Video ya "Gidi'' ya Diamond Platnumz yakosolewa vikali mtandaoni kwa kutumia bendera inayohusishwa na ubaguzi

Video ya "Gidi'' ya Diamond Platnumz yakosolewa vikali mtandaoni kwa kutumia bendera inayohusishwa na ubaguzi

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
1645531657493.png

Mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz amekosolewa mitandaoni kwa kutumia bendera yenye utata katika video ya wimbo wake mpya wa Gidi.

Bendera hiyo ni ya kundi la Shirikisho la majimbo ya kusini ya Marekani ambayo yalipigania kudumisha utumwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe na bendera hiyo inaonekana kama ishara ya mivutano ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani. Moja ya kipande cha video atika wimbo wa Gidi kina bendera mbili zilizoonyeshwa wakati akicheza huku akiwa na muonkeano wa Cowboy.

Nini maoni yako juu ya video hii?

Diamond.jpg


================================================================

Diamond Platinumz: Video ya wimbo mpya Gidi yakosolewa mitandaoni Marekani

Mwanamuziki wa Tanzania, Diamond Platnumz anakosolewa mtandaoni kwa kuangazia bendera ya Shirikisho kwenye video ya wimbo wake mpya.

Shirikisho lilikuwa ni kundi la majimbo ya Kusini ambayo yalipigana kudumisha utumwa wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani na bendera hizo zinaonekana kama ishara ya mivutano ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani.

Moja ya matukio ya video ya Diamond katika wimbo wa Gidi ina bendera mbili zilizoonyeshwa wakati akicheza huku akiwa na muonekano wa Cowboy.

Baadhi ya watumiaji wa Twitter wametoa hisia zao kuhusiana na video ya msanii huyo.

"Bendera ya Muungano katika video yako inasumbua," aliandika mtumiaji mmoja.

"Bendera ya Muungano?"Clyde Blaise aliandika na kujuumisha emoji ya pipa la taka.

Kufikia sasa Diamond hajatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo.
 
Kila kitu kinakosolewa yaani watu wagombane huku na mm niuzishwee jmn
 
Wakazi ndio katoa ushauri kuwa ikiwezekana hiyo scene yenye hizo bendera ifutwe au itafutwe namna ya kuonesha alichokifanya hakukijua.
 
Ningewaelewa kama wangekosoa kufanya shooting sehemu ambayo kuna hiyo bendera lakini kwamba eti kutumia... that's utter nonsense unless kama YouTube yangu inaonesha video kitofauti!

Nilichoona kwenye video ni sehemu ndogo sana ya hiyo bendera ku-flash for a second or two kiasi kwamba usipokuwa makini wala huwezi kuiona!

Kuna kila dalili ama Cimetographer au Editor alihakikisha bendera haionekani lakini waki-miss hicho kipande kidogo tena ambacho bendera yenyewe inaonekana sehemu ndogo kwa chini!!

Sioni popote kwenye video inakoonekana kama ilivyokuwa displayed kwenye hiyo picha hapo juu!
 
Back
Top Bottom