Vidonge vya kuzuia Uzazi kwa Wanaume mbioni kuingia Sokoni

Vidonge vya kuzuia Uzazi kwa Wanaume mbioni kuingia Sokoni

AskariKanzu

Member
Joined
Jul 25, 2025
Posts
38
Reaction score
146
Mamlaka ya chakula na dawa nchini marekani ilipitisha njia mbalimbali zaidi ya 20 za uzazi wa mpango. Njia mbili tu zimethibitishwa kwa wanaume kuweza kuzuia mimba kwa wapenzi wao nazo ni kondomu na kufunga kizazi(vasectomies).

Asilimia 25% ya wanawake wanatumia njia ya kutumia vidonge kupanga uzazi,lakini kwa wanaume hakuna njia za vidonge.

Takwimu kutoka katika chuo cha afya cha Minnesota kipo katika majaribio ya vidonge vya homoni vya kuzuia uzalishaji wa mbegu za kiume kwa muda fulani.

Dawa hizo mpya zinaitwa YCT-529 hormone free lengo ni kuzuia uzalishaji wa manii kwa mwanaume.

Takwimu zinasema

  • Kwa panya dume, dawa zimesababisha ugumba kwa 99% na kuzuia mimba ndani ya wiki nne baada ya matumizi.
  • Kwa viumbe vya kiume visivyo binadamu Kama nyani nk, dawa imeweza kupunguza uzalishwaji wa mbegu ndani ya wiki mbili baada ya matumizi.
  • Kwa panya na viumbe kama nyani wameweza kurutubisha mara baada ya kuacha kutumia dawa hizo. Panya wemerudia uwezo wao wa kurutubisha ndani ya wiki sita, lakini viumbe kama nyani wamerudisha uwezo wa kurutubisha ndani ya wiki 10-15.
  • Hakuna madhara hasi ya matumizi ya dawa hizo kwa viumbe hao.

Njia nzuri na yenye tija kwa uzazi wa mpango kwa wanaume ameeleza-Gunda

Chanzo pharmacy. Umn. edu.

_20250728_132921.JPG
 
Mwanaume atazuaje uzazi wakata kuna wanawake wengi wanahitaji huduma ya kupewa mimba? Hizo watakunywa wehu, kamwe mwanaume rijali hatakunywa kwani kuna sehemu anahitajika akawape mimba wanawake wenye uhitaji wa watoto
 
Kama sitaki kumpa mimba mwanamke bora nitumie kondomu ili nisiharibu mbengu zangu kwani zinahitajika sana kwa mwanamke mwingine kupata mtoto
 
Mungu atupe nini, chanjo ya HIV ishapatikana na huku wanatuletea vidonge vya majira.

Ni mwendo wa kumimiana uji tu sasa hivi bila ya hofu ya ngoma wala kibendi.

Sasa nishajimezea zangu midonge ya majira halafu lije toto la mtu linibambikie mimba, nitalipa mashuti ya kufa mtu.
 
Back
Top Bottom