Vidume tuliopitia kwa ngariba bila ganzi tukutane hapa kukumbushana yale maumivu!

Vidume tuliopitia kwa ngariba bila ganzi tukutane hapa kukumbushana yale maumivu!

Duh! Nyie ndio mnakujaga kutoa hata Siri za jeshini...... Hamfai Kabisa...... She***zy
 
Dah kidume unakatwa halafu unalia? Huko kwetu kitendo cha kutingisha mguu tu wakati unakatwa ni udhaifu mkubwa

Kutoa siri za jandoni ni mwiko
 
Mmh aisee
images(42).jpg
 
Ha ha kuna jamaa alimwaga mbonge la kimba aisee, kwa sasa ni bosi maeneo flani, tukikutana mara chache wik end tukikumbushana mambo ya zamani, nikimchomekea hiyo kitu kukauka mbavu kwa kicheko,lakini kwa sasa na hili tishio la ukimwi, vile vitendea kazi si salama tena...kwa kweli sishauri..Hospitary ni best option.
Duh,, mambo ya aibu jamani.
 
Sisi kwetu hatuna utamaduni wa kutahiri asee. Mi nimejipeleka hospitali mwenyewe nikiwa na miaka 29, nimeoa tayari.
Nashangaa hizi project za tohara bure zimeng'ang'aniwa mikoa ya Iringa, njombe na mbeya wakati na wahaya hasa wakristo hawatahiri.
Jamaa yangu mhaya alikuwa JKT akasikia ukaguzi wa kwenda JWTZ lazima uwe umekatwa akaenda kukatwa.
Wahaya tubadilike
 
Ni miaka mingi imepita tangu niondolewe hili pulizo. Najiskia fahari sana kufanyiwa hii huduma bila ganzi. Niliumia ila leo najivunia.
Ilikuwa asubuhi yenye baridi kali. Kama saa kumi na mbili kasoro. Nikashtuka mlango wa nyumba niliyokuwa nimelala na wenzangu unafunguliwa. Mjomba wangu na vidume viwili vilivyoshiba vikaingia. Nilikuwa na taarifa kuwa leo govinda linarestishwa in pisi, ila sikutegemea ingekuwa kwa mtindo huu.
Nikaamrishwa kupanda mgongoni kwa njemba mojawapo, nikatii. Nlivyokwisha panda mgongoni, nikafunikwa na shuka na safari ikaanza!![emoji32] [emoji32]
Sikujua naelekea wapi, nilishtukia tu nimefika mahali naskia sauti za watu. Ile nashangaashangaa, nkashtukia nimeshushwa chini na kukalishwa mahali(baadae nlikuja kugundua kuwa ni kitanda cha telemka tukaze), nilivyokalishwa juu ya kitanda, nilipigwa pini kwa miguu ambayo hadi leo naiheshimu.
Nkashtuka dushe inashikwa, kutahamaki! Ile naanza kulia..maaa...!![emoji15] Ngariba kamaliza. Haikuchukua muda nikapona tena bila bandeji wala plasta!
Naamini tupo wengi tuliopitia hii huduma bila ganzi. Nimekaa nikaona tutafutane ili ikiwezekana huu utaratibu tuupigie kelele urudi. Naamini hospitali ndio chanzo kikubwa cha mfumko wa vibamia na mashoga nchini! Karibuni.
swadakta mkuu maana tulikua kama 6 ktk kambi yetu.nyimbo za asili ukakamu ndio tiliokua tunafundiswa.kwenye msosi usipime mnaagaza chochote kinaletwa
 
nafikilia ata mwanangu mwezi wa 12.nimpeleke kwa babu yake kijijini akakutane na hiyo maana naisi hapa town anaweza pata kibamia ikawa aibu kwa wakwe zangu
 
Aisee hivi kumbe nyie mnaruhusiwa kutoa siri za jandoni,sisi mbona tunaambiwa kuwa ni mwiko kutoa siri za unyagoni? Kweli mfumo dume hautaisha Afrika.
Hakuna siri niliyotoa hapo, na wala hakuna niliposema nimeenda jando. Nimeongelea kukatwa bila ganzi, na ukataji sio lazima ufanane! Kuna waliokatiwa nyumbani bila ganzi, nalo ni jando?! Ningeelezea vitendo vilivyoendelea baada ya hapo, ingekuwa ndio nimetoa siri! Hata hivyo jando na unyago vinafundishwa mashuleni, kwahiyo wala hakuna cha ajabu hapo!
 
Back
Top Bottom