Video za uokozi maafa ya kariakoo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila, amekanusha taarifa zilizoripotiwa na baadhi ya Vyombo vya Habari na kusambazwa mitandaoni kwamba zoezi la uokoaji wa Watu walio chini ya ghorofa lililoporomoka Kariakoo limesitishwa ambapo amesema uokoaji haujasitishwa na Watu wanaendelea na zoezi hilo usiku huu.

Akiongea na @AyoTV_, RC Chalamila amesema β€œKwa taarifa zinazoendelea hivi sasa imeonesha maokozi yamesitishwa, ukweli ni kwamba maokozi hayajasitishwa hapa tulipo nipo Mimi RC, kuna Wizara mbalimbali, DC , RAS na Vyombo mbalimbali vya Ulinzi na Usalama, zipo Timu mbalimbali za Vyombo vya Dola na Watu binafsi wanaoendelea kutusaidia”
#MillardAyoUPDATES
 
Kaa kimya msije mkapigwa kofi na Mungu maana Mungu hapokei tu report na kutoa maagizo ni yy anaona na kutenda!!
kwa Neema na Baraka za Mungu maelekezo ya Rais Dr.Samia Suluhu Hassan ambae anaongoza serikali ya wanadamu kutoka kwa Mungu, yaendelee kutekelezwa na kuzaa matunda kadiri ya mapenzi ya Mungu mwenyewe.

hakuna haja kubabaika gentleman
 
kwa Neema na Baraka za Mungu maelekezo ya Rais Dr.Samia Suluhu Hassan ambae anaongoza serikali ya wanadamu kutoka kwa Mungu, yaendelee kutekelezwa na kuzaa matunda kadiri ya mapenzi ya Mungu mwenyewe.

hakuna haja kubabaika gentleman
ambae anaongoza serikali ya wanadamu kutoka kwa Mungu,😭😭😭
 
Huu uchawa wenu kila pahala uwe unaishia mtandaoni, mtaani utapigwa mande.
 
Vifaa vya kuokolea siyo greda na oxygen tu!
Nchi za wenzetu wanatumia hydraulic pumps (kama jeki la gari) na vyuma kama hivi kunyanyua kuta, kuhakikisha kuta haziporomoki
Moja hiyo ya mwisho inaitwa Jaws of Life
Sasa sijui kuna vifaa kama hivi na mafunzo wamepitia vikosi vyetu?
Ndugu zetu watolewe Kariakoo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…