Wapi Tanzania imeuzwa?
Hii style ya uongo na kuchafua watu ndio imekuwa lifestyle ya Chadema.
Akiifanya Lissu kwa Mbowe mnajifanya mmeumia kumbe ukabila unawasumbua.
Nimesema Tanganyika ndiyo imeuzwa.
uNAKATAA Mkataba umeuona?
Pili nani ni kabila la Mbowe? una speculate tu na akili mbovu....
At least ume admit kuwa Lisu alifanya vitendo/kauli mbaya kwa Mbowe...bravo!
SAUDI ARABIA WACHUKUA BANDARI YA BAGAMOYO.Saudi Arabia imetangaza kuchukua Bandari ya Bagamoyo iliyopo ardhi ya Tanzania, kama sehemu ya mradi wake unaoitwa “East Gate”.
Mradi huo wa Saudi Arabia unaoitwa “East Gate” unalenga kuimarisha nafasi ya eneo la Bandari kama kitovu cha biashara DunianiUwekezaji huo katika bandari ya Bagamoyo unalenga kuleta uchumi mseto na kufungua masoko mapya kwa mauzo ya nje ya Saudi.
Eneo la mradi ni hekta 887, na kuifanya kuwa moja ya miradi mikubwa ya bahari katika kanda. na eneo maalumu la viwanda hekta 2,200.Fursa za uwekezaji eneo hilo zitatolewa kwa makampuni ya Saudi Arabia katika sekta kama usafiri wa baharini, vifaa, nishati na madini.
Bandari itatumika kama kituo cha masoko kwa ajili ya kusafirisha bidhaa za Saudia, hasa mafuta na mafuta ya petroli, masoko ya Afrika.Lakini Serikali ya Tanzania haijaweka wazi mkataba wa uuzaji huo wa bandari ya Bagamoyo kwa Saudi Arabia au kujadiliwa bungeni.
Mradi huo wa bandari ya Bagamoyo haujaelezwa umeuzwa kwa Saudi Arabia kwa muda wa miaka mingapi na kwa gharama za kiasi gani. Serikali ya Tanzania kupitia TPA 2024/25 ilitenga Sh22 bilioni kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi Bandari ya Bagamoyo.
Zaidi ya US$10 bilioni (takribani Sh23 trilioni) zilitarajiwa kutumika katika ujenzi huo utakaohusisha ujenzi wa bandari yenyeweUjenzi utahusisha kituo cha usafirishaji wa mizigo kwenye eneo la hekta 887, eneo maalumu la viwanda lenye ukubwa wa hekta 2,200.Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari (TPA) imekamilisha kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha mradi ukubwa wa hekta 887.
Wazo la ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo lilianza na mpango uliobuniwa na serikali ya Tanzania 2004 ulioitwa Tanzania-Mini Tiger 2020Mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ulilenga nchi yenye uchumi wa ’tiger’ kupitia viwanda kuzalisha bidhaa zitakazouzwa nje. Uulisukumwa na mafanikio yaliyopatikan katika nchi zinazoitwa ‘Four Asian Tigers’ - Korea Kusini, Hong Kong, Taiwan na Singapore Mradi wa bandari ya Bagamoyo ulianza kutekelezwa 2005, ambapo ulilenga kuendeleza kilimo, elimu, barabara, maji na uwekezaji.
Kipindi cha majaribio kati ya mwaka 2005 mpaka 2020 ulipaswa kuhusisha ujenzi wa kanda maalumu za kiuchumi (SEZ).Ukanda maalumu wa Kiuchumi wa Bagamoyo, ukawekewa misingi na Bandari ya Bagamoyo ilipoonekana ni jambo linalohitajika.Ujenzi ulizinduliwa 2015 na J.K Kikwete, ukasitishwa 2019 na J.P Magufuli kwa madai ya kuwepo masharti magumu ya mwekezaji.
Masharti; baada ya bandari kukamilika, Tanzania haitaruhusiwa kujenga na kuendeleza bandari yoyote pwani ya Bahari ya HindiMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutotakiwa kwenda kukusanya ushuru/ kodi eneo la bandari na kutaka wapewe hakikisho la miaka 33.Huku wawekezaji hao wangeweza kumiliki ardhi hiyo kwa hati ya miaka 99 pamoja na kutoruhusiwa kuulizwa nani anamiliki eneo.Swali.
Je, masharti hayo ya uwekezaji ambayo yalionekana ni magumu na ajabu kutekelezwa na John Magufuli, ndiyo yametumika sasa?Je, bunge limepata nafasi ya kujadili masharti ya uwekezaji na uendelezaji wa mradi wa Bandari ya Bagamoyo?
Bunge la ngapi na kikao gani?Serikali iliamua ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ulioanza 2023/24 usimamiwe na kutekelezwa na Mamlaka ya usimamizi wa Bandari (TPA)Nini kimewafanya TPA na Serikali 2024/25 mwezi pili tu kuwapa Saudi Arabia Bandari ya Bagamoyo ambayo tumewekeza fedha tayari?Sijaona mkataba, lakini kama ni kweli hayo masharti yapo, ni muhimu yakawekwa kwenye mjadala, watanzania wote wajadili masharti.
Binafsi nafahamu, mwekezaji kutoa matrilioni ya shilingi, bila kunufaika kwa namna yoyote, sidhani kama ni rahisi. Haiwezekani kabisa.MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.