watawala; sasa hata nyinyi mkianza kuwa na kumbukumbu fupi kiasi hiki, nani atamkumbusha mwenzie?
Hebu soma vizuri maneno aliyotumia kichaa Ndungai Bungeni kuwahusu hao wabunge unaosema watalia.
Kwani unadhani waliyofanya ya kukaidi maelekezo ya chama makusudi mazima walikuwa hawajui kwamba wanayo kinga?
CHADEMA, mnahitaji watu makini sana kwenye vitengo vyenu wenye mikakati ya kuzijua mbinu hizi. Acheni ubahiri na kutumia ruzuku sehemu isiyoleta tija kwenye chama.
Ndungai kamtangazia Mbowe waziwazi, tena Bungeni, kwamba harudi tena kwenye bunge lifuatalo. Hapo mlipo, mwenyekiti wenu anatishiwa na maneno mazito haya, bado mmetulia tuli kama hakuna lililotokea?
Sasa subirini hapo Oktoba; au hata huko asifike kabisa, kwa kujua tabia za hawa watu.
Sasa hivi wamekwishatambua kwamba kizingiti kikuu cha kuisambaratisha CHADEMA ni Mbowe. Pamoja na kwamba walidhani wangeimaliza CHADEMA mapema, lakini hawakujua Mbowe anazo nguvu kiasi gani ndani ya chama.
Wamejaribu kumwondoa kwa kesi/jela imeshindikana, sasa wanajiapiza "Bungeni Harudi", na wanajua bunge ni mali yao na uchaguzi mkuu ni mazingaombwe!
Lakini CHADEMA kama chama na askari wake kama akina Erythro, hawana kumbukumbu za mitego yote iliyobidi waitegue. Wanasubiri huu wa mwisho uwanase na kuwasambaratisha kabisa, tena wakati wa majeruhi!
Ukiona watu wapo kimya, tena wameamua kabisa kwenda kujificha..., halafu wewe ukabaki hapo ukidhani mipango haisukwi...; wewe utakuwa ni mjinga wa kutupwa.