BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Katika tukio lisilo la kawaida, Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir mwenye miaka 71 ameonekana akitokwa na haja ndogo wakati wa hafla ya Kitaifa na wimbo wa Taifa ukipigwa. Kitendo hicho kinaibua maswali kuhusu hali za kiafya za viongozi wengi duniani kuendelea kukaa madarakani hata baada ya umri wao kuwa mkubwa na wengine wakiwa na afya zisizoridhisha.
Mwaka huu 2022, pia mgombea wa Urais nchini Nigeria Bola Ahmed Adekunle Tinubu mwenye miaka 70 alionekana akiwa na mfuko maalumu wa kuhifadhia mkojo wakati wa mchakato wa kuanza kampeni hali iliyopelekea wananchi kuhoji kuhusu afya yake na majukumu anayotaka kugombea.