Vidume tuliopitia kwa ngariba bila ganzi tukutane hapa kukumbushana yale maumivu!

Duh! Nyie ndio mnakujaga kutoa hata Siri za jeshini...... Hamfai Kabisa...... She***zy
 
Dah kidume unakatwa halafu unalia? Huko kwetu kitendo cha kutingisha mguu tu wakati unakatwa ni udhaifu mkubwa

Kutoa siri za jandoni ni mwiko
 
Duh,, mambo ya aibu jamani.
 
Sisi kwetu hatuna utamaduni wa kutahiri asee. Mi nimejipeleka hospitali mwenyewe nikiwa na miaka 29, nimeoa tayari.
Nashangaa hizi project za tohara bure zimeng'ang'aniwa mikoa ya Iringa, njombe na mbeya wakati na wahaya hasa wakristo hawatahiri.
Jamaa yangu mhaya alikuwa JKT akasikia ukaguzi wa kwenda JWTZ lazima uwe umekatwa akaenda kukatwa.
Wahaya tubadilike
 
swadakta mkuu maana tulikua kama 6 ktk kambi yetu.nyimbo za asili ukakamu ndio tiliokua tunafundiswa.kwenye msosi usipime mnaagaza chochote kinaletwa
 
nafikilia ata mwanangu mwezi wa 12.nimpeleke kwa babu yake kijijini akakutane na hiyo maana naisi hapa town anaweza pata kibamia ikawa aibu kwa wakwe zangu
 
Aisee hivi kumbe nyie mnaruhusiwa kutoa siri za jandoni,sisi mbona tunaambiwa kuwa ni mwiko kutoa siri za unyagoni? Kweli mfumo dume hautaisha Afrika.
Hakuna siri niliyotoa hapo, na wala hakuna niliposema nimeenda jando. Nimeongelea kukatwa bila ganzi, na ukataji sio lazima ufanane! Kuna waliokatiwa nyumbani bila ganzi, nalo ni jando?! Ningeelezea vitendo vilivyoendelea baada ya hapo, ingekuwa ndio nimetoa siri! Hata hivyo jando na unyago vinafundishwa mashuleni, kwahiyo wala hakuna cha ajabu hapo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…