- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Wadau wa JamiiCheck wameshiriki kuthibitisha uhalisia wa video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii na kueleza kuwa ni pikipiki lenye uwezo wa kugeuka kuwa ndege ya kivita, abapo wadau wengi walieleza kuwa video hiyo si halisi kutokana na dosari walizozibainisha. Baadhi ya wadau wameandika;
JKizija - Mdau wa JamiiCheck Instagram
Mwanchimba Junior - Mdau wa JamiiCheck FacebookVipande vya cover za pikipiki ambavyo vimeanguka na kujitenga peke yake, ghafla vikavutwa na kufanya engine ya ndege. Pia tairi la mbele limepotea kimazingaombwe
1: Ndege ilivyoondoka kwa aina ya ndege hii ya kivita ni lazima itembee kama mita 50 mpka 100
Kuntah061 - Mdau wa JamiiCheck Instagram2: Mabadiliko ya mwendeshaji wa pikipiki upande aliokuwepo na sehemu aliyowekwa kama ruban inaondoa uhalisia
1. Dereva ambaye ni binadamu kiuhalisia anayeyuka na kuwa vipande vinavyounda ndege, kitu ambacho hakiwezekani.2. Gari lililokuwa nyuma ya pikipiki limepotea ghafla.3. Ukitazama kwa umakini utagundua kwamba gari lililokuwa likifata pikipiki linaenda uelekeo mmoja na magari ya upande wa pili kitu ambacho hakionyeshi utii wa sheria za barabarani
Uhalisia wa video hiyo kwa mujibu wa JamiiCheck
JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa video hiyo si halisi na imetengenezwa kwa Teknolojia ya Akili Unde, licha ya dosari zinazoonekana pia Nyenzo za kidigitali zinathibitisha hilo.