Video: Watu watatu waanguka kutoka kwenye ndege inayoondoka Kabul (Afghanistan)

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Shirika la Habari la Aśvaka limeripoti kuwa vijana watatu wamefariki baada ya kudondoka kutoka kwenye ndege walipokuwa wakijaribu kuondoka kutoka Kabul, Afghanistan.

Mapema leo, mamia ya raia wa Afghanistan walionekana wakiwa kwenye uwanja wa ndege wakitaka kupanda kwa nguvu kwenye ndege ya Jeshi la Marekani (USAF) aina ya Boeing C-17 iliyokuwa ikiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamid Karzai mjini Kabul. Video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii, ambazo hazikuthibitiswa zilionesha watu wawili wakidondoka kutoka kwenye ndege hiyo.

Chanzo: Aśvaka News Agency

⚠️ TAHADHARI ⚠️

Video hizi zina maudhui ya kuogofya

1629106451990.png

1629106487426.png
 
Wametangaza kuwa nchi ya kifalme ya kiislamu, na wananchi wake wote ni waislamu sasa shida iko wapi? Wanaokimbia sio waislamu?
Sharia za kiislamu waislam wenyewe tunaziogopa ,ww ukikutwa unazini ukiwa ushaoa adhabu yako unafukiwa mwili mzima kinabaki kichwa tu kinapigwa mawe mpk unakufa na mkizini wote hamjaoa wala kuolewa adhabu yenu fimbo 100 kila moja sasa kwann watu wasidandie ndege
 
Daaah aisee yani apo hao wananchi wanatamani roho ya huryma iwaingie wajeda wa kimarekani wawabebe na wao. Raisi wao keshachochora kitambo .

Hao taliban kwanini wanakimbiwa na wananchi wake?? Maana nimeskia kua serikali ya afghanistan imeomba hao wanamgambo wasiwadhuru raia wanaoikimbia nchi, na wanamgambo wametoa ruhusa kwa anaehama ahame mapema.

Kipi kinachowaogopesha wananchi namna hiyo?? Mpaka wanadandia ndege si mchezo aisee.
 
Kwani watu wanakimbia ?waasi wanapoingia madarakani Mara nyingi wao wanapindua serikali na kukaa madarakani Sasa hapo wananchi kwanini wanaamua kukimbia mbona sielewi
Taliban sio sauti ya wananchi ni kundi lina sera zake kama kutomruhusu mwanamke kuongoza. Linaruhusu biashara haramu kama drugs na human trafficking na linaua ovyo. Hao wanaokimbia ni wale wasiofaa kuishi kwenye serikali kama hii. Wafanyakazi wa serikali iliyopita na familia zao, wageni, wapinzani wa Taliban (yenyewe haiaminiki)
 
Sharia za kiislamu waislam wenyewe tunaziogopa ,ww ukikutwa unazini ukiwa ushaoa adhabu yako unafukiwa mwili mzima kinabaki kichwa tu kinapigwa mawe mpk unakufa na mkizini wote hamjaoa wala kuolewa adhabu yenu fimbo 100 kila moja sasa kwann watu wasidandie ndege
Na wanajua watazini...🤣🤣
 
Kwahiyo we unaonaje uzinifu ni mzuri ama lah?
 
Sijaon
Shirika la Habari la Aśvaka limeripoti kuwa vijana watatu wamefariki baada ya kudondoka kutoka kwenye ndege walipokuwa wakijaribu kuondoka kutoka Kabul, Afghanistan.

Mapema leo, mamia ya raia wa Afghanistan walionekana wakiwa kwenye uwanja wa ndege wakitaka kupanda kwa nguvu kwenye ndege ya Jeshi la Marekani (USAF) aina ya Boeing C-17 iliyokuwa ikiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamid Karzai mjini Kabul. Video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii, ambazo hazikuthibitiswa zilionesha watu wawili wakidondoka kutoka kwenye ndege hiyo.

Chanzo: Aśvaka News Agency

⚠️ TAHADHARI ⚠️

Video hizi zina maudhui ya kuogofya

View attachment 1894361

View attachment 1894353

View attachment 1894354

View attachment 1894355
Sijaona mtu aloanguka, wala sijaona picha za kuogofya, acheni propaganda za kijinga
 
Back
Top Bottom