- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nimeona video ikisambaa toka jana ikimuonesha Tundu Lissu akiwa anazomewa na watu waliokuwepo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana tarehe 11/09/2024 wakimzomea na kumuita YUDA je ni cha kweli?
- Tunachokijua
- Tundu Lissu ni Mwanasheria ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA lakini pia aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Singida Mashariki mwaka 2010 hadi mwaka 2020
Siku ya tarehe 11 Septemba 2024 Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliitisha mkutano na waandishi wa habari katika Ofisi zao Mikocheni jijini Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa kuzungumzia masuala mbalimbali yanayoendelea nchini kwa hivi sasa ikiwemo utekaji na kifo kilichotokea hivi karibuni cha kada wa CHADEMA Ally Kibao aliyetekwa na kuuliwa wakati akisafiri kuelekea mkoani Tanga.
Mara baada ya mkutano huo ambapo baadhi ya viongozi walizungumza akiwemo Tundu Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA bara, kumekuwa na kipande cha video kinachosambaa katika mitandao ya kijamii kikimuonesha Makamu Mwenyekiti huyo akizomewa, tazama hapa, hapa na hapa wakati akizungumza kwenye mkutano huo na waandishi wa habari huku baadhi ya maneno yakisikika kumtaja Lissu kama “YUDA”
Jamiicheck imefanya uhakiki wa video hiyo na kubaini video hiyo haina ukweli kwa kulinganisha na video halisi ya mkutano uliofanyika Septemba 11, 2024 Ofisi za CHADEMA, Makao Makuu ya Mikocheni, Dar Es Salaam ambao ulikuwa ukirushwa moja kwa moja kupitia kwenye baadhi ya Youtube channels.
Tumebaini kuwa kipande cha video kinachosambaa mitandaoni kikimuonesha Lissu akizomewa kimehaririwa kwa kuongezewa baadhi ya sauti zinazosikika zikisema Toka wee toka wee, Yuda huyooo eeee, tunamtaka mwenyekiti ambazo hazipo kwenye video halisi kama ambayo inayosambazwa mitandaoni ikiwa imeongezwa sauti, Tazama video halisi hapa na hapa.
Ili kuthibitisha kuwa kipande kinachodai kuwa Lissu alizomewa:
- Tumebaini kipande hicho kina kasi kubwa ya sauti tofati na kasi ya maneno ya video nzima ambayo ni halisi
- Sauti za wanaosikika kuzomewa zina sauti ya juu kama walikuwa wakiongea karibu kabisa na maiki au alipo Lissu hali ya kuwa sauti za watu waliopo kwenye video halisi zinasikika kwa chini kuonesha walipo hakukuwa na maiki ya kunasa sauti zao kwa ukaribu hali ambayo ipo kwenye video halisi kama zilivyorushwa kwenye Youtube channels hivyo kututhibitishia kuwa video hiyo imehaririwa.