Nyafwili
JF-Expert Member
- Nov 27, 2023
- 6,168
- 15,748
Kwa nchi zinazoendelea Vidonda vya tumbo ni mojawapo ya matatizo ya kiafya yanayoathiri watu wengi. Hii inatokea pale ambapo ukuta wa ndani wa tumbo au sehemu ya juu ya utumbo mdogo unapopata jeraha. Watu wengi wamekuwa wakihusisha vidonda vya tumbo na kutokula chakula kwa wakati, kuwa na mawazo, lakini tafiti zipo wazi kuwa sababu kuu za maambukizi ya vidonda vya tumbo ni bakteria aina ya Helicobacter pylori(H. pylori) pamoja na matumizi yasiyo sahihi ya baadhi ya dawa za NSAIDS kwa muda mrefu. Ni muhimu kuelewa chanzo, dalili, kinga na matibabu ya ugonjwa huu lakini tukiendelea kudanganyana baina ya jamiii kwa jamii, hivyo hivyo ugonjwa huu ndivyo unazidi kushamiri na Kuumiza watu wengi.
KIVIPI HELICOBACTER HUAMBUKIZA.
Hizi ndo sababu kuu kabisa zinazo sababisha kuugua ugonjwa huu wa vidonda vya tumbo.
SABABU NYINGINE ZINAZOWEZA KUSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO.
DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
UONGO ULIOPO KWENYE UGONJWA HUU.
Hasa wahudumu wa afya na Madaktari wa mchongo wamekuwa mustari wa mbele kabisa kupotosha jamii ya kuwa ;-
DAWA ZA KUPUNGUZA MAUMIVU YA VIDONDA VYA TUMBO
Dawa zilizotaja hapo juu hutolewa kwa mchanganyiko ili kudhibiti maambukizi kwa usahihi, unaweza kuchanganya na dawa hizi isipokuwa Heligo Kit;-
✔ Kama kuna H. pylori = antibiotics + PPI
Lakini kulingana na taarifa za watumiaji au wagonjwa wenye shida ya vidonda vya tumbo wamekuwa wakilalamika kuwa utumiaji wa dawa hizi umekuwa na msaada mdogo sana kwao, hali ambayo imesababisha ugonjwa kuendelea kukomaa kila kukikcha.
Lakini Mr Nyafwili, nikaamua kwenda mbali zaidi na kugundua kuwa Kiazi mviringo na Mafuta ya Mamba ni tiba sahihi kabisa ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo.
1. Kiazi Mviringo
Chukua kiazi kimoja osha chukua blender kisa saga na maganda yake, baada ya hapo chukua waji kidogo kisha changanya, kiazi kimoja asubuhi(kabla hujala chochote au kula chochote), kiazi kimoja jioni(kabla hujala chakula) tumia kwa siku saba hadi siku 14
2. Mafuta ya mamba
MATUMIZI
Kijiko kimoja asubuhi, kijiko kimoja jioni ndani ya siku 14
Endapo umegundulika na Na vidonda vya tumbo epuka utumiaji wa vyakula hivi mpaka pale utakapokuwa sawa;-
MAADA INAYOFUATA : Je GERD na vitonda vya tumbo chanzo chake ni bakteria aina ya H. Pylori??
KIVIPI HELICOBACTER HUAMBUKIZA.
Hizi ndo sababu kuu kabisa zinazo sababisha kuugua ugonjwa huu wa vidonda vya tumbo.
- Kwa njia ya kupeana denda baina ya mwenza na mwenza.
- Kushirikiana vyombo vya chakula na mtu mwenye Maambukizi ya vidonda vya tumbo
- Kunywa maji machafu hasa maji ya visimani ambapo bakteria hawa wanaweza kuishi
SABABU NYINGINE ZINAZOWEZA KUSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO.
- Matumizi ya muda mrefu ya dawa za maumivu, mfano ;-diclofenac, ibuprofen na dawa nyingine za kundi la NSAIDs
- Uvutaji sigara
- Matumizi ya pombe kupita kiasi
DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
- Maumivu au kuwaka moto sehemu ya juu ya tumbo
- Kichefuchefu na kutapika
- Kujisikia kushiba haraka unapokula
- Tumbo kujaa gesi na kubanwa
- Kukosa hamu ya kula
- Kupungua uzito bila sababu ya wazi
- kutapika damu au kupata choo cheusi kama lami
UONGO ULIOPO KWENYE UGONJWA HUU.
Hasa wahudumu wa afya na Madaktari wa mchongo wamekuwa mustari wa mbele kabisa kupotosha jamii ya kuwa ;-
- Vidonda vya tumbo vinasababishwa na Msongo wa mawazo, huu ni uongo
- Vidonda vya tumbo vinasababishwa kwa sababu ya kutokula kwa wakati, huu ni uongo.
DAWA ZA KUPUNGUZA MAUMIVU YA VIDONDA VYA TUMBO
- Misoprostol +Mife, hii dawa ni mahususi kwa ajili ya vidonda vya tumbo hasa kwa vidonda vinavyo sababishwa na NSAIDs, lakini kutokana na walimwengu walivyokuwa na speed ya ujuaji basi wakaamua kubadilishia matumizi na mpaka sasa imekuwa dawa haramu(kwa sasa inatumika kwenye utoaji mimba) .
- Omeprazole, ina allergy kwa baadhi ya watu
- Pantoprazole, ina allergy kwa baadhi ya watu
- Esomeprazole, ina allergy kwa baadhi ya watu.
- Heligo kit, ina mchanganyiko wa Clarithromycin, Tinidazole na Lansoprazole, hivyo usichanganye na dawa zingine za antibiotics .
Dawa zilizotaja hapo juu hutolewa kwa mchanganyiko ili kudhibiti maambukizi kwa usahihi, unaweza kuchanganya na dawa hizi isipokuwa Heligo Kit;-
- Amoxicillin caps
- Clarithromycin tabs
- Metronidazole tabs
- Cephalexin caps
- Azithromycin Tabs/caps
✔ Kama kuna H. pylori = antibiotics + PPI
Lakini kulingana na taarifa za watumiaji au wagonjwa wenye shida ya vidonda vya tumbo wamekuwa wakilalamika kuwa utumiaji wa dawa hizi umekuwa na msaada mdogo sana kwao, hali ambayo imesababisha ugonjwa kuendelea kukomaa kila kukikcha.
Lakini Mr Nyafwili, nikaamua kwenda mbali zaidi na kugundua kuwa Kiazi mviringo na Mafuta ya Mamba ni tiba sahihi kabisa ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo.
1. Kiazi Mviringo
- Kazi kuu ya kiazi ni kufyonza tindikali , lakini ina neutralize HCl iliyopo tumboni kwa kiasi kubwa.
- Kazi kuu ya kiazi mviringo, inazuia H. Pylori kuvunja kimiminika cha urea kwenda urease kilichopo tumboni na kukigeuza kuwa ammonia na carbon dioxide.
- Mbali na urease, bakteria hawa pia huzalisha vimeng'enya vingine kama vile Catalase (kujilinda dhidi ya seli nyeupe za damu), Phospholipases, na Proteases (vinavyosaidia kuvunja ute wa tumbo na kuharibu seli za ukuta wa tumbo.
Chukua kiazi kimoja osha chukua blender kisa saga na maganda yake, baada ya hapo chukua waji kidogo kisha changanya, kiazi kimoja asubuhi(kabla hujala chochote au kula chochote), kiazi kimoja jioni(kabla hujala chakula) tumia kwa siku saba hadi siku 14
2. Mafuta ya mamba
Mafuta ya mamba ni asili ya lipidi, na asidi za mafuta kazi kuu ni kufyonzwa. Ingredients na virutubisho vyake vikuu ni Fatty Acids, unsaturated fatty acids, kama vile
• Omega-3 na Omega-6 inasidia kupunguza uvimbe na kulainisha ngozi.
• Omega-9 (Oleic Acid, inaupa ugumu bakteria aina ya H. Pylori kuendelea kuzaliana na inasaidia katika ukarabati wa ngozi na uponyaji wa vidonda
MATUMIZI
Kijiko kimoja asubuhi, kijiko kimoja jioni ndani ya siku 14
Endapo umegundulika na Na vidonda vya tumbo epuka utumiaji wa vyakula hivi mpaka pale utakapokuwa sawa;-
- Maharagwe
- Pili pili
- Pilau
- Kachumbari
- Matumizi ya nyanya
- Chips
- Ugali wa Dona
MAADA INAYOFUATA : Je GERD na vitonda vya tumbo chanzo chake ni bakteria aina ya H. Pylori??