Sakata la sukari nchini ni ishara ya kuwa soko lipo! Sasa maamuzi yanayofanyika ndo yanaonesha tofauti ya akili za kichuuzi/kitapeli na akili za kimaendeleo.
Kimaendeleo wizara ilipaswa kubanana na viwanda vya ndani hata kwa ruzuku, stimulus packs n.k. Akili hii ingevisaidia viwanda hivyo kuongeza uzalishaji, kurahisisha bei na kuongeza ajira kwa raia (kwa muda mrefu)
Akili za kichuuzi na kitapeli ni kama alizochukua Bashe za kulifanya sakata la sukari kuwa huria hadi kampuni za stationery zikajihusisha. Economic leakages, Short-term fixs, 10% based solutions kimsingi zinanufaisha zaidi nchi inakotoka sukari.
Tuache uchumi tuje kwenye afya: Je, ni wewe au Bashe au nani anaweza kuthibitisha UBORA wa hizo sukari kwa matumizi na afya za WaTanzania? Hivi kampuni isiyokuwa na uzoefu au weledi wa ununuzi wa sukari inaweza kuwa na check & balance kuhakiki ubora? Au kipaumbele kilikuwa sukari ipatikane hata kama ni sumu?
Alafu unashangaa kuna watu wanahoji mbona tuna ardhi hatulimi kwa faida... mbona tuna vijana hawana kazi... mbona maradhi na matatizo ya kiafya yanaongezeka!
Kwa akili za kichuuzi na kitapeli tusahau. Tutaishia tu kuwasindikiza wengine huko duniani.
Akili za kimaendeleo zingejiuliza: Kama watu washatengenezwa vichwa kiasi kwamba hawawezi kuishi bila sukari ni kwanini tusiwafanye kuwa mradi wa kilimo wenye tija!?
NB: ONYO: SUKARI ya kigeni ni hatari kwa afya. Kama unaweza kuishi bila hiyo sukari fanya hivyo!