Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watanzania wanachama wa vyama vingi yani Yuko ccm na pia Yuko CHADEMA fahamu tu iloNikuondoe hofu ndugu yangu, CCM ina wanachama milioni 17 Tanzania nzima ambao wote wanavyeti vya kupiga kura na wamejiandikisha kupiga kura mwaka huu.
Jumla ya wapiga kura wote waliojiandikisha nchini ni milioni 29. Na ili mgombea urais aweze kupita anahitaji asilimia 51 ya kura zilizopigwa. Wataalam wanaita majority rule.
Sasa ukiangalia mahesabu yalivyo, kutokana na idadi ya wanachama wa CCM peke yake, watakao mpigia kura Rais Magufuli, imezidi nusu ya idadi ya wapiga kura wote waliojiandikisha.
Mimi sielewi kwa idadi hii ya wanachama wa kadi na sio wafuasi wa CCM, Tundu Lissu, Malim Seif na nyie wafuasi na mashabiki wa vyama vya upinzani mnapata wapi ubavu wa kusema kuwa mnauwezo wa kuishinda CCM mwaka huu na kumwangusha Magufuli? Hamwoni kuwa mnajipa stress za bure?
Kama Lissu amewatumia hao wafadhili wake kummpa pesa ya kuwahonga baadhi ya wanachama wa CCM ili wampigie kura yeye badala ya Magufuli, hapo naweza sema sawa. Vinginevyo ningemshauri siku ya uchaguzi atafute haraka sana njia ya kukitoa kurudi huko aliko toka, maana matokeo yakitangazwa na ikaonekana kwamba ameshindwa uchaguzi, ajue hii nchi itakuwa chungu sana kwake na kwa familia yake.
Matusi yote aliyo yaporomosha kwa Mweshimiwa Rais Magufuli na vyombo vya usalama, sidhani kama atabaki salama nchi hii. Akitaka kujua mengi, kwanini nasema
hivi, ninge mwomba amwuulize Manji kilicho mtokea, baada ya kuwaambia waandishi wa habari kuwa yeye anaongea na mwenye mbwa na sio mwangalizi wa mbwa.
Lissu asiwadanganye watanzania na The Hague yake. The Hague atapelekwa yeye na wachochezi wa amani na usalama wa nchi kama vurugu itatokea na sio Rais Magufuli wala mastafu wa vyombo vya Dola. Aache usanii wake wa kuwaadaa nyie makachero wake.
Lissu kwanza sio mwanasheria mjuaji ana shahad za mambo yanayo husu sheria na hajui sheria hata moja. Ni mlopokajia tu. Yeye ninavyo mwona mimi ni msomaji tu wa vitabu vya kihistoria na kupanga maneno yanayo husu historia, lakini sio mjua sheria. Ana fantasy tu kichwani.
Kauli zake za kuwaambia watu wasitoke kwenye vituo vya uchaguzi na kwamba matokeo yakitangazwa kinyume cha mategemeo yao waende barabarani, hiyo tayari ni tendo la uchochezi na ni uvunjifu wa amani kama hajui na jambo ambalo yeye linaweza likampeleka In The Hague na kushtakiwa endapo machufuko na umwagaji wa damu utatokea.
Yeye anavyo wahimiza wafuasi wake waende barabarani na sisi tunao mpenda Magufuli je, tutakuwa wapi? Anafikiri sisi tutakaa tu nyumbani na kuwaangalia wao wanavyo andamana barabarani kwenye TV na Social Media? Inatakiwa asahau kitu kama hicho. Sisi nasi tuta ji-mobilize tukutane nao barabarani. Mengine yatajulikana huko.
Yeye kama mgombea wa Urais alitakiwa amwage sera za kujenga Taifa na sio kauli za kuleta vurugu. Hii yote anajua kuwa ushindi hata upata kwa hiyo amekuja kuleta chaos kwetu kama alivyo tumwa na matechnician wake wa nje wa kuleta vujo.
Bernad Kamilius Membe mimi namwona ni mtu makini sana, japo kuwa watu wana mdharau na kumwona yeye chizi tu. Alisema kwenye kikao chake juzi na wahandishi wa habari kuwa ushindi wake unategemea mpasuko wa CCM na sio vingine. Yeye anajua fika bila mfarakano wa CCM, hawezi ambulia kitu. Ni kujidanganya mwenyewe.
Na ndiyo maana lengo lake kubwa, kwa wale wanao msikiliza vizuri, ni kukisambaratisha chama cha CCM au kama mwenyewe anavyo sema kuleta mpasuko ndani ya CCM. Lakini
kwa hivi sasa jinsi hali inavyo onekana, bila mpasuko wa CCM hakuna mgombea hata mmoja yukonkwenye position ya kukishinda chama cha mapinduzi, hata angekusanya watu kiasingani kwenye kampeni yake ya uchaguzi, anaweza sema eti atashinda uchaguzi wa 2020 zidi ya CCM. Huo ni uongo wa hali ya juu. Watu watakao kuwa wanawaza hivi nafikiri wanaota njozi za mchana.
Ndio maana akawasisitiza kufyatua sana watoto ili wakusanye hizo 70k kwa wingi....
Wakati wake zetu wakienda kujifungua wanalipishwa elfu 70,000
Bashiru amekuwa mkali mpaka anamtisha mdada wa watu, Bashiru ukiulizwa swali jibu, sio unaulizwa na wewe unajibu kwa kuuliza, tena kwa sauti ya ukali, tulieni hii ndio Tanzania ya watanzania, na Lissu ndio chaguo letu.