Sijasema elimu ni kila kitu. Nimesema Utu ni muhimu kuliko hela.Elimu ingekuwa ndio kila kitu mbona hela kakuzidi Sana
Utu upi unazungumzia ambao ameshindwa kufanyaSijasema elimu ni kila kitu. Nimesema Utu ni muhimu kuliko hela.
Narudia tena, hela sio kila kitu. Usifanye hela kuwa malengo ya maisha yako, fanya hela kuwa kitendea kazi cha wewe kufikia malengo yako. Ukihusudu hela, dunia itakuhadaa na ni rahisi kupoteza utu wako.
Una wivu
Unapotumia alama ambayo inaakisi unyama waliofanyiwa (na kwa kiasi wanaendelea kufanyiwa) kundi fulani, halafu unapoambiwa kuwa alama hiyo inawaumiza ukakataa kuiondoa, ni kukosa utu.Utu upi unazungumzia ambao ameshindwa kufanya
Kasema akiingiza tamu akichomoa tamuHumo hajataja rungu la kipepe?
Hivi wewe unajua kuwa Kanyewest ni mentally disturbed. Hana akili sawa sawa. Anapesa na ana mafanikio lakini recently ameonyesha dalili za kutokuwa sawa kiakili.Vipi kuhusu hawa wa marekani weus nao Elimu ndogo au i?
View attachment 2128428
View attachment 2128429
View attachment 2128430
Ingekuwa Na Maana sana Kama Diamond Angekuwa Ni Mtu Mweupe Na Kavaa Hiyo Bendera Inge Sound, Ila Mtu Mweusi kuvaa Hiyo Bendera na Kulivanjuga hili Jambo ni Kukosa Akili.
Hakuna Mtu Mweusi Anaye Support Ubaguzi, Kwasababu Mtu Mweusi ndio Mtu wa Kwanza Kubaguliwa. So Hoja zote Za Kumtaka Diamond Kutoa hicho Kipande Ni Za Kijinga.
Halafu Ambao Hamjajua Kwanini Diamond Toka Anatoa Kamwambia Hadi Sahizi Kwenye Gidi, Bado Anaongelewa na Hajakauka Vinywani Mwa Watu Ni Pamoja na Mambo Kama Haya, Unafanya Kitu Kwa Makusudi Ili watu wakuongeleer hadi March 4 ukitoa EP yako Unakuwa Bado Uko kwenye Masikio Ya watu.
Waliosoma Marketing Wanajua Nini Naongea, Hivi Huwa Mnadhani Kuwa Wale Selena Hotel au Hyatt Regency Hotel huwa wanafanya Bahati mbaya Kusema Kuwa Valentine Usiku Mmoja ni Millioni 24? huwa Sio Bahati Mbaya huwa ni Akili Ya Marketing, Hasa Kwa Watanzania, Wanajua kuwa Kila Mtanzania Atapost, Ata Repost, atashangaa na Ipo Siku atataka kwenda Kutumia Hata Laki 1 sehemu ambayo Watu walilala usiku 1 kwa Millioni 24, hivyo kupelekea hizi Hotel, Kupata Airtime ya Bure kwenye Vyombo vya habari, kwenye mitandao ya Kijamii na Kuwafikia watu wengi zaidi just tuu kuna watu ni washamba Walishadadia bila kujua na Wakajikuta Wanatoa Promition Ya Bure ambayo hizo Hotel zingelipia Gharama kubwa sana Kupata Hiyo AirTime. Ni Akili Ya Marketing tuuuuu [emoji23][emoji23][emoji23] Kama Hujasoma Marketing Huwezi kugundua hili.
Mziki Wa Diamond Marekani Bado sanaa, Ila Trust Me Kwa Hicho Kipande Cha Video, Atapata Free promotion, Airtime na Kuongolewa. Si Ajabu kwa Sasa Wanao Ongoza Ku view hiyo Video ni Wamerekani. Sasa Ukiwa Huna Akili Utarukia Juu kwa Jui Bila Kujua hiki ni Nini? Hizo Ndio “Kiki” zenye akili na Zinazokufikisha Mbali.
Diamond Ni Mtu Mweusi Hana Cha Kupoteza Kwenye Maisha Ya Ubaguzi kwasababu Tumeshabaguliwa Sanaaa, Anacho Hitaji kwa sasa ni Kuendelea Kuongelewa Kwenye Vyombo vya Habari na Kwa Watu mbalimbali na Sehemu Tofauti Tofauti kama Tunavyo Fanya Hapa Ili Akitoa EP yake Tarehe 4 itukute Bado Tuna Mjadara na Yeye. Akili Mtu Wangu.
So Bravo Diamond, Jambo Limefanikiwa.
Tatizo ni kuiga bila kufanya utafiti wa hicho unachokiiga, jamaa wa Tandale kajifanya cowboy na wakati huo huo cowboy mweusi anayenyanyaswa kwa ubaguzi anasifia bendera ya wabaguzi, hivi domo kasoma hadi darasa la ngapi? na je anatumia washauri gani katika shughuli zakeakina mkubwa Fela na babu Tale
Mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz amekosolewa mitandaoni kwa kutumia bendera yenye utata katika video ya wimbo wake mpya wa Gidi.
Bendera hiyo ni ya kundi la Shirikisho la majimbo ya kusini ya Marekani ambayo yalipigania kudumisha utumwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe na bendera hiyo inaonekana kama ishara ya mivutano ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani. Moja ya kipande cha video atika wimbo wa Gidi kina bendera mbili zilizoonyeshwa wakati akicheza huku akiwa na muonkeano wa Cowboy.
Nini maoni yako juu ya video hii?
================================================================
Diamond Platinumz: Video ya wimbo mpya Gidi yakosolewa mitandaoni Marekani
Mwanamuziki wa Tanzania, Diamond Platnumz anakosolewa mtandaoni kwa kuangazia bendera ya Shirikisho kwenye video ya wimbo wake mpya.
Shirikisho lilikuwa ni kundi la majimbo ya Kusini ambayo yalipigana kudumisha utumwa wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani na bendera hizo zinaonekana kama ishara ya mivutano ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani.
Moja ya matukio ya video ya Diamond katika wimbo wa Gidi ina bendera mbili zilizoonyeshwa wakati akicheza huku akiwa na muonekano wa Cowboy.
Baadhi ya watumiaji wa Twitter wametoa hisia zao kuhusiana na video ya msanii huyo.
"Bendera ya Muungano katika video yako inasumbua," aliandika mtumiaji mmoja.
"Bendera ya Muungano?"Clyde Blaise aliandika na kujuumisha emoji ya pipa la taka.
Kufikia sasa Diamond hajatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo.
Hivi anatuonaje huyu?Kasema akiingiza tamu akichomoa tamu
Nafikiri huyu Mondi alitamani 'kufanania' na Lil Nas X, sasa akawa anaweka vitu bila ufahamu. Nimeona pia RODEO pale juu. Tahadhari tu asije kufanya video kama ya INDUSTRY BABY.Tatizo ni kuiga bila kufanya utafiti wa hicho unachokiiga, jamaa wa Tandale kajifanya cowboy na wakati huo huo cowboy mweusi anayenyanyaswa kwa ubaguzi anasifia bendera ya wabaguzi, hivi domo kasoma hadi darasa la ngapi? na je anatumia washauri gani katika shughuli zakeakina mkubwa Fela na babu Tale je wanaufahamu wa mambo ya dunia, tukisema mjifunze historia ya kidunia mnabaki kusoma na kuwatukuza wajinga, mna muda mwingi wa kuwazungumzia watu wajinga ,wanaokaa uchi,wanaongeza makalio ,wanaonyesha six pack badala ya kutafuta elimu na kujua historia , kila taifa lina utamaduni na historia yake,kwa hiyo kama mimi mtanzania nataka kufanya jambo lenye maudhui ya kijerumani basi yapasa nijifunze historia na utamaduni wa kijerumani, nikitaka kumuiga Mfalme Mswati basi yanipasa angalau niwe na ABC ya utamaduni na historia ya kwao akina Mswati. Domo na timu yake wameonyesha umbumbu walio nao, tukisema Domo ni mjinga watu wanatoa mapovu,yeye uwezo wake ni kuimba tu mambo ya kijinga ,mara msambwanda,jeje na ujinga kibao,amedhani kwa kuiga umarekani basi wimbo wake utakuwa maarufu duniani kwa kuwa unaonyesha taswira ya cowboy wa Kimarekani.
Jamaa hajuwi lolote anapelekwa tu
Ova
Hela sio kila kitu! Umuhimu ni utu na kuelewa madhara ya matendo yako kwa wengine. Hela huweza kuisha muda wowote.
Asipoomba msamaha na kushusha hiyo video asahau soko la wamarekani weusi Marekani, na hata nchi nyingine za nje zinazoelewa maana ya hiyo bendera na madhila yake.
Jombaa apo kuna luda na wengineHivi wewe unajua kuwa Kanyewest ni mentally disturbed. Hana akili sawa sawa. Anapesa na ana mafanikio lakini recently ameonyesha dalili za kutokuwa sawa kiakili.
Na hata mkewe Kim Kardashian ameona jamaa sio mzima ndio maana akamua kutengana nae maana sio mzima. Kiakili.
Unatakiwa kuwa mbovu wa akili kupeperusha bendera ambayo ina uhusiano na vikundi vya unyanyasaji, mateso, ubaguzi na mauwaji ya halaiki ya watu unaoshare nao race yaani watu weusi in this case.
Ume comment kishamba sanaJinsi huyo jamaa alivyo mshamba, sidhani hata kama alikuwa akijua ni nini maana yake...
Kwanza kitendo tu cha kuvaa kama cowboy kwa mtu anayetoka Tandale, ni ushamba mwingine...