Vifo vya vijana hawa miaka 80 na early 90 huko ushuani, Oysterbay

Hili life kama movie
 
Magu alikua kama wengine tuu yani kulikua na Mawaziri wengi tuu Obay so haikua ajabu kumuona wala kuwa kama a family friends , baada ya kua raisi ndio akawa big deal .lol
Kuna siku mshua alimchana sana live Mkapa kuhusu ubinafsishaji. Kesho yake Magu - alikuwa waziri siku hizo- akampigia simu mshua wangu na kumpongeza sana akimwambia mshua wangu kwamba mshua alimchana Mkapa vizuri sana. Kwamba wengi wanataka kusema kama alivyosema mshua wangu, ila wanaogopa tu.Alikuwa anaonesha solidarity na mshua.

Maana yake Magu alikuwa hakubaliani na mambo mengi ya ubinafsishaji aliyofanya Mkapa, lakini hakuweza kupinga maamuzi ya baraza la mawaziri. Chinichini alikuwa anapinga.

Hii historia ngumu kuipata hata kwenye vitabu, tunaijua tulioishuhudia.
 
Oya nimecheka sana umepita mule mule le super dadaz.... nyenyeee le kokobanga boma yeee. Mmenielewa? [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mbona vifo kama hivyo vipo sana, hapo hakuna dalili ya sumu, ila ni pombe Kali kupitiliza hadi ini linashindwa kuchuja na kupasuka, ndio maana damu inatoka na Sio matapishi!! RIP, ila Kuna Jina lake kitaalamu
 
Dah, ndiyo hao hao Halima na Hamida.

Waarabu wamemchukua Lulu, halafu wanakuja kuchukua mpaka bandari [emoji28][emoji28][emoji28]
Mwarabu alimbeba jumla ila demu naye si mchezo, ndoa yao ilifungwa Kanisani St Peter na uarabu wake , Lulu si mchezo na ndugu wa Jamaa wakaja Bongo kwnye harusi hahahahaha
 
Oya nimecheka sana umepita mule mule le super dadaz.... nyenyeee le kokobanga boma yeee. Mmenielewa? [emoji23][emoji23][emoji23]
Yule hakua mtoto wa Obay wala Upanga, ndio sababu unaona tabia yake , alikua ana kuwa kama limbukeni fulani baada kupata umaarufu wa mtandaoni , ndugu zake walipo kula bata kama wa ushuani yeye alikua bado ana struggle na baadae alipo pata nafasi ndio akaanza fujo zake baada kujilazimisha kuzoea watu ., ziku zote mpenda bata akichelewa kula bata basi hata uzeeni ata kula bata kama a teenager ,ndio sababu unaona ile behavior haikua ya kawaida .
 
Ndio maan alipo shika nchi akawa chejia watu kibao , hahaa likau na agenda zake ila alikua n amezea tuu, alipo shika ndio aka toa makucha hahahahaahahha
 
Kuna wakati polisi waliletwa wengi Obay sana na ikawa wana kamata watu ovyo , sasa siku vijana wa OFC wakamatwa , waka wa wamesimamishwa barabarani , kidogo kuna gari ika simama, akashuka mama mmoja, akauliza kwanini hawa vijana wame kamatwa?, Police kwa dharau na akamjibu vibaya yule mama , kitu kam ali mpush yule mama , , yule mama aka soma number yake , kumbe kuja kukuta huyo mama ni Mama Warioba , kipindi hicho ndio Warioba ame kuwa Waziri mkuu , police hawakumjua , Sijui kilicho mkuta huko Oysterbay Police huyo police nasikia kitu kama ali vuliwa ranks or something.
 
Wazee zamani walikuwa hawajitangazi,sasa siku hizi watu kutwa kutembea na vitambulisho vyao vinaninginia shingoni
Nlikuwaga na watoto wa mosha wale twins wa kiume,forodhani
Mzee wao alifarikigi basi msiba ulikuwa mkubwa kweli

Ova
Kweli hiyo , maana wengie hata majirani zetu sikujua wanafaya kazi gani lol
 
OFC ilikuwa kama timu ya taifa, kuna siku Mzee Warioba alikuwa anakuja kuangalia watoto wanacheza mpira OFC.

Yani mnacheza mpira halafu Waziri Mkuu ka chill tu pembeni anawaangalia.

Kuna picha alipiga na timu nzima ya OFC niliiona kwa Gotta.

Mzee Warioba mtu poa sana alikuwa anakuja mpaka kwenye concerts za Reggae alizoandaa Gotta.

Halafu yule Mzee kwa misiba basi, yani humkosi ni kama ana kikosi maalum cha kumjulisha misiba yote anahudhuria.

Kuna siku kulikuwa na msiba wa mzee mmoja Msasani huku, nikamkuta Mzee Warioba kakaa kwenye jamvi anapiga stories na wazee wa Msasani msibani halafu yuko easy tu.
 
Ebwana itabidi unipe contact zake, nmetafute , sio kimapenzi ila tuu ni mjulie hali kama mwana Obay mwenzangu lol. nimefurahi sana kusikia yuko salama . ukionana naye msalimie sana mwambia kuna katoto kalikua kanakupenda sana zamani hahahahaha
Hahahaa Judy mtu mzima sana ujue. Kwa sasa ni bibi kabisa.

Ila sasa hivi hata ukimtafuta utakuwa safe maana kaka zake hawatokufanya chochote 😀
 
Mzee yule kweli hana makuu kabisa, mtu wa watu, nakumbuka kwnye Finals za league, ilifanyika hapo uwanja wa Obay Primry school ,OFC sijui na timu gani ilikua, Mgeni rasmi akawa Wariba na wazee wengine wakaja ku support watoto wao hapo, OFC ika shinda ila kutokana na points timu iliyo shindwa ndio ika chukua Kombe , tulijisikai kama aibu fulani . lol
 
Hahahaa Judy mtu mzima sana ujue. Kwa sasa ni bibi kabisa.

Ila sasa hivi hata ukimtafuta utakuwa safe maana kama zake hawatokufanya chochote 😀
Hahahahahaha najua atakua mtu mzima sana , sababu alikua ruka moja na cousin wangu ambaye alikua mkubwa sana , huyo souzin wangu alisha olew ana wajukuu ni Bibi sasa hivi, alisoma Kisutu, na yeye ndio alijua na mzimia Juddy akawa anaitania Mchumba wako Juddy lol
 
Jama hivi wale waarabu walio kuwa wana sponsor OFC ni walikua kina nani ? isije kuwa ndio hawa kina Ghalib GSM?
 
Ernest yuko wapi,
tulikuwa tunamwita "General Mwita Kiaro"
Hahaaa,

Mkuu wewe unamjua. Hilo jina la maskani kabisa wewe unazijua code.

Jamaa alikuwa anakuja maskani na Benzi la Ikulu.

Kiaro yuko wapi sijui siku hizi. Mara ya mwisho niliongea naye alikuwa Nairobi kwenye deal zake.

Kuna siku mshkaji wetu mmoja alikuwa na daladala lake, basi likakamatwa na Polisi. Likawekwa Oysterbay pale.Polisi walikuwa wanamzingua tu mshkaji wanataka hela.

Basi mshkaji akamwambia Kiaro, Kiaro ee, kuna Wamwera wananizingua huku, njoo useme nao.

Basi daah, Kiaro akanunua ile kesi mara moja.

Basi Kiaro akaenda na Benzi la Ikulu akapaki mlangoni pale Oysterbay Polisi.

Sasa si unajua mwana alivyopanda hewani, Kiaro hapo kipande cha mtu anapiga vyuma kama hana akili nzuri, halafu kapiga upara wake ule ameupaka mafuta unag'aa kama kioo, ana miwani ya jua ya kijasusi ile, juu kapiga T Shirt, chini ana Jeans kali, halafu kapiga buti la jeshi jeusiiii linang'ara.

Kaingia Oysterbay Polisi tu akaanza kuwaamrisha wale askari anawaambia "nataka mliachie hili daladala mara moja" yani hakuna majadiliano wala nini.

Wale Polisi kumuangalia tu wakawa wanaogopa, wanajiuliza huyu kiumbe ni nani, usalama wa taifa? Hii Benzi mbona kama ya Ikulu? Huyu jamaa kajiamini vipi kuingia kituo cha Polisi Oysterbay na buti za kijeshi? Huyu ni mwanajeshi au vipi?

Basi akaitwa mkuu wa kituo pale, yule mkuu wa kituo alikuwa anamjua Kiaro, akaanza kujichekesha chekesha lile daladala likatolewa mara moja.

Kiaro mtu poa sana, hana shobo wala mashauzi na mtu, mnakaa naye maskani mnapiga stories, jioni huyo anarudi Sea View anaenda kumnyoa nywele rais Benjamin Mkapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…