Kuna mambo mengine hata ukisema unapinga hayapunguzi waka kuongeza kitu kwa maana mambo yenyewe yanafanyika gizani, huwezi hata kuthibitisha.
Mabinti wengine wanadai ni marafiki sana, kila mara wapo wote, wanalala chumba kimoja, hujui kama ni urafiki tu au ndio wanafanyiana huo uchafu, na huna uwezo wa kuthibitisha.
Tukazane kuwalea watoto wetu katika maadili tunayoyaamini japo hatuna uhakika wa 100% kuwa hawawezi kuja kuyageuka maadili yetu.
Lakini kwa upande mwingine, si aheri shoga kuliko wanaoteka watu, wanawaua, wanapora mali za watu, halafu bado tunawashangilia kwa sababu wamepanda punda au lorry. Shoga anafanya huo uchafu kwenye mwili wake, lakini haya majitu tunayoyashangilia yalikuwa yanaumiza na kupoteza nafsi za watu wasio na hatia.
Bila shaka itakuwa rahisi kwa shoga kuionja ahera kuliko watekaji, wauaji na wadhulumu mali za watu kwa kutumia madaraka yao. Yamelaanika majitu hayo na vizazi vyao.
Hata haya mafisadi ya kwenye report ya CAG, yanaumiza jamii kubwa ya watu kuliko mashoga. Kila.mmoja akiulizwa ameumizwa na nini na kwa kiasi gani na mashoga, ni wachache sana watakaopatikama, na zaidi watakuwa wanafamilia wa hao mashoga, na zaidi watakuwa wameuamia kisaikolojia kuliko ule uhalisia wa moja kwa moja.