Watoto wa Mkapa hawakukaa Oysterbay, walikaa sana Canada, US, briefly Nigeria baba yao alivyokuwa balozi, halafu Upanga / Sea View.
Utotoni tulikuwa tunaenda kwenye birthday parties zao, walikuwa wanalalamika sana mshua wao alikuwa anawakataza kunywa maji kabla ya kumaliza chakula. Walikuwa hawapendi sana.
Kuna siku moja tulikuwa tumekaa maskani Upanga.
Mara tukaona polisi kama ishirini wanakuja wamebeba marungu na bunduki.
Basi mimi nikawaambia madogo maskani, kama hujiamini, ondoka kabisa, hapa tunakuja kupewa dhahama na hawa polisi.
Basi, polisi wakafika maskani.
Mmoja akasema "Aisee, mnafanya nini hapa?"
Jamaa mmoja akawajibu "Afande, kwani hivyo ndivyo mlivyofundishwa kusalimu watu?"
Polisi akanywea, akawa kama anashangaa, huyu dogo anajiamini vipi kuniuluza hivi?
Basi mkuu wao akaanza kutuukuza, mmoja mmoja, wewe unakaa wapi? Basi mtu anamuonesha pale, mwingine anaulizwa hivyo hivyo, anaonesha pale.
Wakamfikia mchizi mmoja, wakamuuliza, wewe unakaa wapi? Akajibu "Kwa Benjamin".
Sasa yule polisi akawa kashangaa, akauliza kwa Benjamin, Benjamin gani?
Jamaa akamwambia "Benjamin huyo huyo wa Jamhuri ya Muungano, kwani kuna nani mwingine"?
Yule polisi akawa kama hajaamini, lakini kuna wenzake walikuwa wanamjua jamaa, wakamwambia ni kweli huyu huwa tunamuona kwa Mkapa tukienda kulinda.
Basi hapo hapo tukaona polisi wanabadilika kabisa. Yule kiongozi wao akasema "Aah, unajua wazee tunatambuana tu, hakuna tati,o, tunafahamiana tu".
Baadaye nasikia kile kijiwe walikipigia X kwenye ramani yao kituoni, wakimaanisha msiguse kijiwe hiki wanakaa watoto wa Mkapa hapa.
Nilifikiria sana kama kijiwe kingekuwa cha hohehahe wangetupa msala gani siku ile.