DOKEZO VIDEO: Wazazi angalieni Walimu Shule ya Sekondari Majaliwa

DOKEZO VIDEO: Wazazi angalieni Walimu Shule ya Sekondari Majaliwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mtu unamuona anamchapa mtoto sana au anapitiliza ! Kwanini huo muda wa kumrekodi usitumie kumnyang'anya fimbo huyo mwalimu?

Ili asimuumize mtoto !! Serikali iwe inawafukuza hata wanaorekodi ! Jifunzeni kuonyana na kuelemishana nyie kwa nyie.

Yaani kama una uwezo wa kushuhudia na kurekodi mtoto anapigwa hivyo , maana yake hata wewe ni katili unamrekodi katili mwenzio.

Huku mtandaoni tumewachoka ! Kila siku nyie kurekodiana tu au ndo fashion Walimu
 
Mtu unamuona anamchapa mtoto sana au anapitiliza ! Kwanini huo muda wa kumrekodi usitumie kumnyang'anya fimbo huyo mwalimu...
Usikimbilie kulaumu bro,unafikiri mimi naweza angalia na nikamuacha,alie record ni miongoni mwa hao waalim nimetumiwa tu fanya namna huu unyama uishe sio kunilaumu mimi.

Shule ipo kusini inaitwa Qassim Majaliwa Secondary school...so kazi kwako,sijaileta hapa ili iwe watu ku enjoy..we need to do something wewe na mimi.
 
Wakipiga marufuku kupiga mashuleni,
Hata ukatili majumbani utapungua pia
Serikali ndio chanzo cha ukatili na wanashindwa kutoa maamuzi magumu

Huwezi kusema tu tutaliangalia
PM hana maamuzi peke yake ni lazima lijadiliwe kwa upana

Kila leo tunasikia ooh nchi ya Amani lakini kuna ukatili zaidi ya nchi zenye vita
Mara baba kamlawiti mwanae, wanawalawiti na watoto wanashindwa kusema kwa sababu na shule wakienda wakishindwa kujibu wanachapwa na hao wapumbavu badala ya kumuuliza mtoto nini kinachokusibu mpaka unakuwa mnyonge hivyo?

Mwalimu hana ukaribu na mwanafunzi anamuona kama adui yaani kama mfungwa na gereza au mgonjwa na nesi au doctor yaani wote wamoja

Hii ni kwa sababu hatuongei kwa kutaka kujua tatizo na kutatua bali ni matusi, kufoka, adhabu na fimbo na hata kuuwa kabisa

Poleni sana kama hamtabadilika mtaishi kama wanyama tu
 
Ktk nchi hii kada ambayo inawatu hamnazo Basi ni hii kada, hata wewe uliyeleta hii video hopeless kabisa.haya Mambo muwe mnaonyana wenyewe huko, mnatia aibu, tumewachoka mitandaoni. Kwanza hapo uliporekodi tayari wamekugundua kuwa wewe ndio mnoko, pochi lako linaonekana, dawati ulilokaa. Hii kada inawatu wa ajabu kweli.
 
Mtu unamuona anamchapa mtoto sana au anapitiliza ! Kwanini huo muda wa kumrekodi usitumie kumnyang'anya fimbo huyo mwalimu...
Hapana! Kuna walimu ni wabishi hata wakizuiwa hawako tayari kubadilika.
Wanahamishia stress zao za kutolipwa madai, kwa wanafunzi. Idadi ya wanafunzi ni kubwa kuliko uwezo wao.

Fikiria, wanafunzi wako zaidi ya 200 kwenye chumba kimoja cha darasa; mwalimu anaambiwa ahakikishe wote wanajua kusoma na kuandika vizuri. Ama sivyo atawajibishwa. Kwahiyo baadhi yao wanatumia nguvu zaidi kuliko mbinu.

Serikali iingilie kati. Siku hizi ukatili mashuleni unazidi kushika kasi.
 
Walimu was Kizazi kipya na wanafunz wa dot com.

Huwez ukamrekodi mwenzio unakuaa unahatarisha kazi yake.

Huwezi ukaacha kuongea tukasikia hapo .. mwambie aache, amchape vi3 tu. Na azungumze na mtoto( amshauri)

Huwezi Kaa ukirekodi, location yako inaonekana, side uliuokaa kwamba hutajulikana. Yaani wewe mchukua video ni abunuasi ..halafu haka ni kadada.

Mwanaume hawez fanya huo upuuzi.

NB.
Hii shule inajitahidi kuomdoa sifuri. Jitahidi I kubaini walimu wapuuz kama mrekodi hii clip.

Walimu wachache mnaangushana huyo mwalimu namlaani Sana na ataishia pabaya. Huyu mrekodi picha. Moigaji Sina shida naye. Watoto hamueajui vzr.. tatizo mchapaji hafuati utaratibu
 
Mtu unamuona anamchapa mtoto sana au anapitiliza ! Kwanini huo muda wa kumrekodi usitumie kumnyang'anya fimbo huyo mwalimu ? ili asimuumize mtoto !! Serikali iwe inawafukuza hata wanaorekodi ! Jifunzeni kuonyana na kuelemishana nyie kwa nyie.
Yaani kama una uwezo wa kushuhudia na kurekodi mtoto anapigwa hivyo , maana yake hata wewe ni katili unamrekodi katili mwenzio.

Huku mtandaoni tumewachoka ! Kila siku nyie kurekodiana tu au ndo fashion Walimu
Prof Mkenda take note na chukua hatua
 
Wazazi walindeni waoto wenu, mtotot akikushitakia lala mbele na mwalimu mhusika. Kwa sasa hatuna walimu, ni takataka za kutesa watoto. Chukueni sheria mkononi mnusuru watoto wenu! Serikali does not care , wanusuru watoto wenu!
 
Back
Top Bottom