Mkuu nilisema humu kuwa kuna kila aina ya ukiritimba na urasimu katika majeshi hasa polisi na magereza wengi wakanitukana na kunikejeli kwenda polisi au magereza kwa msomi ni kujichoresha maana utaishi kulinda na kuagizwa kama mbwa.
Sasa mkuu!!,una masters ya nyuki,wakupandishe cheo haraka ili wakutumie kwenye nini labda?
Na ukumbuke pia mfumo wa vyeo vya polisi,unaanzia 1-15,namaanisha kama wakifuata kitabu chao kinavyosema kila kuruta aliyepo ccp leo baada 30yrs atakuwa senior super of polisi.wote watakuwa maafisa wakubwa wakifuatiwa na wadogo zao ambao watakuwa warakibu,litakuwa jeshi la maafisa sasa.ambalo halipo hata mbinguni.
Sasa embu niambie,leo una degree,unajiunga na jeshi la polisi,unataka kuanza tu uanze na nyota-then after 30 kutakuwa na maofisa wangapi hapo juu?,sababu wanakupa mshahara wa elimu yako,we kausha,othwerwise kama unapenda ubwana mkubwa,kama ukiona kutumwa noma JIAJIRI,maana mpaka bosi wa mabosi kuna mtu anamtuma.
Halafu nikwambie kitu.
Cheo kinachopanda kwa uzoefu wa kazi,ndio cheo kilichokusudiwa na muasisi wa jeshi,elimu ya darasani haina nafasi jeshini,ndio maana unaambiwa uiache getini ukianza kuburuzwa.piramid itazingatiwa hata kama we ni prof sababu umekuja leo lazima ujue kwanza guard ninini?then mengine jah aki bless.