Video ya mfanyabiashara alienusurika kutekwa kwa mtazamo wa kiuchambuzi Inafikirisha sana

. Wewe mwenye akili kikubwa, nipe introduction ya sativa ilipoazia..

. Hao polisi ni akina nani, niletee majina yao hapa..

Wamesema wenyewe kwenye video wao ni polisi. Hiyo inatosha kujua wao ni akina nani sihitaji conspiracy theory wakati kila kitu kinajieleza. Mhalifu gani anakuja kukuteka na pingu?
 
Matukio yote yanahusisha wachaga na wanyakusa na yanatojea maeneo ya ngome ya CHADEMA
 
= wahalifu.
= kutekeleza


Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Wamesema wenyewe kwenye video wao ni polisi. Hiyo inatosha kujua wao ni akina nani sihitaji conspiracy theory wakati kila kitu kinajieleza. Mhalifu gani anakuja kukuteka na pingu?
. Wamesema wao ni polisi 🤔🤔???

. Vipi wangejitambulisha kama wao ni misukule, ungekubali kuwa kweli wao ni misukule????

. Pingu hata watu binafsi wanamiliki ✍️.


Swali langu bado lipo pale pale, huyo mtu alikuwa anajihushisha na nini??... Tukipata jibu hapa ndo tutajua shida imeazia wapi...
 

Hata wangesema wao ni miungu ningeamini. Kwanini uhangaike wakati kila kitu kipo in plain sight.

Mtu binafsi umiliki pingu kwa faida gani? Wapi huko mnakokaa ambako watu wanamiliki pingu for fun?

Hata angekua anauza chips, kwanini polisi wamteke au wakubali kutumika kumteka raia wa kawaida?

Dr. Ulimboka, Sativa na wengine wametekwa na polisi hao hao unaotumia nguvu kuwatetea wakati wenyewe wamejitambulisha kuwa ni polisi.
 
Umechambua lakini hoja zako za kiuchambuzi ni nyepesi sana na zinaonesha na zinaonesha uchanga wana kifikra

Alitekwa MO na watekaji hawakupatikana hadi leo,je? Mo ni mwana harakati? Kuna wale wafanya biashara wa madini morogoro ambao polisi walishiri na kesi ikahukumiwa je? Yule likuwa ni mwana harakati?

Ukitizama tukio lile kuna watu wamesimama nyuma kule na wamesimama kwa utulivu kabisa jee? Unadhani wasinge weza kurekodi kwa utulivu?

Hivyo rudi kafanye tena uchambuzi wako hoja zako laini sana
 
Hiv

Hivi CCTV camera huwa inatoa sauti?
Can CCTV Cameras Pick Up and Record Sound? In short, yes, they can. CCTV cameras can record audio, although this works differently depending on whether you have IP CCTV cameras or more traditional analogue cameras. Analogue cameras need to have audio input directly through the DVR (digital video recorder).
 
. Hao akina DR. Ulimboka na Sativa, ipo wazi kuwa source ilikuwa ni nini..✍️ ✍️ ✍️

. Hata ukija yule jamaa aliyeuawa na polisi ( kijana wa madini mtwara pia inajulikana source ilikuwa ni nini..✍️ ✍️)


Hata angekua anauza chips, kwanini polisi wamteke au wakubali kutumika kumteka raia wa kawaida?
Wenye busara kama mimi na mtoa maada tumefikiria hili toka mwanzo, "kuwa kwa nini atekwe shida ni nini hasa!!!

. Je anasiri za Kambi ya serikali??

. Je ni mwanaharakati wa Chama fulani ??

. Je kuna mali za magendo wamezungukana??
 

Unajiita una busara ila mimi nakuona mweupe kama ream paper.

Tatizo sio kosa/shida iliyopelekea kutekwa. Tatizo ni njia iliyotumika kumkamata. Kwa "busara" zako wanasiasa pinzani na wanaharakati ni sahihi kutekwa? Kwanini njia sahihi zisitumike kukamata kama mtu anakosa fulani?
 
Sahihi kabisa.
 
1. Pingu
2. Sisi ni polisi
3. Tutakuuua
4. Tutakufata tena

Fanyeni ujinga tu, mtakuja kusababisha MAUJI KWA WATU WASIO NA HATIA. HAO MNAOWATUMA WANAFAMILIA PIA KUMBUKENI. FAMILIA ZAO ZIPO HUKU HUKU MTAANI.

SAWA, TUSUBIRI.
 
1. Pingu
2. Sisi ni polisi
3. Tutakuuua
4. Tutakufata tena

Fanyeni ujinga tu, mtakuja kusababisha MAUJI KWA WATU WASIO NA HATIA. HAO MNAOWATUMA WANAFAMILIA PIA KUMBUKENI. FAMILIA ZAO ZIPO HUKU HUKU MTAANI.

SAWA, TUSUBIRI.
Hakika.
 
. Ngoja nikuache..... Maana naona nabishana na picha ya ukutani 🖼️🖼️.

. Mimi sihitaji namna wanavyokamata, mimi nataka nijue chanzo ni nini hasa mpaka wafike hiyo hatua ya kushikana mashart.. ✍️.

. Tukisha jua source ni nini, Ndo tutahoji kwa nini alikamatwa kwa style ile!!!.

Sasa tatizo lako wewe unakuja kwa kukurupuka, then unafananisha Dr. Ulimboka, sativa na huyu jamaa..
 
Tuachie polisi kwanza tuone taarifa yao itakuaje, maana inasemekana kwa wanaowajua hao "watekaji" wawili wametambuliwa kama ni polisi...
incredible terminator ana hoja ya msingi ila 1. Ameweka doubts ambazo hazina mantiki 2. Uandishi wake ni majanga kwenye L na R
Mimi nilichoelewa ni kuwa mwanzisha thread anasema tuwe macho isijekuwa hili ni igizo limefanywa na na vyombo vya usalama ili kuwaaminisha watu kuwa utekaji unaofanywa vyombo vya dola havihusiki. Yaani ni kuwa script imeshaandalia kuwa baadae polisi watasema wameshafanya uchunguzi na kuwakamata wahusika na imegundulika kuwa siyo polisi na watawekwa mbele ya waandishi wa habari na kukiri kuwa wao wanajihusisha na kuteka watu. Hapo polisi itasema siyo kila utekaji na wa vyombo vya dola. Anyways, hata mimi siamini iko hivyo ila ni vizuri kuangalia hili tukio kwa angle zote.
 
Kila tukio la utekaji linapotokea lazima waje chawa kama mtoa mada na vimaswali vya kijinga. Mzee Ally Kibao alivyotekwa mliongea hivi hivi, ila alipouawa mkabadilisha maneno. Ni unafiki kujadili matokeo baadala ya sababu.
 

Ni mfanya biashara
 
Duh!mkuu umejithd kuifafanua kulingan na uelew wko,mim sikupingi mkuu Kun fact meipat angalau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…