SI KWELI Video ya ndege ya Brazili muda mchache kabla ya kupata ajali

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Salaam Wakuu,

Nimekutana na hii video ikidai ni tukio la kweli kuhusu ajali ya ndege nchini Brazil. Kuna ukweli?



Your browser is not able to display this video.
 
Tunachokijua
Mnamo August 09, 2024 ilitokea ajali ya ndege ya abiria nchini Brazil. Taarifa zilieleza kuwa watu 61 waliokuwapo kwenye ndege hiyo wote walifariki (soma hapa).

Baada ya tukio hilo, siku ya tarehe Agosti 15 Kupitia mtandao wa TikTok kumeibuka video (hii) ambayo imewekwa na Haongbado10040 ikiwa na ujumbe "Muda mfupi kabla ya Ndege ya Brazil kuanguka".

Kuna ukweli kwenye video hiyo?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck.com umebaini kuwa video hii haina ukweli na haihusiani na tukio la ajali ya Brazili kama ujumbe huo unavyodai. Rangi na muonekano wa ndege iliyo kwenye video hiyo haiendani na ndege iliyopata ajali nchini Brazil Tazama (hapa)


Ndege ya Voepass kabla ya ajali


Mabaki ya Ndege ya Voepass baada ya ajali


Ndege iliyopo kwenye video inayohusishwa na ndege ya Brazil

Zaidi ya hayo, JamiiCheck imebaini kuwa, Video hii imechukuliwa kutoka katika mission ya game ya Great Theft Auto (GTA5).

Hoja nyingine zinazothibitisha kuwa video hii haijatokea katika mazingira halisi ni pamoja na

1. Namna video ilivyochukuliwa katika angle mbalimbali haina uhalisia

2. Sauti inayosikika ya watu haipotei japo ndege inaonekana kwenda mazingira mbalimbali

3. Namna ndege ilivyotua baharini haioneshi mtikitisiko wowote kwenye ardhi na kwenye maji.

4. Wadau wa JamiiCheck wa mitandaoni nao walitoa hoja zao kuonesha kuwa tukio hili halikuwa halisi Soma (hapa).

Je, wewe umeona nini kingine?
Sure nadhani ndio walichokifanya kutengeneza hio video
Yaaah ndo hivo....wanafanya simulation ..
Hayo mambo yapo sana kwenye Channel inaitwa national geograph sijui kuna kipindi kinaitwa plane crush investigation unakutana na miamba au wanyangende wanajiita BEA hao wanachunguza ajari as if walikuepo after that...

Wanatoa short video kuhusu hiyo ajari.. mkuu ukifatilia hiko kipindi kuna vingi sana utajua kuhusu hizi ajari za ndege na mengine mengi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…