Video ya LIVE ya Rais Samia kwenye kilele cha mbio za Mwenge yaondolewa YouTube. Je, sababu ni kukohoa kwenye hotuba?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Leo nilitaka kurudia kutazama tukio la jana la kilele cha Mbio za Mwenge na Kumbukumbu ya Miaka 25 ya kifo cha Hayati Mwalimu Nyerere, Oktoba 14 pale Mwanza, nimejiuliza maswali mengi kuhusu hili, kwanini video hiyo imeondolewa YouTube au kwasababu Rais Samia wakati akihutubia alikohoa mara kadhaa kati kati ya hotuba?.

Awali, tukio lote lilirushwa live online na vyombo mbalimbali, ikiwemo Ikulu Tanzania, TBC na hata kwenye chaneli ya CCM lakini sasa limeondolewa kwenye majukwaa mengi na video iliyopo kwenye chaneli ya Ikulu Tanzania ina urefu wa dakika 33:02 pekee.

Kama shida ni Kikohozi, mbona ni jambo la kawaida tu kwa mtu kushikwa na Kikohozi au kuna kitu zaidi kilichofanya video hiyo iondolewe na kusababisha wananchi tukose taarifa?
Your browser is not able to display this video.
Soma, Pia:
+ Rais Samia akishiriki kilele cha Mbio za Mwenge na Kumbukizi ya Miaka 25 ya kifo cha Hayati Mwalimu Nyerere
 
Kuna kahoma fulani hivi kanapita kitaa kakiambatana na kikohozi kikavu wengine wanasema ni korona toleo la tatu
 
Sasa
Kama umegundua hilo,hapo ndipo shida ilipo!

Haijaondolewa kwa bahati mbaya!wanajua kwanini!

Kama Ile ya shehe yahaya Hussein ilivyooondolewa enzi hizo!!

Kabla ya uchaguzi Kuna sarakasi kibao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…