1. Kwa nini hii kauli ya kutofanikiwa isikike na "wazee" wa simba tu? Mbona viongozi hawatoi kauli?
2. Meneja wa Uwanja sii mwajiri wa TFF, mmiliki wa uwanja ni serikali. Sasa hawa wapangaji wanatoa wapi jeuri ya kuamua nani asimamie uwanja?
3. Huu ni ushahidi wa wazi hii yinu inaendekeza sana ushirikina. Haya yote ya kutaka meneja awapishe ni njia ya kutafuta kufanya uchawi uwanjani. Meneja hataki huo upuuzi, kama ilivyokuwa siku ya dabi.
4. Meneja anahusikaje na mbinu za kiufundi za simba mpaka "kauli" yake kwamba simba lazima wafungwe isababishe kupoteza mchezo? Meneja anaweza kuongea hivyo kama ilivyo kwa mashabiki wengine kwa mtazamo wake akizingatia ubovu wa timu iliyopo.
5. Baada ya kuchungulia kwenye rada zao za kishirikina na kubaini uwezekano wa kupata ushindi ni mdogo, waliamua kumshirikisha Mwamposa aliyewapa sharti la kutotumia ulozi, jqmvo ambalo kwa makolo ni ndoto. Sasa wamelazimika kurejea tena kwenye tunguli zilizokwama. Kwa maana nyingine hawa wazee wanaandaa mazingira ya kumshushia lawama meneja wa uwanja pale watakapotolewa. Huu ni upuuzi wa hali ya juu kabisa.